Waziri wa mambo ya nje wa Israel Bi. Tzipi Livni na waziri mkuu wa zamani wa Palestina Bw. Ahmed Qureia tarehe 14 walifanya mazungumzo huko Jerusalem kuhusu masuala ya msingi yakiwemo hatma ya Jerusalem, kurudishwa kwa wakimbizi wa Palestina na mpaka wa Palestina baada ya kuwa nchi. Mazungumzo hayo kwa mara ya kwanza yaligusia masuala hayo ya msingi tokea mazungumzo yalipoanza tena mwezi Desemba mwaka uliopita.
Mazungumzo yalifanyika kwa muda wa saa mbili, na pande mbili zilifia makubaliano kuhusu masuala mawili tu, moja ni kuwa mazungumzo yatafanyika kila wiki kama ikiwezekana, pili ni kuwa ili kuhakikisha mazungumzo yasiingiliwe kati habari kuhusu mazungumzo hayo hazitakiwi kuvuja. Licha ya mambo hayo mawili mazungumzo hayakufikia makubaliano yoyote. Wachambuzi wanaona kuwa ni kawaida kwa mazungumzo hayo kutopata maendeleo yoyote baada ya pande mbili kugusia masuala ya msingi.
Kwanza, mvutano wa masuala yanayohusiana moja kwa moja na maslahi ya pande mbili umekuwa ni wa muda mrefu, kwa hiyo utatuzi wa matatizo hayo ni wa kutatanisha sana. Ili kuondoa vizuizi kwenye mazungumzo hayo, Rais Goerge Bush amemaliza ziara yake nchini Israel na Palestina hivi karibuni, lakini Bw. George Bush alihimiza tu pande mbili zifanye mazungumzo kuhusu masuala ya msingi na kujitahidi kufikia makubaliano kabla ya yeye kuondoka madarakani, lakini msimamo wake kuhusu masuala hayo haukuwa wazi, kwa hiyo hakuna kanuni yoyote inayoweza kufuatwa kwenye mazungumzo hayo. Tofauti imetokea tena kuhusu madhumuni tofauti ya kufanya mazungumzo yaliyotokea kabla ya mkutano wa Annapolis wa amani ya Mashariki ya Kati. Kwa mujibu wa ofisa wa Israel, madhumuni aliyotaka Ehud Olmert ni kutafuta makubaliano ya kimsingi na Palestina kuhusu kuanzisha nchi kamili, lakini makubaliano ni lazima yaahirishwe mpaka wakati ambapo Palestina inaweza kuhakikisha usalama wa Israel, lakini Bw. Abbas alitaka pande mbili zifikie makubaliano ya amani na kuiwezesha Palestina kuwa nchi kamili mwishoni mwa mwaka 2008 wakati uliowekwa na Rais George Bush. Katika hali ambapo pande mbili zinatofautiana kuhusu madhumuni ya kufanya mazungumzo, mazungumzo hayo ya mara ya kwanza hakika hayawezi kupata mafanikio yoyote.
Pili, viongozi wa pande mbili wote wanakabiliwa na shinikizo. Hivi sasa Ehud Olmert anakabiliwa na shinikizo kutoka pande mbili, moja inatoka kutoka kundi la Yisrael Beiteinu likisema kuwa kama Israel na Palestina zikifanya mazungumzo kuhusu masuala ya msingi, basi kundi hilo litajitoa kutoka kwenye serikali ya mseto, shinikizo jingine ni kuwa chama cha Hezbollah cha Lebanon kinachofanya uchunguzi kuhusu mgogoro uliotokea mwaka 2006 kati ya Israel na Lebanon, na tarehe 30 mwezi huu kitatoa ripoti ya mwisho. Mambo hayo yote yanahatarisha uimara wa serikali ya Bw. Ehud Olmert. Bw. Abbas bado ni dhaifu katika udhibiti wa ukanda wa Gaza, mkutano wa vyama vya upinzani utakaofanyika hivi karibuni ni uthibitisho wa hali hiyo. Hivi karibuni Syria imekubali kundi la Hamas, kundi la Jihad na kundi la PFLP kufanya mkutano huko Damaskas, mji mkuu wa Syria kujadili hali ya kisiasa nchini Palestina. Baadhi ya maofisa waandamizi walio karibu na Bw. Abbas wana wasiwasi kwamba, heunda kwenye mkutano huo kundi la Hamas na makundi mengine ya upinzani yataunda jumuyia iliyo kama chama cha ukombozi wa Palestina, na chini ya jumuyia hiyo kuunda kundi la viongozi badala ya serikali ya mpito.
Hali kama hiyo iliyoelezwa hapo juu imeamua mazungumzo hayo yaliyofanyika kutokana na shinikizo la Marekani hayawezi kupata mafanikio katika muda mfupi.
Idhaa ya kiswahili 2008-01-15
|