Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-01-17 11:14:54    
Kituo cha kuwalazimisha watumiaji wanawake wa mihadarati kuacha kutumia mihadarati na kufufua afya cha China chaanzishwa mjini Lanzhou

cri

Kituo cha kwanza cha kuwalazimisha watumiaji wanawake wa mihadarati kuacha kutumia mihadarati na kufufua afya kilianzishwa hivi karibuni mjini Lanzhou, mkoani Gansu, China. Katika kituo hicho, watumiaji wa mihadarati wanaweza kuacha kutumia mihadarati kwa hiari na kupata mafunzo ya ufundi wa kazi. Hivi sasa wanawake 30 wanaotumia mihadarati wameanza mpango wa kuacha kutumia mihadarati katika kituo hicho na kupata mafunzo ya ufundi wa kazi.

Kituo hicho kiko kwenye wilaya ya Yuzhong mjini Lanzhou. Wanawake waliotumia dawa ya kulevya na kulazimishwa kuacha kutumia dawa hizo, wanaweza kwenda kwenye kituo hicho kwa hiari na kufufua afya na kupata mafunzo ya ufundi wa kazi.

Kituo hicho huwawekea hali ya kimsingi ya chakula na malazi, kuwatibu magonjwa ya kawaida bila malipo, na kuwaandaa wanawake hao kushiriki kwenye uzalishaji, na kuwapa malipo kila mwezi watu hao kutokana na ufanisi wa uzalishaji na hali walivyofanya kazi.

Habari nyingine zinasema, mfuko wa kwanza unaofuatilia afya ya saikolojia ya watoto nchini China ulianzishwa rasmi tarehe 8 hapa Beijing. Naibu spika wa kamati ya kudumu ya bunge la umma la China Bi. Gu Xiulian, mwenyekiti wa heshima wa kamati ya michezo ya Olimpiki ya China Bw. He Zhenliang na watu wengine maarufu walizindua mfuko huo.

Habari zinasema, mfuko huo ulianzishwa na mfuko wa watoto wa China na tovuti ya afya 863 ya China kwenye mtandao wa Internet. Na mfuko huo utashughulikia kazi za vibarua kutoa ujuzi wa afya ya saikolojia kwa watoto wanaobaki vijijini ambao wazazi wao wanafanya kazi mijini, watoto wa familia zenye matatizo ya kiuchumi na watoto wa familia zenye mzazi mmoja. Kwenye uzinduzi wa mfuko huo, Bibi Gu Xiulian kwa niaba ya mfuko wa watoto wa China alipokea michango ya yuan milioni 5 iliyotolewa na tovuti ya afya 863.

Naibu mkurugenzi wa baraza la mfuko wa watoto wa China Bibi Feng Cui alisema, hivi karibuni idadi ya watoto waliobaki vijijini ambao wazazi wao wanafanya kazi za vibarua mijini imefikia milioni 20, na inaendelea kuongezeka. Kutokana na kuwa watoto hao hawaishi pamoja na wazazi wao, watoto hao wana matatizo makubwa ya kisaikolojia, na uslama. Inapaswa kuwaandaa walimu wa vijijini mara moja kuhusu elimu ya saikolojia inayohusiana na watoto wanaobaki vijijini.

Na habari kuhusu Jumba la makumbusho la akina mama na watoto la China zinasema, tarehe 9 mwezi Janurari jumba hilo lilipokea fedha za renminbi milioni 21.55 zilizochangishwa na makampuni na watu binafsi. Hadi sasa, jumba hilo la makumbusho litakalofunguliwa limepata fedha zilizochangwa zaidi ya yuan milioni 45.

Naibu mwenyekiti wa shirikisho la akina mama la China, ambaye pia ni katibu wa ofisi ya sekretarieti Bibi Mo Wenxiu alisema, ujenzi wa jumba la makumbusho la akina mama na watoto la China ni jambo muhimu la maendeleo ya shughuli za akina mama na watoto wa China, ambayo siyo tu ni zawadi kubwa kwa michezo ya Olimpiki ya Beijing ya mwaka 2008, bali pia ni hatua kubwa katika maendeleo ya shughuli za utamaduni za China.

Shirikisho hilo pia lilisifu idara na watu binafsi waliotoa michango.

Habari zinasema, jumba la makumbusho ya wanawake na watoto la China ambalo ni jumba la kwanza la makumbusho kuhusu wanawake na watoto nchini China litafunguliwa mwishoni mwa mwezi Julai mwaka 2008.

Kabla ya hapo, shirikisho kuu la wanawake wa China lilianzisha mfuko maalumu wa Jumba la makumbusho ya wanawake na watoto la China katika mfuko wa watoto na vijana wa China, na kupokea michango iliyotolewa na watu wa hali mbalimbali kutoka kwenye jamii.

Idhaa ya kiswahili 2008-01-17