Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-01-16 19:56:19    
Mapishi ya kuku aliyekaangwa

cri

Mahitaji

kuku mmoja, chumvi gramu 3, sukari gramu 15, mchuzi wa sosi gramu 10, mvinyo wa kupikia gramu 15, pilipili manga gramu 2, vitunguu maji gramu 15, tangawizi gramu 15, chembechembe za kukoleza ladha gramu 1, mafuta ya ufuta gramu 10.

Njia

1.Kataa kichwa, miguu ya kuku, halafu weka kwenye maji moto, chemsha kwa dakika 5 halafu apakue.

2.Changanya chumvi, sukari, mchuzi wa sosi, mvinyo wa kupikia, pilipili manga halafu paka kwenye kuku, halafu weka tangawizi na vitunguu maji kwenye tumbo la kuku, halafu weka kwenye sahani, chemsha maji, endelea kuchemsha maji kwa mvuke. Halafu pakua, na kupaka sukari na ondoa vitunguu maji, tangawizi na pilipili manga.

3.Washa moto mimina mafuta kwenye sufuria, weka kuku kwenye sufuria kasha mkaange, mpaka ngozi yake iwe rangi ya hudhurungi, ipakue. Uikate iwe vipande.

4.Koroga chembechembe za kukoleza ladha, sukari na mafuta ya ufuta pamoja na sosi ya kuchemshia kuku, halafu mimina kwenye kuku. Mpaka hapo kitoweo hiki kiko tayari kuliwa.