Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-12-28 19:15:39    
Kampuni za China barani Afrika zimekuwa ni daraja la kuongeza maelewano kati ya China na Afrika

cri

Kutokana na maendeleo ya kasi ya uhusiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na Afrika, kampuni nyingi zaidi na zaidi za China zimeanzisha shughuli zao barani Afrika kwenye fursa na changamoto. Wakati zinapojiendeleza na kuleta manufaa kwa sehemu za huko, kampuni hizo za China zimekuwa daraja la kuhimiza maelewano kati ya China na Afrika.

Kampuni ya ushirikiano wa kimataifa ya Sichuan China, ni moja ya kampuni za China zilizowekeza nchi za nje mwanzoni wakati China ilipoanza mageuzi na kufungua mlango. Maneja mkuu wa kampuni ya maendeleo ya Afrika ya kampuni ya ushirikiano wa kimataifa ya Sichuan China Bw. Li Jincheng alijulisha kuwa, kampuni hiyo ilianza shughuli zake barani Afrika mwaka 1981, katika miaka zaidi ya 20 iliyopita, kampuni hiyo ilifanya kazi ya ujenzi wa miradi mingi nchini Kenya, Tanzania, Zambia, na Uganda, na kusifiwa sana na wananchi wa huko.

    

Urafiki kati ya China na Afrika zina ulianza tangu enzi na dahari, lakini kwa kuwa ziko mbali sana, maelewano kati ya pande hizo mbili bado si ya kutosha. Bw. Li Jincheng alisema miaka kadhaa iliyopita, baadhi ya maofisa wa Kenya walikuwa wanaona China bado ni nchi maskini. Kwa mfano?miaka kadhaa iliyopita miji kadhaa nchini China ilitaka kujenga uhusiano wa kirafiki na mji wa Nairobi, lakini meya wa wakati ule wa mji wa Nairobi Bw. Akech alikataa matakwa hayo, alisema Nairobi ni mji mkuu ambao ni mwenyeji wa shirika la Umoja wa Mataifa. Mwaka 2003 kutokana na msaada wa kampuni ya ushirikiano wa kimataifa ya Sichuan, China, meya Akech alifanya ziara mjini Chengdu, mkoani Sichuan, China, mpango mzuri wa mji na miundo mbinu ya mji wa Chengdu vilimpa picha nzuri. Alisaini makubaliano mara moja na serikali ya mji wa Chengdu, na kuamua kujenga uhusiano wa kirafiki kati ya Nairobi na Chengdu. Baada ya kurudi mjini Nairobi, meya Akech pia alitoa azizo la kupanda maua na majani kwenye barabara kuu mjini Nairobi kama ilivyo ya ujenzi wa miji ya China.

Bw. Li Jincheng pia ni mkurugenzi wa shirika la uchumi na biashara la China nchini Kenya, alisema katika miaka kadhaa iliyopita, maoni ya wakenya kuhusu hali ya China yamebadilika sana, lakini bado kuna wachina wengi ambao hawalielewi vizuri bara la Afrika. Kampuni kubwa kadhaa za China bado zinaona kuwa Afrika ni bara maskini lenye migogoro, joto, na magonjwa, hivyo hazithubutu kwenda kuwekeza barani Afrika. Kihalisi baada ya kwenda Afrika kufanya uchunguzi, wanakampuni wengi wa China walibadilisha maoni hayo. Kampuni nyingi za China barani Afrika pia ziliwaambia watu wa China hali halisi ya Afrika kwa kupitia shughuli zao za kiuchumi na kibiashara.

Licha ya hayo, kampuni za China barani Afrika vilevile zinafanya juhudi kuwaandaa watu wenye ujuzi wa huko wanaojua utamaduni wa lugha ya Kichina. Tarehe 4 mwezi Desemba, kampuni ya ushirikiano wa kimataifa ya Sichuan, China ilitoa shilingi laki 4.8 za kikenya kwa chuo cha Confucius cha chuo kikuu cha Nairobi nchini Kenya, na kuwasaidia wanafunzi kutoka Kenya na nchi nyingine kujifunza lugha ya Kichina, baada ya kuhitimu kutoka chuo hicho, wanafunzi hao watapewa kipaumbele kuajiriwa na kampuni hiyo. Mkuu wa kampuni hiyo Bw. Lin Douming alisema, nia ya kutoa fedha kwa chuo cha Confucius ni kueneza utamaduni wa China, vilevile ni kuihimiza kampuni iajiri wafanyakazi wa huko.

Naibu mkuu wa chuo cha Confucius Bw. Sa Dequan alisema, ushirikiano kati ya kampuni za China na chuo cha Confucius unasaidia kutatua suala la ajira linalozikabili nchi za Afrika, wanafunzi wa chuo cha Confucius wanaweza kutumia elimu waliyopata, pia utahimiza maendeleo ya chuo cha Confucius. Vilevile ushirikiano huo unasaidia kampuni za China kuajiri wafanyakazi wa huko, na kuzisaidia kampuni hizo kuendelezwa vizuri zaidi barani Afrika.

Katika miaka zaidi ya kumi iliyopita, kampuni nyingi zaidi za China zilikwenda Zambia kuanzisha viwanda, kufanya kazi ya ujenzi, na kufanya biashara. Kampuni nyingi zilipata mafanikio makubwa, vilevile zilihimiza maendeleo ya uchumi wa huko.

Hadi sasa kuna kampuni zaidi ya 200 za China, na thamani ya uwekezaji nchini Zambia kutoka China imezidi dola za kimarekani milioni 600. China imekuwa ni nchi kubwa ya tatu inayowekeza nchini Zambia, baada ya Afrika Kusini na Uingereza. Zambia ina ardhi kubwa lakini ina watu wachache, ambayo ina mazingira mazuri yanayofaa kwa maendeleo ya kilimo. Lakini kutokana na sababu nyingi, katika muda mrefu uliopita Zambia ilikuwa na upungufu wa nafaka. Mashamba yaliyoanzishwa na China yalisaidia kwa ufanisi kupunguza tatizo la upungufu wa nafaka nchini Zambia.

China ilianza kuendeleza kilimo nchini Zambia tangu mwisho wa miaka ya 80 ya karne iliyopita. Hivi sasa kuna mashamba 15 yaliyowekezwa na China nchini Zambia, na mashamba hayo yote yanaendelezwa vizuri sana. Ni muhimu zaidi kuwa mashamba hayo yanaonesha umuhimu mkubwa katika utoaji wa nafaka nchini Zambia.

Shamba la urafiki la China na Zambia ni shamba la kwanza lililowekezwa na China nchini Zambia, mwaka 2005 idadi ya uzalishaji wa nafaka wa shamba hilo lilifikia tani elfu 37. Shamba hilo linakuwa na ufanisi zaidi ya asilimia 30 kwa mwaka, hata katika mwaka wa maafa, matumizi na mapato ya shamba hilo pia yanaweza kudumisha uwiano kwa kimsingi.

Nchini Zambia shamba la China linalojulikana sana ni shamba la Zhongken linaloendeshwa na kampuni kuu ya maendeleo ya kilimo ya China. Shamba la Zhongken limeajiri wafanyakazi 200 wa huko, na limefuga kuku laki 1.2, ng'ombe elfu moja, nguruwe elfu 2, na mayai yanayouzwa na shamba hilo yanachukua asilimia 10 kwenye soko la Zambia. Shamba hilo linaonesha umuhimu mkubwa zaidi katika utoaji wa vyakula nchini Zambia.

Licha ya hayo, sehemu ya ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na Zambia pia ni njia yenye ufanisi ya kuhimiza maendeleo ya uchumi wa huko.

Sehemu ya ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na Zambia, ni sehemu ya kwanza iliyoanzishwa na China barani Afrika. Tangu mwezi Februari mwaka 2007 sehemu hiyo ilipoanzishwa, idadi ya kampuni zilizoingia kwenye sehemu hiyo imefikia 12, na thamani ya jumla ya uwekezaji imezidi dola za kimarekani milioni 350.

Inakadiriwa kuwa kila mwaka sehemu hiyo inailetea Zambia thamani ya uuzaji yenye dola za kimarekani milioni 500, na mapato ya kodi ya dola za kimarekani milioni 10. Aidha, idadi ya nafasi za ajira zilizotolewa na sehemu hiyo hivi karibuni itafikia elfu 6, pia sehemu hiyo itawaandaa wafanyakazi wengi wa huko.