Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-01-07 14:49:00    
Kituo cha Taifa cha Sanaa za Maonesho chazinduliwa na kuanza kipindi cha kwanza cha maonesho ya usanii

cri

Baada ya ujenzi wa miaka kadhaa Kituo cha Taifa cha Sanaa za Maonesho cha China ambacho kinasifiwa kuwa ni alama ya karne ya 21 nchini China, kilizinduliwa rasmi tarehe 22 Desemba mwaka 2007 na kuanza kipindi cha miezi mitatu ya maonesho ya usanii.

Jioni ya tarehe 22 kituo hicho kilichojengwa kama umbo la zeituni kilichopo kwenye upande wa magharibi wa uwanja wa Tian An Men mjini Beijing kilionekana kama mbingu ya samawati, na taa zilizopangwa kwenye sura yake zilikuwa kama nyota, na ziwa lililochimbwa na zunguka kituo hicho linametameta, na kivuli cha kituo hicho kilichoungana na kituo chenyewe kilikuwa kitu kizima kinachoonekana kama kioo ndani ya maji. Tokea siku hiyo katika muda wa miezi mitatu ijayo wasanii wa nchini na kutoka nje ya China watafanya maonesho ya usanii zaidi ya 180, kati ya maonesho hayo, muziki uliooneshwa kuanzia 22 hadi tarehe 24 ni maonesho ya ufunguzi wa kituo hicho, ambayo yote yataoneshwa na wanamuziki mashuhuri duniani. Msimamizi wa sanaa wa kituo hicho Bw. Chen Zuohuang alisema,

"Wazo la kutaka kujenga kituo hicho lilianza miaka 50 iliyopita, watu waliokuwa na matumaini makubwa ya kujengwa kwa kituo hicho ni wasanii wa China, kwani kituo hicho kitaleta nguvu kubwa ya kusukuma mbele utamaduni na usanii wa China. Baada ya kituo hicho kukamilishwa, muziki kwenye uzinduzi wa kituo hicho ulitokana na uchaguzi mkali ili kuonesha kiwango cha usanii wa China."

Mliosikia ni muziki wa fidla nne, wapigaji wanne wote waliwahi kupata tuzo katika mashindano ya kimataifa ya muziki wa fidla ya Paganini nchini Italia. Mmoja kati ya hao Bw. Lu Siqing alisema,

"Maonesho ya muziki kwenye uzinduzi wa Kituo cha Taifa cha Sanaa za Maonesho sio tu yanatarajiwa sana na watu wa China, lakini hata wapenda muziki wa nchi za nje. Ni matumaini yangu kuwa muziki uliooneshwa katika uzinduzi huo utawapatia kumbukumbu za daima."

Tokea China ianze kutekeleza sera ya mageuzi ya kiuchumi, uwezo wa taifa unaimarika haraka, kituo hicho kimejengwa ili kulingana na maendeleo ya jamii ya China na kukidhi mahitaji ya kiutamaduni ya wananchi. Kituo hicho kilianza kujengwa mwaka 2001, licha ya sura yake ambayo ilisanifiwa na Mfaransa Bw. Paul Andreu, kazi ya ujenzi wake pia ilikuwa ni changamoto kubwa. Mkuu wa uhandisi wa ujenzi wa kituo hicho Bw. Peng Chengjun alisema, umbo la kituo hicho ni kama zeituni, nafasi yake ndani ni kubwa kuliko majumba yote duniani, na paa lake pia ni kubwa kabisa nchini China. Alisema,

"Fremu ya paa la jengo hilo ni ya chuma cha pua, ambayo eneo lake ni mita za mraba elfu 25.5. Fremu ya paa kubwa kama hiyo inawezaje kujengwa? Mshauri mmoja wa serikali ya Beijing alisema, alishughulika na kazi ya ujenzi kwa miaka 53 lakini hakuwahi kujenga paa kubwa na nzito kama hili linalotatanisha kwa maboriti mengi."

Ujenzi wa kituo hicho ulikamilishwa kwa miaka sita, jengo juu ya ardhi lina urefu wa mita 47, na jengo chini ya ardhi ni mita 33. Sehemu ya ndani ya jengo hilo ilijengwa kwa teknolojia ya kisasa, na inaonesha usanifu wa mtindo wa Kichina na wa kisasa. Mmoja wa wasanifu wa kituo hicho Bw. Chen Youjian alisema,

"Kabla ya kituo hicho kukamilishwa nilikuja Beijing mara kadhaa kuangalia kazi zilivyoendelea, ingawa sura yake bado haikuwa wazi lakini ilinivutia sana. Nikiwa Mchina najivunia jengo hilo."

Kituo cha Taifa cha Sanaa za Maonesho ikiwa ni pamoja na ukumbi wa michezo ya sanaa, ukumbi wa muziki na ukumbi wa opera na michezo ya kuigiza, kina viti 5,400 vya watazamaji. Ukumbi wa michezo ya sanaa ni jengo la fahari zaidi. Ukumbi wa muziki unaonekana wenye mzingira ya kistaarabu na kimya. Kinanda cha ogani chenye paipu za sauti 6,500 ni kikubwa kabisa nchini China, ambacho kinaweza kukidhi mahitaji ya aina zote za muziki. Kumbi zote hizo ni matokeo ya muungano wa uzuri wa ujenzi na elimu ya sauti. Mtazamaji Bi. Li Yun alisema,

"Kumbi hizo zilijengwa kwa umakini sana, sauti haipotei hata kidogo kutokana na usanifu mzuri wa paa na ukuta. Nadhani watu wote wakija watastaajabu."

Maonesho ya muziki kwenye uzinduzi wa kituo hicho yamewavutia watu wengi duniani. Mwimbaji Placido Domingo wa Hispania na idara nyingi za wasanii zilituma barua za pongezi, vituo vya televisheni vya Marekani, Ujerumani, Uingereza na Japan vitarekodi muziki wa kusherehekea mwaka mpya, na wasanii wengi wanataka kuonesha michezo yao katika kituo hicho. Msimamizi mkuu wa sanaa wa kituo hicho Bw. Chen Zuohuang alisema, kituo hicho kitatumika vya kutosha. Alisema,

"Kituo cha Taifa cha Sanaa za Maonesho ni jukwaa la wasanii wa China na huku pia ni jukwaa kubwa la maingiliano ya kiutamaduni kati ya China na nchi za nje, na zaidi ya hayo kituo hicho kina wajibu wake mkubwa wa kutoa na kueneza elimu ya sanaa miongoni mwa wananchi."

Bw. Chen Zuohuang alisema, kituo hicho kimeanzisha ofisi ya uenezi wa elimu ya sanaa, kutokana na mpango kila mwaka kitaandaa semina mia kadhaa. Naibu waziri mkuu wa zamani Bw. Li Lanqing kwenye semina ya kwanza alitoa mhadhara unaoitwa "Muziki, Sanaa na Maisha ya Binadamu".

Idhaa ya kiswahili 2008-01-07