Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-01-16 18:33:00    
Hospitali za Taiwan zaingia kwa hamasa kwenye soko la matibabu la China bara

 


cri

Baada ya kufanya maandalizi kwa miaka miwili, kituo cha kwanza cha huduma za matibabu kilichoanzishwa na hospitali maarufu ya Changgeng ya Taiwan hapa China bara kitafunguliwa hivi karibuni mjini Xiamen mkoani Fujian. Tangu mwaka 2000 serikali ya China ilipoanza kutekeleza sera ya kuruhusu wawekezaji kutoka Taiwan kuanzisha hospitali kwa ubia hapa China bara, makampuni na idara za matibabu za Taiwan ziliingia kwa hamasa kwenye soko la matibabu la China bara.

Hospitali ya Changgeng ya Xiamen iliyowekezwa na kampuni ya viwanda vya plastiki ya Taiwan iko kwenye eneo la uwekezaji kutoka Taiwan la Haicang. Hospitali hiyo lenye eneo la hekta 70 ina sehemu tatu yaani eneo la hospitali, eneo la chuo kikuu cha udaktari na eneo la kurudisha afya. Baada ya kumalizika kujengwa kwa hospitali hiyo iliyowekezwa Yuan bilioni 1.2 itakuwa na vitanda 4500. Mkurugenzi mtendaji wa hospitali hiyo Bw. Zheng Minghui alisema, mji wa Xiamen unatazamana na Taiwan kwa kutengwa na bahari, wafanyabiashara wengi wa Taiwan wamewekeza katika mji huo, hiyo pia ni sababu muhimu kwa hospitali ya Changgeng kujengwa mjini humo. Bw. Zheng Minghui alisema:

"wafanyabiashara wa Taiwan wakienda kwenye hospitali hiyo wanajisikia kama wako nyumbani, kwa kuwa hospitali hiyo mjini Xiamen na katika sehemu nyingine huko Taiwan zote zinafanana, utaratibu wa huduma, sifa ya madaktari na wauguzi pia ni sawasawa na ile ya Taiwan. Tofauti ni kwamba kama wafanyabiashara wa Taiwan wakienda kwenye hospitali hiyo wanaweza kuhamishiwa rekodi zake za matibabu kutoka Taiwan kwa kutumia mfumo wa kielektroniki, hivyo watajisikia kama wako nyumbani."

Hospitali ya Wangwang ya mji wa Changsha ambayo ni hospitali ya kwanza iliyowekezwa na makampuni ya Taiwan nchini China imetoa huduma kwa muda wa zaidi ya miaka miwili. Kuanzia mwaka 2005 hadi leo, mfumo wa uendeshaji wa hospitali hiyo umekuwa unapevuka hatua kwa hatua. Mkurugenzi wa hospitali hiyo Bw. Li Yongguo alisema, walichagua kujenga hospitali hiyo kwenye mkoa wa ndani wa Hunan katika China bara baada ya kufanya uchambuzi kwa makini. Bw. Li Yongguo alisema:

"mkoa wa Hunan una watu zaidi ya milioni 67, ambayo ni mara tatu kuliko ile ya kisiwa cha Taiwan. Lakini mkoa huo una hospitali kubwa chache. Aidha, mikoa majirani yake kama vile, Guangxi, Jiangxi na Guizhou yote iko nyuma katika shughuli za matibabu. Lakini kwa kawaida watu wanapenda kupata matibabu kwenye hospitali za karibu, hivyo tulifanya uamuzi wa kujenga hospitali hiyo huko"

Mtafiti wa Taasisi ya suala la Taiwan katika chuo kikuu cha Qinghua Dk. Huang Dehai anaona kuwa, kuna sababu mbili kwa hospitali za Taiwan kuingia kwa hamasa kwenye soko la matibabu la China bara, ya kwanza ni kuwa kuna wafanyabiashara wengi wanaokuja kuwekeza China bara, pia kuna watalii wengi zaidi kutoka Taiwan wanaotembelea China. Hii ni sababu ya moja kwa moja kwa idara za matibabu ya Taiwan kuingia China bara. Sababu nyingine kubwa ni hali ya idara za matibabu huko Taiwan kuwa nyingi na mustakabali mkubwa wa soko la matibabu la China bara. Dk. Huang Dehai alisema:

"Taiwan ina watu milioni 23, lakini shughuli zake za matibabu ni kubwa zaidi na za kiwango cha juu. Katika miaka miwili au mitatu ijayo, kiwango cha jumla cha matibabu cha Taiwan kitaendelea kuinuka. Taiwan ina idara elfu 20 za matibabu, kwa wastani idara moja inahudumia watu elfu moja tu, idara hizo kwa jumla zina vitanda laki 1.5, kwa wastani kila watu elfu moja wana vitanda 6.5, na watu 9 katika watu elfu moja huko Taiwan wanafanya kazi zinazohusu huduma za afya."

Hospitali za Taiwan zikiingia kwenye soko la matibabu la China bara, lazima zijiunge kwenye mfumo wa matibabu wa China bara na kutoa chaguo kwa wagonjwa, hospitali hizo zina umaalumu gani ambao unaweza kuzisaidia kujitokeza? Dk. Huang Dehai anaona kuwa, katika kazi za upangaji wa idara za magonjwa na utaratibu wa uendeshaji, hospitali za Taiwan ni tofauti na zile za kiserikali za China, zinatilia maanani zaidi mahitaji ya wagonjwa, uzoefu mkubwa wa usimamizi wa hospitali hizo pia ni mambo yanayokosekana katika hospitali nyingi za kiserikali za China bara.

Mkurugenzi mtendaji wa hospitali ya Changgeng Bw. Zheng Minghui alisema, hospitali hiyo imefuata utaratibu na uzoefu wa miaka mingi wa hospitali ya Changgeng ya Taiwan kuhusu usimamizi na uendeshaji. Aidha vifaa na miundombinu ya hospitali hiyo pia vimefikia kiwango cha juu cha kimataifa. Baada ya kufunguliwa rasmi, hospitali hiyo itaingiza hatua kwa hatua teknolojia zenye ufanisi za Taiwan kuhusu uhamishaji wa viungo mwilini, urekebishaji wa sura na upasuaji wa moyo, pia hospitali hiyo inataka kuanzisha ushirikiano wa kitaaluma na idara za matibabu za China bara. Bw. Zheng Minghui alisema:

"tunataka kushirikiana na hospitali za China bara, tuna madaktari 1700, wengi kati yao ni wataalamu hodari, tunaweza kuwaalika kuja kutoa maelekezo na ushauri, aidha tutaandaa makongamano mara kwa mara, ili kutoa nafasi kwa mawasiliano kati ya wataalamu wa pande mbili za mlangobahari wa Taiwan. Kwa hivyo tutadumisha utaratibu huo wa makongamano."

Mbali na hospitali ya Wangwang na ya Changgeng, hospitali mbili za Taiwan mijini Nanjing na Suzhou pia zitafunguliwa hivi karibuni.Hospitali nyingi za Taiwan zinafanya maandalizi ya kujenga hospitali China bara. Mtafiti wa taasisi ya suala la Taiwan katika chuo kikuu cha Qinghua Dk. Huang Dehai alisema, hali hiyo imeonesha kuwa, baada ya viwanda vya utengenezaji, mawasiliano kati ya hospitali kati ya China bara na Taiwan yanaendelea kuimarika.