Tufanye juhudi kwa pamoja kusukuma mbele jitihada kubwa ya amani na maendeleo ya binadamu
Mabibi, Mabwana, Ndugu na Marafiki:
Kengele ya mwaka mpya itagonga sasa hivi, mwaka mpya 2008 umekaribia. Katika wakati huo uliojaa matumaini, nina furaha kupitia Radio China Kimataifa, Radio ya serikali kuu ya China na Kituo cha televisheni cha taifa CCTV kuwatakia furaha ya mwaka mpya wananchi wa makabila mbalimbali, ndugu wa mikoa ya utawala maalum ya Hongkong na Makau, ndugu wa Taiwan na ndugu wanaoishi ng'ambo, pamoja na marafiki wa nchi mbalimbali duniani.
Mwaka 2007, mabadiliko mapya yametokea duniani, ambapo China pia imepata maendeleo mapya. Wananchi wa makabila mbalimbali wa China wanajiunga kama kitu kimoja wakiendelea kusukuma mbele mchakato wa kujenga jamii yenye maisha bora kote nchini. Nguvu ya jumla ya China imeimarishwa zaidi, na maisha ya wananchi yameboreshwa zaidi. Wananchi wa China wanatilia mkazo mawasiliano na ushirikiano na wananchi wa nchi mbalimbali, kujitahidi kushiriki katika kushughulikia utatuzi mwafaka wa masuala makubwa yanayofuatiliwa duniani, kujitahidi kuhimiza juhudi za kujenga dunia yenye masikilizano iliyo ya amani na ustawi wa pamoja. Zaidi ya miezi miwili iliyopita, Chama cha Kikomunisti cha China kilitiisha mkutano mkuu wa 17, mkutano huo ulitoa mpango kabambe wa kuendelea kujenga jamii yenye maisha bora kote nchini katika hali mpya ya zama hizi, na kuharakisha ujenzi wa mambo ya kisasa ya kijamaa. Wananchi wa makabila mbalimbali wa China wenye bidii na busara wanachapa kazi kwa ajili ya kujenga maisha yao bora zaidi.
Kwa wananchi wa China, Mwaka 2008 utakuwa mwaka muhimu sana, tutaadhimisha kwa shangwe miaka 30 tangu tuanze kutekeleza sera ya mageuzi na kufungua mlango. Kufanya mageuzi na ufunguaji mlango kuanzia mwaka 1978 ni chaguo muhimu la kuamua mustakabali wa China katika zama za hivi leo, kutekeleza sera hiyo kumeifanya sura ya China inayofuata mfumo wa ujamaa ikutane na mabadiliko ya kihistoria, tutainua juu bendera tukufu ya ujamaa wenye umaalum wa kichina, kutekeleza kwa kina wazo la kujiendeleza kwa njia ya kisayansi, kuendelea kujikomboa kifikra, kushikilia mageuzi na ufunguaji mlango, kuendeleza uchumi wa soko huria?kuendeleza siasa ya demokrasia ya kijamaa, kuendeleza utamaduni wa kisasa wa kijamaa, katika kazi yetu ya kuimarisha ujenzi wa jamii, tutaendelea kuweka mkazo katika kuboresha maisha ya wananchi, na kuwawezesha wananchi wote wapate elimu, mapato yanayolingana na kazi zao, kupata matibabu wakiwa wagonjwa, wazee wapate malipo ya uzeeni, na watu wote wapate makazi, ili kuhimiza hali ya masikilizano kwenye jamii. Tutashikilia sera ya "nchi moja mifumo miwili" na kuwaacha wahongkong na wamakau waendeshe mambo yao wenyewe kwenye kiwango cha juu, na tutashirikiana na ndugu wa Hongkong na Makau katika kulinda pamoja ustawi na utulivu wa muda mrefu, kufuata barabara mambo makuu ya maendeleo ya amani ya uhusiano kati ya China bara na Taiwan, na kufanya juhudi bila kulegalega kwa ajili ya kuleta ustawi na neema kwa ndugu wa China bara na Taiwan na kuleta amani kwa pande mbili za mlangobahari wa Taiwan, na kulinda kithabiti mamlaka ya nchi na ukamilifu wa ardhi wa taifa. Hivi sasa hali ya jumla duniani ni ya utulivu, wakati huo hali isiyo ya uwiano inazidi kuongezeka katika uchumi wa dunia nzima, hali ya usalama wa kimataifa imekuwa na utatanishi zaidi, na binadamu wanakabiliwa na taabu na changamoto nyingi. Kunufaika pamoja na fursa ya maendeleo, kukabiliana pamoja na changamoto za aina mbalimbali, na kuhimiza jitihada kubwa za amani na maendeleo ya binadamu ni matumaini ya pamoja ya wananchi wa nchi mbalimbali. Kwa kutumia fursa hii, napenda kusisitiza kuwa China itainua juu bendera ya amani, maendeleo na ushirikiano, itashikilia bila kulegalega hata kidogo njia ya kujiendeleza kwa amani, kushikilia bila kutikisika mikakati ya kufungua mlango ili kufanya ushirikiano wa kunufaishana, kuendelea na juhudi za kuhimiza demokrasia katika uhusiano wa kimataifa, kuhimiza utandawazi wa uchumi duniani uendelee kuelekea kwenye hali ya uwiano, kunufaisha sehemu zote na kupata maendeleo ya pamoja, kuhimiza maingiliano na kufundishana kati ya ustaarabu wa binadamu, kulinda dunia hii ambayo binadamu inaitegemea kwa maisha yake, na kulinda amani na utulivu wa dunia.
Wakati huo tunawakumbuka watu wa sehemu mbalimbali duniani wanaoteseka sana katika vurugu za vita, umaskini, magonjwa na maafa. Wananchi wa China wanawahurumia sana kutokana na hali yao, wanapenda kuwasaidia kadiri wawezavyo ili wajiondoe kutoka kwenye hali taabani mapema iwezekanavyo. Tuna matumaini ya dhati wananchi wa nchi zote duniani waishi pamoja kwenye dunia hii yenye uhuru, usawa, masikilizano na heri na fanaka, ili kunufaika pamoja na matunda ya amani na maendeleo ya binadamu.
Michezo ya Olimpiki ya 29 ya majira ya siku za joto na Michezo ya Olimpiki ya walemavu itafanyika Mwaka 2008 mjini Beijing. Tutafanya juhudi kubwa zaidi kadiri tuwezavyo, ili kuifanya michezo hiyo ya Olimpiki iwe mkutano mkubwa wa kuongeza maelewano na ushirikiano wa kirafiki kati ya wananchi wa China na wa nchi mbalimbali duniani. Tunawakaribisha wachezaji hodari wa nchi mbalimbali duniani waje China kushiriki kwenye Michezo ya Olimpiki na Michezo ya Olimpiki ya walemavu, pia kuwakaribisha marafiki wa nchi mbalimbali waje China kutazama michezo ya Olimpiki na michezo ya Olimpiki ya walemavu.
Mwisho napenda kuwasalimu kutoka hapa Beijing na kuwatakia wote heri na baraka katika mwaka mpya wa 2008.
|