Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-01-04 18:54:35    
Wafanyakazi wa Afrika waonesha umuhimu mkubwa katika kampuni za China barani Afrika

cri

Katika miaka ya karibuni iliyopita, kutokana na upanuaji wa mawasiliano ya kiuchumi na kibiashara kati ya China na nchi za Afrika, kampuni nyingi zaidi na zaidi zimekwenda Afrika kufanya biashara. Kampuni za China zinaajiri wafanyakazi wengi wa huko barani Afrika, ili waweze kuonesha umuhimu wao. Si kama tu kampuni za China zimepata maendeleo kwa kutegemea wafanyakazi wa Afrika, bali pia wafanyakazi hao wa Afrika wamepata fursa za kuonesha uwezo wao katika kampuni za China.

Kampuni ya Huali?Cotec ya China kwenye nchi za Afrika ya mashariki inashughulikia uuzaji wa dawa ya malaria nchini Kenya, na kampuni hiyo ina wafanyakazi 21, kati yao kuna wachina watatu tu, wengine wote ni waafrika. Meneja mkuu wa kampuni hiyo Bw. Wang Wenqing alisema, kwa kupitia ushirikiano na wafanyakazi wa huko kwa miaka miwili, aliona kuwa wafanyakazi wa Afrika wanazoea hali halisi ya soko la huko na desturi za huko, hao ni wasiokosekana kwa maendeleo ya kampuni. Alisema waafrika wengi ni hodari na wenye bidii katika kazi

M-uganda Bw. Frances Akaya ni meneja wa idara ya kutoa mafunzo ya kampuni ya Huali-Cotec ya China kwenye nchi za Afrika ya mashariki. Yeye ana uwezo mkubwa wa kazi na anachapa kazi sana, kampuni yake inamuamini na kumwunga mkono sana. Mwaka 2007 kampuni hiyo ilimtuma nchini China kushiriki semina ya mafunzo ya mwezi mmoja, ili kumsaidia kujifunza njia ya usimamizi wa kampuni na utamaduni wa China.

Bw. Wang Wenqing alisema, baada ya kurudi nchini Kenya kutoka China, Bw. Akaya alijitahidi zaidi kufanya kazi. Amekuwa mfano mzuri kwa wafanyakazi wote wa kampuni hiyo, ambapo sifa ya kazi za wafanyakazi wote wa kampuni ikahimizwa na kuboreshwa. Aidha kongamano lililoendeshwa na Bw. Akaya pia lilisifiwa na madaktari ya huko nchini Kenya, na kuiletea sifa nzuri kampuni hiyo.

Katika miaka ya karibuni iliyopita, kampuni ya Huawei ya China ilipata maendeleo ya kasi barani Afrika, na ilianzisha ofisi nyingi barani Afrika. Idadi ya wafanyakazi wa kampuni ya Huawei barani Afrika imezidi elfu 2.5, kati yao asilimia 60 ya wafanyakazi ni wenyeji wa huko. Kampuni ya Huawei inaamua kuendelea kuajiri wafanyakazi wengi zaidi wa huko.

Mjumbe wa kampuni ya Huawei nchini Chad Bw. Liang Ting alisema, kampuni ya Huawei inataka kupata maendeleo kwa muda mrefu barani Afrika, hivyo inasisitiza kuheshimu wafanyakazi wa huko, na kuheshimu desturi za huko, ili kuweka mazingira yenye masikilizano ya kujiendeleza kwa kampuni. Bw. Liang Ting alisema, wafanyakazi wa Afrika si kama tu wanaweza kufanya vizuri kazi zao, bali pia wanaweza kuwalinda wafanyakazi wa China wakati wa hatari, na wamejenga urafiki mzuri na wafanyakazi wa China.

Mwezi Aprili mwaka 2006, mapinduzi ya kisiasa yalitokea nchini Chad, jeshi la upinzani la Chad lilishambulia N'Djamena, mji mkuu wa nchi hiyo. Usiku wa siku moja, jeshi la serikali la Chad na jeshi la upinzani yalitangaza kusimamisha mapambano kwa muda. Wakati huo kulikuwa na watu wengi waliokuwa wanafyatua risasi mitaani, wafanyakazi wawili wa huko wa kampuni ya Huawei walikwenda kwa pikipiki kwenye sehemu walipoishi wafanyakazi 18 wa China, kuongoza magari yaliyowachukua wafanyakazi wa China hadi kufikia kwenye mpaka kati ya Chad na Cameroon, wafanyakazi hao waliwasili Cameroon salama.

Wakati ule wafanyakazi wa China wa kampuni ya Huawei waliwaalika wafanyakazi hao wawili wa huko kwenda Cameroon ili kukwepa vita, lakini walikataa mwaliko huo. Wafanyakazi hao wawili wa Afrika walisema hawawezi kuondoka kutoka kwa nchi yao na familia zao, kama wafanyakazi wa China wakiondoka salama, wao hawatakuwa na wasiwasi.

Baada ya kukomeshwa kwa vita vya ndani vya Chad, wafanyakazi wa China wa kampuni ya Huawei walirudi nchini Chad, na wafanyakazi hao wa huko pia walirudi kwenye kazi zao, hivi sasa bado wanafanya kazi katika kampuni ya Huawei. China na nchi za Afrika zina tofauti kubwa ya lugha, utamaduni na jamii, pia wachina na waafrika wana mitazamo tofauti ya mambo. Wafanyakazi wa Afrika katika kampuni za China walijenga daraja la mawasiliano kati ya kampuni za China na idara za serikali na jamii za huko, na kampuni za China zilitoa fursa nyingi kwa wafanyakazi hao wa Afrika za kuonesha uwezo wao.

Kama wakitembea mitaani kwenye miji mikubwa nchini Tanzania, watu wengi watavutwa na majengo mapya ya hoteli na majengo ya ofisi. Karibu asilimia 50 ya majengo hayo yalijengwa na kampuni ya makundi ya ujenzi ya reli ya China nchini Tanzania.

Meneja mkuu wa kampuni hiyo Bw. Bao Qinglian alisema, yeye alikwenda Tanzania mwaka 1994, wakati ule kampuni hiyo bado ilikuwa ni kikundi cha ujenzi, na thamani ya biashara yake kwa mwaka haikufikia dola za kimarekani laki 3. Ingawa kikundi hicho kilikuwa na wafanyakazi zaidi ya kumi, lakini bado ilikuwa ni vigumu kuwalipa wafanyakazi hao.

Lakini hivi sasa kampuni hiyo ina wafanyakazi zaidi ya 200. Katika miaka ya hivi karibuni, thamani ya makubaliano ya kampuni hiyo kwa mwaka ilizidi dola za kimarekani milioni 50, na thamani ya biashara halisi kwa mwaka ilifikia dola za kimarekani milioni 25, pia inaongezeka kwa asilimia 20 kwa mwaka. Bw. Bao Qinglian aliona kuwa upashanaji habari, uhusiano mzuri, na marafiki wengi ni sababu za kupata mafanikio makubwa kwa kampuni hiyo barani Afrika.

Barani Afrika, kuajiri wafanyakazi wa huko ni hatua ya kawaida inayochukuliwa na kampuni za China. Hii si kama tu inaweka kupunguza gharama ya ajira, bali pia inakaribishwa na watu wa huko. Bw. Bao Lianqing alisema, kampuni ya makundi ya ujenzi ya reli ya China kila mwaka inaajiri watanzania zaidi ya elfu 5, hii si kama tu imeleta nafasi nyingi za ajira kwa watu wa huko, bali pia imewaandaa watu wengi wenye ujuzi kwa nchi hiyo.

Bw. Bao Lianqing alisema kampuni hiyo inafanya juhudi kuajiri wafanyakazi wengi zaidi, kampuni hiyo si kama tu imeajiri wafanyakazi wa huko kushughulikia kazi za kimsingi, bali pia imeajiri mhandisi wa huko kushughulikia usimamizi wa miradi na kazi ya kutathimini gharama za miradi. Bw. Bao Lianqing alisema hivi sasa kampuni hiyo inaendelezwa kwa kasi, siku za baadaye huenda itawekeza kwenye sekta nyingine, ili kupanua zaidi eneo la biashara la kampuni hiyo.