Tarehe 2 mwezi Januari mwaka 2008 ilikuwa siku ya kwanza kwa biashara ya mafuta ya petroli yatakayozalishwa kwenye soko la mafuta ya petroli duniani. Bei ya mafuta ya asili ya petroli yatakayozalishwa katika mwezi Februari katika siku hiyo ilipanda sana kwa kiasi cha kushangaza, hata ilizidi dola za kimarekani 100 kwa pipa, ambayo ni mara ya kwanza kutokea kwenye historia ya biashara ya mafuta yatakayozalishwa.
Siku hiyo, bei ya mafuta kwenye soko la dunia ilipanda kwa kiwango kikubwa, na ilifikia dola za kimarekani 100 kwa pipa katika saa 6 na dakika 6 kwa muda wa sehemu ya mashariki ya Marekani, bei hiyo mpya ilivunja rekodi ya juu ya dola za kimarekani 99.62 kwa pipa.
Katika siku hiyo, mafuta ya asili ya Brent ya bahari ya Kaskazini yatakayozalishwa mwezi Februari kwenye soko la mafuta la kimataifa la London, ilipanda kwa dola za kimarekani 3.99 na kufikia dola za kimarekani 97.84. Wachambuzi wanaona kuwa, kuna mambo mengi yaliyosababisha bei ya mafuta kupanda kwa kiwango kikubwa.
Kwanza, mgogoro wa nchini Nigeria, ambayo ni nchi inayotoa mafuta ya petroli kwa wingi barani Afrika, umesababisha wasiwasi mkubwa kwa wafanyabiashara wa mafuta. Watu wenye silaha nchini Nigeria, tarehe 1 mwezi Januari walishambulia sehemu muhimu inayozalisha mafuta ya nchi hiyo, na kusababisha vifo vya watu wengi. Nigeria ni nchi inayozalisha mafuta kwa wingi barani Afrika, na pia ni moja ya nchi muhimu zinazotoa mafuta kwa Marekani katika nchi za nje. Mgogoro wa nchini Nigeria ulikuwa sababu ya moja kwa moja ya kupanda kwa bei ya mafuta hadi kufikia dola 100 za kimarekani.
Pili, taarifa moja iliyotolewa na jumuiya ya OPEC terehe 2 mwezi Januari ilichangia kupanda kwa bei ya mafuta. Taarifa hiyo ilionya kuwa jumuiya hiyo itashindwa kukidhi mahitaji ya mafuta ya duniani kabla ya mwaka 2024.
Tatu, kushukiwa na soko la mafuta kupungua kwa akiba ya mafuta ya Marekani kwa shughuli za biashara katika wiki iliyopita, pia ilizidisha wasiwasi kwa wawekezaji. Wizara ya nishati ya Marekani tarehe 3 mwezi Januari itatangaza taarifa kuhusu akiba ya mafuta ya kila wiki. Wafanyabiashara wa masoko wanakadiria kuwa akiba ya mafuta ya shughuli za biashara ilipungua kwa kiasi cha mapipa milioni 1.7 katika wiki iliyopita.
Mbali na hayo, kuendelea kupungua kwa thamani ya dola za kimarekani siku hiyo katika kubadilisha fedha hizo kwa fedha muhimu za nchi za magharibi, kuendelea kupanda kwa bei ya dhahabu na bidhaa muhimu nyingine zitakazozalishwa kwenye masoko ya kimataifa, kufikia kipindi cha kutumia mafuta mengi katika kuleta joto majumbani katika majira ya baridi kwenye sehemu ya kaskazini ya dunia, na kuuawa kwa waziri mkuu wa zamani wa Pakistan Bi. Benazir Bhutto katika wiki iliyopita, ni mambo yaliyochangia kupanda kwa bei ya mafuta ya asili ya petroli.
Baadhi ya wachambuzi wanaona kuwa, mambo yote yaliyotajwa hapo juu, yalikuwa sababu za juu juu zilizochangia kupanda kwa bei ya mafuta, lakini chanzo muhimu cha kupanda kwa bei ya mafuta ni kukosa uwiano kati ya utoaji na ununuzi wa mafuta kwenye masoko ya kimataifa. Katika mwaka uliopita, bei ya mafuta duniani ilipanda kwa kiwango kikubwa, kutokea mwanzoni mwa mwaka jana, bei ya mafuta iliendelea kupanda kutoka dola za kimarekani 50 kwa pipa. Toka mwaka 2003, ongezeko la uchumi la dunia lilizidi 4% kwa mfululizo katika miaka minne iliyopita, na ni kipindi cha maendeleo ya kasi ya uchumi baada ya vita kuu ya pili ya dunia. Ingawa bei ya mafuta ilipanda kwa mfululizo, lakini kwenye msingi wa ongezeko kubwa la uchumi, mahitaji ya nchi mbalimbali kuhusu mafuta ya petroli yanaendelea kuongezeka. Shirika la nishati duniani linakadiria kuwa katika miaka michache ijayo, kutokana na ongezeko kubwa la uchumi duniani, mahitaji ya nishati duniani yataendelea kuongezeka.
Kuhusu mwelekeo wa bei ya mafuta ya petroli, wachambuzi wanasema, kutokana na kutoweza kubadilika kwa uwiano kati ya utoaji na ununuzi wa mafuta kwenye soko la kimataifa, hivyo hali ya kupanda kwa bei ya mafuta ni vigumu kubadilishwa katika muda mfupi ujao, mwaka huu bei ya mafuta itaendelea kuwa kubwa.
|