Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-01-17 17:15:40    
Ziara ya Rais Gorge Bush kwenye nchi za Mashariki ya Kati imepata mafanikio gani?

cri

Tarehe 16 Rais George Bush alimaliza ziara yake kwenye nchi za Mashariki ya Kati. Kwenye ziara hiyo Rais Bush alizitembelea Israel, Palestina, Kuwait, Bahrain, Falme za Kiarabu, Saudi Arabia na Misri. Mapema kabla ya ziara yake, Rais Gorge Bush alisema wazi kwamba ziara yake ina malengo mawili, moja ni kusukuma mazungumzo ya amani kati ya Palestina na Israel, nyingine ni kuziunganisha nchi za Kiarabu ili kudhibiti Iran. Lakini je ziara yake imefikia malengo hayo?

"Viongozi wa Israel na Palestina wote wamekubali kufanya juhudi za kufikia makubaliano ya kuwepo kwa nchi zote mbili kwa wakati mmoja. Nchi jirani, na hasa Misri pia imekubali kuchangia juhudi hizo. Mimi nafurahia sana uungaji mkoko kutoka Misri na nchi nyingine katika mchakato huo wa amani."

Hii ni kauli ya Rais Gorge Bush alipokuwa akizungumza na Rais Bubarak wa Misri alipokuwa katika kituo cha mwisho cha ziara yake. Suala la amani kati ya Palestina na Israel ilikuwa ni ajenda muhimu katika ziara ya George Bush kwenye nchi za Mashariki ya Kati. Tarehe 9 na 10 kwa nyakati tofauti alizungumza na viongozi wa Israel na Palestina na alitoa mapendekezo yake kuhusu mazungumzo ya amani kati ya Palestina na Israel. Lakini mwandishi wetu Yuan Qi aliyekuwa Jerusalem anaona kuwa ingawa ziara ya Rais Georg Bush haikuwa ya bure, lakini haikutatua masuala ya msingi kati ya Palestina na Israel.

"Kwanza, suala la hatma ya Jerusalem halikutatuliwa. Rais George Bush hakujibu wazi ombi la Palestina kuhusu kuweka mji mkuu Jerusalem kwa mujibu wa azimio la Umoja wa Mataifa, na kwa upande mwingine Bw. Olmert pia alikataa matakwa ya Marekani kuhusu kusimamisha kujenga makazi ya Wayahudi. Pili, msimamo wa Rais George Bush kuhusu masuala mengi unaonekana kama ni wa haki, lakini kutokana na uchambuzi wa maneno aliyosema ziarani watu wamegundua kwamba anaipendelea Israel. Kwa hiyo mazungumzo yatakayofanyika kati ya Palestina na Israel yatakabiliwa na chamgamoto."

Hata hivyo, mkuu wa Chuo cha Utafiti wa Mambo ya Kimataifa cha China ambaye pia ni mtaalamu wa masuala ya Mashariki ya Kati Bw. Li Shaoxian anaona kuwa hivi sasa mazungumzo kuhusu masuala ya msingi kati ya pande mbili yameanza, hii inamaanisha kuwa ziara ya Rais George Bush haikuwa bure katika kusukuma mazungumzo hayo. Alisema,

"Mchakato wa amani kati ya Palestina na Israel unahitaji masharti mawili, moja ni mahitaji ya ndani ya nchi hizo mbili ambayo yanataka kutatua suala la amani kwa kufanya mazungumzo, pili ni nguvu ya kuyasukuma kutoka Marekani. Baada ya mwaka 2000 mazungumzo kati ya pande mbili yalianza kukwama, sababu muhimu ni kuwa Marekani haikulipa suala hilo kipaumbele, kwa hiyo ama mkutano wa amani ya Mashariki ya Kati uliofanyika Novemba mwaka jana au ziara hiyo ya George Bush, yote yana maana kwa mchakato wa amani kati ya Palestina na Israel."

Lengo jingine la ziara ya George Bush ni kudhibiti athari ya Iran kwenye Mashariki ya Kati. Tarehe 9 Bw. George Bush alipokuwa Jerusalem alisema, ingawa ripoti iliyotolewa na idara ya upelelezi ya Marekani imesema Iran ilisimamisha shughuli za utafiti wa silaha za nyuklia mapema mwaka 2003, lakini George Bush anaona kuwa kama jumuyia ya kimataifa haitachukua hatua, Iran itakuwa tishio kwa dunia nzima.

Mtaalamu wa Chuo cha Utafiti wa Uhusiano wa Kimataifa nchini China Bw. Gao Zugui alisema, ziarani George Bush amefikia kwa kiasi fulani lengo lake la kuunganisha nchi za Ghuba na kuitenga Iran, na huku inaonesha kuwa Marekani kwa msimamo wa kidete itachukua sera ya kuidhibiti Iran kwa muda mrefu.