Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-01-10 15:51:34    
Mgeni anaifanya China maskani ya pili

cri

Ingawa Bibi Shizuko ana umri zaidi ya miaka 70, lakini yeye anaonekana na afya nzuri na mwenye nguvu kubwa anapokuwa darasani. Anafundisha wanafunzi wake kwa makini, na wanafunzi wanampenda sana. Kila baada ya masomo, anaimba nyimbo pamoja na wanafunzi wake, ili kupunguza uchovu.

Mwanafunzi mmoja He Hongtan alisema,

"Bibi Shizuko anatutendea vizuri, tunapoongea naye huwa tunafurahi."

Mwanafunzi mwingine Li Meng alisema,

"ufundishaji wake unavutia sana, na anafuatilia sana wanafunzi wake."

Mwanafunzi Huang Jingdong alitathimini Bibi Shizuko akisema,

"yeye ni mwalimu mzuri. Ingawa anaonekana kama mpole, lakini wakati fulani yeye huwenza kuonesha utundu wake. Wakati tunapozungumza naye anapenda kutuchekesha, sisi tunapenda kuzungumza naye."

Baada ya kazi, Bibi Shizuko pia anawafundisha vijana lugha ya kijapan, na wakati mwingine wanamaliza masomo yao baada ya saa 4 usiku. Wakati huo huo, Bibi Li Huiqun na mume wake wanatoa huduma kwa wanafunzi hao, kuwapatia chai na kuwapikia. Ingawa walikuwa na maoni tofauti katika maisha yao, lakini kutokana na maelewano kati yao, wanaheshimiana na kukubaliana.

Bw. Xie alisema,

"Tulimtendea kama dada yetu mkubwa, kwa sababu yeye ana umri mkubwa kuliko sisi. Maelewano kati yetu yanaweza kuondoa maoni ya tofauti. Tunaweza kuishi kwa pamoja vizuri zaidi."

Wakati Bibi Shizuko aliporudi nyumbani kwa muda, mjukuu wa kiume wa Bibi Li Huiqun alimwuliza, Bibi Shizuko atarudi nchini China lini? Na bibi Shizuko pia alisema kama akiwezekana, anapenda kuishi nchini China daima. Bibi Shizuko alisema,

"Sijui kwa nini ninapenda Chengdu. Ninapenda vyakula vya Sichuan, na wapenda zaidi watu wa Chengdu na mji huo."

Lakini Bibi Shizuko anakumbwa na matatizo ya kiuchumi na afya, na mwaka 2008 atarudi Japan. Alipozungumzia mambo hayo alikuwa na masikitiko sana. Alisema,

"Ingawa nilisema baada ya kufariki dunia nitazikwa nchini China, lakini ni vigumu kufanya hivyo kutokana na hali halisi. Na sasa matumaini yangu makubwa ni kuishi mjini Chengdu kwa muda mrefu zaidi, na kuwafundisha vijana wa Chengdu lugha ya kijapan.

Idhaa ya kiswahili 2008-01-10