Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-01-16 18:48:32    
Vipindi vya uhifadhi wa mazingira shuleni kwenye uwanda wa juu wa Qinghai-Tibet

cri
Sehemu ya kusini magharibi ya mkoa wa Qinghai, inajulikana kama Chanzo cha Mito Mitatu kutokana na kuwa na vyanzo vya mito mitatu mikubwa ya China ya Changjiang, Huanghe na Lancangjiang. Sehemu hiyo iliyoko katikati ya Uwanda wa Juu wa Qinghai-Tibet ina mito na maziwa mengi, ni chanzo muhimu cha maji nchini China. Ili kuhifadhi mazingira ya kimaumbile kwenye mkoa huo, katika miaka ya hivi karibuni serikali ilichukua hatua mbalimbali, ikiwemo kuanzisha vipindi vya uhifadhi wa mazingira shuleni.

"Dunia, maskani yetu pekee, tanaipenda daima dawama, dunia, mama yetu, tunastarehe vilivyo chini ya mwanga wa jua kwenye dunia."

Wapendwa wasikilizaji, mliosikia ni sauti ya kusoma shairi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Bendera Nyekundu kwenye tarafa ya Jiegu ya wilaya inayojidenesha ya kabila la Watibet ya Yushu mkoani Qinghai. Shairi hilo lenye jina la Dunia ni Mama Yetu linahusu mwito wa kuhifadhi mazingira.

Wilaya ya Yushu iko kwenye sehemu ya Chanzo cha Mito Mitatu. Mwezi Agosti mwaka 2005, serikali ya China ilianza kutekeleza mpango wa jumla wa kuhifadhi na kujenga mazingira ya asili kwenye hifadhi ya Chanzo cha Mito Mitatu, na wilaya ya Yushu ni sehemu muhimu kwenye hifadhi hiyo.

Katika miaka ya hivi karibuni, kutokana na kupungua kwa maji ya sehemu ya Chanzo cha Mito Mitatu na kuongezeka kwa joto, asilimia 50 ya mbuga kwenye sehemu hiyo ilidhoofika, hali hii ilisababisha upungufu wa maji kwenye Mto Huanghe kwa miaka saba mfululizo. Idara zinazohusika za serikali ya China inafuatlia sana suala hilo. Kwa kufuata mwito wa serikali, wakazi wa sehemu hiyo wanatilia maanani sana shughuli za kuhifadhi mazingira.

"Kwanza, tunapaswa kujua tunaishi kwenye sehemu maalumu, kwa nini tunasema hivyo?"

Hii ni sauti ya mwalimu wa Shule ya Msingi ya Bendera Nyekundu anayefundisha watoto elimu ya uhifadhi wa mazingira. Kwenye shule hiyo somo la uhifadhi wa mazingira lipo kila wiki. Suonan Baji kutoka kabila la Watibet ni mwanafunzi wa mwaka wa tano, alipewa jina la mlinzi mdogo wa mazingira wa kimaumbile, aliona fahari kubwa kwa kupewa jina hilo, na alisema,

"Mazingira ya kimaumbile ni muhimu sana kwa binadamu, kwa kuwa mazingira ikiharibiwa, tutakosa mahali pa kuishi. Naona fahari kuwa ninaweza kutoa mchango kwa ajili ya kuhifadhi mazingira. Tunaishi kwenye sehemu ya chanzo cha mito ya Changjiang, Huanghe na Lancangjiang, chanzo hicho kikichafuliwa hakika sehemu ya chini ya mtiririko wa mito itachafuliwa."

Somo la uhifadhi mazingira kwenye shule linawafundisha wanafunzi watoto elimu wa uhifadhi wa mazingira, na kuwafahamisha umuhimu wa kuhifadhi mazingira, aidha somo hilo viliwafanya wawe waenezaji wa uhifadhi wa mazingira. Mwanafunzi wengine wa Shule ya Msingi wa Bendera Nyekundu Chen Yingjing alisema,

"Niliwaambia wazazi wangu wasitupe ovyo mifuko ya plastiki, kwa kuwa mifuko hiyo inachafua mazingira ya kimaumbile."

Bibi Zhuoma Qingshui ni ofisa wa Shirikisho la Uhifadhi wa Mazingira la Sehemu ya Chanzo cha Mito Mitatu kwenye wilaya inayojiendesha ya kabila la Watibet ya Yushu, anashughulikia mradi wa elimu ya uhifadhi wa mazingira kwenye shule ya msingi. Bibi Zhuoma Qingshui alisema, kazi kuu ya mradi huo ni kufanya majaribio ya kuanzisha elimu ya uhifadhi wa mazingira kwenye shule tano za tarafa ya Jiegu ya wilaya ya Yushu, na baadaye somo la elimu hiyo litawekwa kwenye shule zote za sehemu ya Chanzo cha Mito Mitatu.

Bibi Zhuoma Qingshui anatoka mkoa wa utawala maalumu wa Hongkong, amefanya kazi ya kujitolea kwenye Shirikisho la Uhifadhi wa Mazingira la Sehemu ya Chanzo cha Mito Mitatu la wilaya ya Yushu kwa miezi tisa. Kabla ya hapo, alifanya kazi ya kufundisha elimu ya maumbile kwa miaka zaidi ya 10 huko Hongkong. Bibi Zhuoma Qingshui alisema,

"Mazingira ya asili kwenye sehemu ya Chanzo cha Mito Mitatu ni muhimu na mazuri, pia ni rahisi kuharibika. Lakini watu wengine wanaona tu mazingra mazuri, hawajui kasi ya uchafuzi wa mazingira kwenye shemu hiyo."

Wakati wa kufanya kazi ya kueneza elimu ya uhifadhi wa mazingira kwenye sehemu hiyo, bibi Zhuma Qingshui aliona nia na juhudi kubwa za Watibet wa huko kwa uhifadhi wa mazingira, lakini pia aliona kuwa hawana elimu ya kutosha kuhusu uhifadhi wa mazingira. Alisema,

"Maisha ya jadi ya kabila la Watibet hayaleta athari kubwa kwa mazingira ya kimaumbile, lakini sasa mtindo mpya wa maisha kutoka sehemu za nje umeingia, watu hao wanapanda pikipiki badala ya farasi, na kununua chakula kinachofungwa na mifuko ya plastiki. Hawajui vitu hivyo vinaweza kuchafua mazingira."

Ili kueneza elimu ya uhifadhi wa mazingira kwa watu wa kabila la Watibet, bibi Zhuoma Qingshui alikwenda maeneo ya ufugaji kuwaandalia semina, na kuwafundisha njia rahisi ya kuhifadhi mazingira. Alisema hatua bora zaidi ni kuwaenezea watoto elimu ya uhifadhi wa mazingira, na kufanya elimu hiyo iwe na mzizi mioyoni mwa watoto hao.

Wakati waandishi wa habari walipomaliza mahojiano, kipindi cha elimu ya uhifadhi wa mazingira kilikuwa kinaendelea kwenye Shule ya Msingi ya Bendera Nyekundu. Mwalimu alisema,

"Kila mtu ni mbegu mdogo, tunapaswa kukumbuka elimu ya uhifadhi wa mazingira kwenye ubongo wetu, halafu kuieneza kama mbegu unaota. Hivyo watu wanaotilia maanani elimu hiyo wataongezeka siku hadi siku, na mazingira ya kimaumbile duniani yataboreshwa siku hadi siku."

Idhaa ya kiswahili 2008-01-16