Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-01-09 18:00:36    
Mapishi ya vipande vya mzizi wa yungiyungi

cri

Mahitaji Mzizi mmoja wa yungiyungi, pilipili hoho gramu 10, vitunguu saumu gramu 5, chumvi kijiko kimoja, sukari kijiko kimoja, siki vijiko viwili, mchuzi wa sosi nusu kijiko

Njia:

1. kata mzizi wa yungiyungi uwe vipande, halafu weka vipande kwenye maji, kasha katakata pilipili hoho iwe vipande.

2. washa moto, tia mafuta kwenye sufuria, halafu tia vipande vya pilipili hoho, vitunguu swaumu, korogakoroga, halafu tia vipande vya mzizi wa yungiyungi, korogakoroga, tia chumvi, mchuzi wa sosi, siki na sukari, korogakoroga, halafu ipakue. Mpaka hapo kitoweo hiki kiko tayari kuliwa.