Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-01-11 16:45:11    
Matibabu ya kichina yatoa mchango kwa waafrika

cri

Bw. Barrows anayefundisha kwenye chuo kikuu nchini Angola anasumbuliwa na ugonjwa wa shinikizo la damu na kisukari, na amekuwa akitibiwa kwa miaka mingi lakini hakupona. Hivi karibuni, alisafiri kwenda mbali ili kutibiwa na daktari Sun Qingfu kwenye kliniki ya matibabu ya kichina, huko Johannesburg nchini Afrika ya Kusini.

Bw. Barrows alikwenda kutibiwa na Daktari Sun kutokana na kushauriwa na rafiki yake. Rafiki huyo alipona kidhahiri baada ya kutibiwa na Daktari Sun. Kuna madaktari watatu kwenye kliniki ya Daktari Sun, na wanatumia njia mbalimbali kutoa matibabu ya jadi ya kichina, ikiwemo tiba ya akyupancha, dawa za mitishamba na njia ya kukanda mwili.

Baada ya kuondoka kwa Bw. Barrows, ilikuwa imekaribia saa tisa alasiri. Lakini Daktari Sun alikuwa hajapata chakula cha mchana. Alimwambia mwandishi wa habari kuwa, kila siku watu zaidi ya 20 wanakwenda kutibiwa kwenye kliniki yake na wengi ni wenyeji wa Afrika kusini, lakini pia kuna watu kutoka nchi za nje kama Bw. Barrows.

Tangu mwaka 2001 matibabu ya kichina yalipopewa idhini ya kutolewa nchini Afrika ya Kusini, matibabu hayo yaliendelezwa kwa haraka, sasa kuna kliniki zaidi ya 50 zinazotoa matibabu ya kichina huko Johannesburg. Takwimu za wizara ya afya ya Afrika ya Kusini zinaonesha kuwa, hivi sasa kuna madaktari 1000 wanaotoa matibabu ya kichina walioandikishwa nchini Afrika ya Kusini, wakiwemo madaktari wa matibabu ya kimagharibi wanaotumia njia ya matibabu ya kichina. Mwenyekiti wa kamati ya taalamu ya madaktari wa matibabu ya kiasili ya Afrika ya Kusini Bw. Cokana alisema matibabu ya kichina yameenezwa nchini humo siku hadi siku.

Kwenye bara zima la Afrika, matibabu ya kichina pia yanaonesha kazi yake katika kuwatibu watu. Tangu miaka ya 1960 ya karne iliyopita, China ilituma vikundi vingi vya madaktari barani Afrika, wakiwemo madaktari wengi wa matibabu ya kichina. Waafrika wanafahamu na kupenda matibabu ya kichina kutokana na bidii na ustadi wa matibabu wa madaktari wa China. Katika nchi nyingi barani Afrika, kutoka marais hadi raia wote wanapenda kupewa matibabu ya kichina, hasa wanapenda kutibiwa kwa tiba ya akyupancha.

Madaktari wa China waliotumwa barani Afrika pia walisaidia kuwaandaa madaktari wa huko kutoa matibabu ya kichina. Kutokana na sifa ya matibabu ya kichina, kuanzia miaka ya 1960 ya karne iliyopita, wanafunzi zaidi ya 1000 wa Afrika walikuja China kujifunza matibabu ya kichina, baadhi yao walipata shahada za uzamili au udaktari.

Matibabu ya China yalionesha kuwa na ufanisi dhidi ya magonjwa ya kuambukiza barani Afrika. Nchini Tanzania, kutibu ugonjwa wa ukimwi kwa njia ya kichina kumekuwa kunafanyika kwa miaka 20, na wagonjwa zaidi ya 10,000 walioambukizwa virusi vya ukimwi wanatibiwa. Kwa kutibu ugonjwa wa malaria, dawa ya aoteexin iliyotengenezwa kwa mitishamba ya kichina inatumiwa kwa wingi nchini Kenya na Burundi. Aidha, ikilinganishwa na matibabu ya kimagharibi, matibabu ya kichina ni ya bei ya chini. Kwenye kliniki ya daktari Sun, bei ya matibabu ya kichina ni asilimia 10 ya malipo ya matibabu ya kimagharibi.

Katika miaka ya karibuni, nchi nyingi za Afrika zimekuwa zinataka kupanua kiwango cha matibabu ya kichina nchini humo. Serikali ya Tunisia imesema inapenda kupanua ushirikiano na China katika matibabu ya kichina na kutaka kupanua kituo cha tiba ya akyupancha ambacho ni kikubwa kabisa barani Afrika kuwa kituo cha matibabu cha kichina.

Lakini ingawa matibabu ya kichina yanakaribishwa kwenye nchi nyingi za Afrika, lakini pia kuna upungufu wa madaktari wazuri wa matibabu ya kichina kwenye nchi kadhaa. Kwa hivyo daktari Sun anajianda kuanzisha shule ya matibabu ya kichina huko Johannesburg ili kuandaa watu wenye ujuzi wa kutoa matibabu ya kichina.

Habari nyingine zinasema mawasiliano kati ya China na Afrika katika sekta za uchumi na biashara yanaimarishwa siku hadi siku, na China imekuwa mwenzi mkubwa wa tatu kibiashara kwa Afrika. Thamani ya biashara kati ya China na Afrika kwa mwaka 2006 ilifikia dola za kimarekani bilioni 55.5. Takwimu kutoka wizara ya biashara ya China zinaonesha kuwa hadi kufikia mwishoni mwa mwaka 2006, China ilikuwa imewekeza dola za kimarekani zaidi ya bilioni 6.6 barani Afrika kwa ujumla katika kilimo, mawasiliano, nishati na utengenezaji. Mawasiliano ya kiuchumi na kibiashara kati ya China na Afrika yanayoimarishwa siku hadi siku, yanatoa mchango mkubwa kwa maendeleo ya Afrika.

Bidhaa za China ni za bei nafuu na zina sifa nzuri, hivyo bidhaa za China zimechangia soko la bidhaa barani Afrika na kuwanufaisha wateja wa Afrika. Naibu mkurugenzi wa shirikisho la wafanyabiashara wachina wanaoishi nchini Angola Bw. Li Jishe alieleza kuwa kutokana na kiwango cha chini cha shughuli za utengenezaji, shati la kawaida liliwahi kuuzwa kwa bei ya dola 50 za kimarekani nchini Angola, hata wakati fulani hawakuweza kupata bidhaa wanazohitaji japo walikuwa na fedha. Lakini kutokana na kuingizwa kwa bidhaa za China, sasa bei ya shati moja ni dola za kimarekani 5 tu.

Biashara kati ya China na Afrika imesukuma mbele ongezeko la uchumi wa Afrika kwa kiwango kikubwa. Mwaka 2006 ongezeko la uchumi wa Afrika lilifikia asilimia 5.5, nguvu muhimu ya kuhimiza ongezeko ilitokana na soko la kimataifa hasa mahitaji ya China. Wataalamu wanakadiria kuwa, hivi sasa kiasi cha mchango unaotolewa na biashara kati ya China na Afrika kwa uchumi wa Afrika umefikia asilimia 20.

Ushirikiano kati ya China na Afrika katika ujenzi wa miundo mbinu una umuhimu mkubwa. Kuanzia mwaka 2000, makampuni ya China yalijenga barabara zenye urefu wa kilomita zaidi ya 6000 barani Afrika, reli yenye urefu wa zaidi ya kilomita 3000, vituo vinane vikubwa na vyenye ukubwa wa kati vya kuzalisha umeme ili kuzisaidia nchi za Afrika kupunguza gharama za ujenzi wa miradi hiyo, na kuongeza uwezo wa kujiendeleza wa nchi za Afrika katika ujenzi wa uchumi. Makampuni ya China pia yalijenga shule na hospitali kwa nchi za Afrika.

Uwekezaji wa China barani Afrika umeinua kiwango cha teknolojia kwa nchi za huko. Katika sekta ya kilimo, China ilianzisha semina za mafunzo kwa ajili ya kusaidia Afrika kuendeleza teknolojia ya kilimo, pia serikali ya China iliahidi kuanzisha vituo 10 vya vielelezo vya teknolojia ya kilimo barani Afrika ndani ya miaka mitatu, na kutuma wataalamu 100 wa kilimo. Katika upande wa mawasiliano ya simu, makampuni ya China, ikiwemo kampuni ya Huawei ya China yalisaini kumbukumbu za maelewano na shirikisho la mawasiliano ya simu la kimataifa na kutoa mipango mingi ya kuwaandaa mafundi.

Aidha makampuni ya China yalikwenda kujiendeleza barani Afrika na kutoa nafasi nyingi za ajira kwa watu wa Afrika. Miongoni mwa wafanyakazi zaidi ya 2500 wa kampuni ya Huawei barani Afrika, 60% ni wenyeji, na miongoni mwa wafanyakazi 230 wa kampuni ya maendeleo ya Haixin nchini Afrika ya Kusini, 90% ni wenyeji wa huko.

Makampuni ya China yanashiriki kwenye ujenzi wa uchumi wa Afrika na kutoa mchango mkubwa katika kutekekeleza wajibu wa jamii. Nchini Sudan, kampuni ya gesi na mafuta ya China ilisaidia kujenga hospitali na kujenga miundo mbinu, ikiwemo madaraja, uwanja wa ndege na barabara. Takwimu zinaonesha kuwa katika miaka kumi iliyopita, kampuni hiyo imewekeza dola za kimarekani milioni 32.28 kwa ajili ya mambo ya umma ya jamii ya Sudan na kuwanufaisha watu zaidi ya milioni 1.5.

Idhaa ya kiswahili 2008-01-11