Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-01-02 19:45:30    
Mapishi ya matango ya baharini na pilipili hoho

cri

Mahitaji

Matango kumi ya baharini, pilipili hoho gramu 10, vipande vya vitunguu maji, mvinyo wa kupikia kijiko kimoja, sukari nusu ya kijiko, mchuzi wa sosi kijiko kimoja, maji ya wanga vijiko viwili, chumvi vijiko viwili.

Njia

1. osha matango ya baharini, halafu chemsha maji, tia matango ya baharini kwenye maji, halafu yapakue na uyakate yawe vipande.

2. washa moto, tia mafuta kwenye sufuria, tia vipande vya vitunguu maji, halafu tia matango ya baharini, korogakoroga, mimina mvinyo wa kupikia, tia sukari, mchuzi wa sosi, mimina maji ya wanga, baada ya kuchemka, tia pilipili hoho korogakoroga, tia chumvi korogakoroga, ipakue. Mpaka hapo kitoweo hiki kiko tayari kuliwa.