Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-01-07 18:53:01    
Mkutano wa dharura wajadili msukosuko wa kisiasa wa Lebanon na hali ya Palestina na Israel

cri

Mkutano wa dharura wa Umoja wa nchi za kiarabu ulifanyika tarehe 6 huko Cairo, ambapo mawaziri wa mambo ya nje au wawakilishi wa nchi wanachama wa Umoja wa nchi za kiarabu, walijadili msukosuko wa kisiasa wa Lebanon na kuanzisha upya mazungumzo ya amani kati ya Palestina na Israel.

Ili kukomesha msukosuko wa kisiasa wa Lebanon, azimio lilipitishwa kwenye Mkutano huo kuhusu mpango wa utekelezaji na limeweka kanuni ya kupiga hatua tatu, yaani kuzitaka pande husika mbalimbali za Lebanon ziafikiane mapema iwezekanavyo kuhusu uchaguzi wa rais, kumchagua amri jeshi mkuu wa jeshi la Lebanon Bw. Michel Suleiman kuwa rais mpya kwa mujibu wa katiba ya Lebanon; iundwe mara moja serikali ya muungano wa kitaifa; kutunga mswada mpya kuhusu sheria mpya ya uchaguzi baada ya kuchaguliwa kwa rais na kuundwa kwa serikali ya muungano wa kitaifa.

Kutokana hali ya hivi sasa, makundi mawili yanayopambana ya Lebanon yote yanafurahia azimio hilo. Kiongozi mmoja wa kundi la watu wengi kwenye bunge la Lebanon ambaye pia ni kiongozi wa chama cha siku za mbele cha Lebanon Bw. Saad al Hariri alisema, azimio hilo limeonesha msimamo wa kuwajibika wa Umoja wa nchi za kiarabu, ambalo limewapa walebanon nguvu ya kujikwamua kutoka kwenye hali taabani ya hivi sasa na kufungua hali mpya. Na kiongozi mmoja wa kundi la upinzani la Lebanon ambaye pia ni spika wa bunge la nchi hiyo Bw. Nabeet Baria alisema, mawaziri wa mambo ya nje wa nchi za kiarabu wamechukua msimamo wa kihistoria kwa ajili ya maslahi ya Lebanon.

Wachambuzi wanaona kuwa, kundi la watu wengi na kundi la upinzani nchini Lebanon yanafurahia azimio hilo ni kwa sababu azimio hilo limekidhi ufuatiliaji wa kila upande, kwamba mpango utatekelezwa hatua kwa hatua, hii inakidhi matakwa ya kundi la watu wengi; na azimio hilo linazitaka pande husika ziunde serikali ya muungano wa kitaifa, hii huenda italiwezesha kundi la upinzani lipate fursa nyingi za kushiriki kwenye utoaji wa sera wa serikali. Syria pia imekubaliaana na azimio hilo. Waziri wa mambo ya nje wa Syria Bw. Walid Muallem tarehe 6 huko Cairo alisisitiza kuwa, azimio hilo ni mpango wa kutatua kikamilifu msukosuko wa Lebaon, pia alisisitza kuwa, Suala la Lebanon lazima litatuliwe kwa kuwategemea wananchi wa Lebanon kutimiza maafikiano.

Kutokana na mpango uliowekwa, Mkutano wa bunge la Lebanon utaitishwa tena tarehe 12 ili kumchagua rais. Hivyo Mkutano uliofanyika tarehe 6 umeweka mazingira mazuri kwa ajili ya uchaguzi wa rais, na kuwapa watu matumaini mapya kuhusu uchaguzi wa rais na kutatua msukosuko wa kisiasa.

Mada muhimu nyingine ya mkutano huo ni kujadili hali ya Palestina na Israel. Mkutano wa kimataifa kuhusu Suala la mashariki ya kati uliofanyika mwishoni mwa mwezi Novemba mwaka jana nchini Marekani, uliamua kuanzisha upya mazungumzo ya amani kati ya Palestina na Israel, baada ya hapo mazungumzo hayo yamekumbwa na taabu kutokana na Israel kutangaza kupanua ujenzi wa makazi. Kama alivyosema mwenyekiti wa mamlaka ya utawala wa Palestina Bw. Mahmoud Abbas, Suala la makazi ni kikwazo kikubwa cha mazungumzo ya amani kati ya pande hizo mbili.

Kuhusu Suala hilo Mkutano uliofanyika tarehe 6 umepitisha mswada wa azimio la kuitaka serikali ya Israel ichukue hatua ya kusimamisha ujenzi wa makazi, na kutekeleza utaratibu husika wa usimamizi uliofikiwa kwenye Mkutano wa kimataifa. Mswada huo wa azimio ulisema, vitendo vya Israel kuendelea kupanua ujenzi wa makazi, na kushambulia Gaza, vitaweza tu kuharibu matokeo yaliyopatikana kwenye Mkutano wa Annapolis kuhusu kuanzisha upya mazungumzo ya amani kati ya Palestina na Israel. Ingawa kabla ya Mkutano wa tarehe 6, Misri, Jordan na Saudi Arabia zimesema zinapinga Israel kupanua ujenzi wa makazi, na kusema hatua hiyo haisaidii mchakato wa mazungumzo ya amani kati ya Palestina na Israel, lakini mswada wa azimio uliopitishwa kwenye Mkutano huo wa dharura umeonesha msimamo wa pamoja wa nchi zote 22 za wananchama wa Umoja wa nchi za kiarabu, hakika hii italeta shinikizo kwa Israel. Kufanyika kwa wakati kwa Mkutano huo kunatokana na juhudi nyingi zilizofanywa na nchi za kiarabu ili kuimarisha mshikamano na ushirikiano.