Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-01-17 17:47:13    
Maisha mazuri ya wakulima wanaofanya kazi za vibarua mjini Shanghai

cri

Hivi sasa nchini China kuna wakulima milioni 120 wanaofanya kazi za vibarua mijini, ambao wanashughulikia kazi za ujenzi, uhifadhi wa mazingira na afya, utengenezaji, na utoaji wa huduma za nyumbani. Katika mji wa Shanghai tu, kuna wakulima zaidi ya milioni 4 wanaofanya kazi za vibarua, ambao wanatoa mchango mkubwa kwa maendeleo ya Shanghai. Serikali ya mji wa Shanghai inafanya juhudi ili kuboresha mazingira yao ya kazi na maisha, ambayo ni pamoja na uhakikisho wa matibabu na elimu, ili waweze kunufaika na maendeleo ya Shanghai.

Jumba la ghorofa la Yongsheng lililojengwa miaka mitatu iliyopita ni moja ya majumba makubwa kabisa ya makazi mjini Shanghai kwa watu wanaotoka sehemu nyingine na kufanya kazi mjini humo. Jumba hilo linaongozwa na serikali, na kugharamiwa Yuan za RMB zaidi ya milioni 300. Mkulima Huang Falei aliyetoka mkoani Shandong na kufanya kazi za vibarua mjini Shanghai anaishi katika jumba hilo, na kila mwezi anatoa Yuan za RMB 80 tu. Bw. Huang Falei alisema,

"Kuishi kwenye jumba hili ni starehe kuliko kuishi nje. Ulinzi wa usalama ni mzuri hapa. Naona kuwa kuishi nje ya makazi kama hayo tunakuta taabu zaidi hata tutatugharimu pesa nyingi."

Jumba la ghorofa la Yongsheng lina majengo 10 yenye ghorofa 6. Bustani ndani ya jumba hilo inawapendeza watu, na miundo mbinu ya maisha kama vile mikahawa, supamaketi, kliniki na benki za kujihudumia zote zimejengwa kwenye makazi hayo. Aidha kuna maktaba, ukumbi wenye sehemu za kufanya shughuli mbalimbali, sehemu ya huduma ya mtandao wa internet na vifaa vya mazoezi za kujenga mwili, ili kukidhi mahitaji ya wafanyakazi vijana kufanya mazoezi ya kujenga mwili, kujifunza na kustarehe. Kituo cha utoaji huduma na usimamizi wa mtaa pia kinaalika walimu wa vyuo vikuu na washauri wa sheria, ili kutoa huduma kwa wakulima wanaofanya kazi za vibarua mijini.

Licha ya Jumba la ghorofa, mji wa Shanghai pia unajenga nyumba za kodi ndogo kwa wakulima wanaofanya kazi za vibarua mijini, na kujaribu kukarabati viwanda vya mjini visivyotumika kuwa mabweni, ili kuboresha mazingira ya maisha ya wakulima wanaofanya kazi za vibarua mjini.

Mbali na kuhakikisha mazingira ya maisha ya kimsingi ya wakulima wanaofanya kazi za vibarua mijini, mji wa Shanghai pia unafanya juhudi kutoa huduma za uhakikisho wa jamii zinazokamilika zaidi kwa ajili ya wakulima hao. Mkurugenzi wa ofisi ya mkutano wa kazi ya wakulima wanaofanya kazi za vibarua mjini Shanghai Bw. Zhao Jiande alisema, mji wa Shanghai unajenga "uhakikisho" wa maisha kwa wakulima milioni 4 wanaofanya kazi za vibarua mjini humo. Kwa mujibu wa takwimu mpya zilizotolewa na idara ya kazi na huduma za jamii ya Shanghai, eneo la bima za aina mbalimbali kwa wakulima wanaofanya kazi za vibarua mjini Shanghai linapanuka siku hadi siku, hadi kufikia mwishoni mwa mwezi Septemba mwaka 2007, idadi ya watu wanaoshiriki kwenye bima ilifikia milioni 3.19, ambayo ilichukua asilimia 80 ya idadi yote ya watu mjini humo. Mji wa Shanghai unapanga kuifanya idadi hiyo ifikie asilimia 90 ifikapo mwaka 2010.

Suala la utoaji elimu kwa watoto wa wakulima wanaofanya kazi za vibarua mijini, ambalo linafuatiliwa kabisa na wakulima hao, sasa limetatuliwa. Mjini Shanghai watoto wa wakulima hao wanatendewa sawa na wanafunzi wa huko. Shule zote za serikali mjini Shanghai zinafunguliwa kwa watoto wa wakulima wanaofanya kazi za vibarua mijini. Aidha, watoto hao wanaweza kusoma katika shule zilizo karibu na mahali wazazi wao wanapofanya kazi. Shule hizo zinaandikisha watoto wa wakulima hao, ambazo nyingi zilianzishwa kwa kutegemea nguvu za jamii, nyingine pia zilipewa msaada na serikali.

Shule ya msingi ya Huaxing wilayani Minhang ni shule iliyoanzishwa kwa ajili ya watoto wa wakulima wanaofanya kazi za vibarua mjini Shanghai. Watoto zaidi ya 1,000 kutoka sehemu mbalimbali nchini China wanasoma kwenye shule hiyo. Dong Jie na Liao Ying wanatoka mikoa ya Sichuang na Jiangxi, na walianza kusoma kwenye shule hiyo miaka mitatu iliyopita.

"Darasa la hapa ni nadhifu na kubwa zaidi, nafurahi kusoma hapa. Napenda kabisa somo la sayansi na teknolojia, kwa sababu tunaweza kushiriki katika shughuli nyingi."

"Mimi napenda kipindi cha kusoma kila wiki, kwa sababu napenda kusoma vitabu, naona ninaweza kupata ujuzi mwingi kutoka kwenye vitabu."

Katika wilaya ya Minhang, kuna shule 33 zinazoandikisha watoto wa wakulima wanaofanya kazi za vibarua mjini Shanghai, ambazo zina wanafunzi zaidi ya elfu 20. Ofisa wa idara ya elimu ya wilaya hiyo Bw. Wang Yixin alisema, serikali inaunga mkono shule hizo. Alisema,

"Bima za wajibu wa upande wa shule kwa wanafunzi watoto wa wakulima wanaofanya kazi za vibarua mjini Shanghai karibu zinakatwa na kamati ya elimu ya Shanghai. Mwaka 2007 serikali ya mji wa Shanghai imetenga Yuan za RMB zaidi ya milioni 14 kwa ajili ya wilaya ya Minhang, ili kufanya marekebisho ya vifaa vya shuleni, na kununua vitabu na vifaa vya matibabu."

Mwaka 2006 kamati ya elimu ya mji wa Shanghai ilitenga Yuan za RMB milioni 30, na kufanya marekebisho kwa miundo mbinu ya shule za msingi 277 zinazoandikisha watoto wa vijijini mjini humo.

Wakulima wanaofanya kazi za vibarua mjini wamekuwa sehemu ya mji huo mkubwa wa Shanghai. Vituo vyote vya utoaji wa huduma za utamaduni vya mitaa mjini humo vinafunguliwa kwao. Mkurugenzi wa ofisi ya mkutano wa kazi ya wakulima wanaofanya kazi za vibarua mjini Shanghai Bw. Zhao Jiande alisema, serikali itachukua hatua nyingine zaidi ili kuinua zaidi sifa za maisha ya wakulima hao, ili waweze kujiunga na mji wa Shanghai.

Idhaa ya kiswahili 2008-01-17