Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-01-21 20:10:26    
Kwa nini waziri mkuu wa Japan Yasuo Fukuda atilia mkazo sera ya "mazingira " ?

cri

Tarehe 21 hali ya "vuta nikuvute" itatokea katika bunge la Japan. Wakati huo waziri mkuu wa Japan Bw. Yasuo Fukuda alikuwa anaulizwa maswali na wabunge kuhusu sera zake alizotoa tarehe 18. Kwenye hotuba aliyotoa tarehe 18 alitangaza na kutilia mkazo sera tano za kitaifa, nazo ni kubadilisha mfumo wa fedha ili kuhakikisha huduma za jamii na usalama, kujenga jamii iwe na uchangamfu wa kiuchumi, kuijenga Japan iwe nchi inayochangia amani na kuifanya Japan iwe jamii inayotoa "kiasi kidogo cha hewa ya Crabon dioxide". Kati ya sera hizo tano alitilia mkazo sera ya mapambano dhidi ya utoaji wa hewa ya Carbon dioxide na kwa mara ya kwanza alitoa sera ya kujenga "jamii inayotoa kiasi kidogo cha hewa ya carbon dioxide".

Wachambuzi wanaona kuwa kutanguliza mbele sera ya "mazingira safi" inatokana na nia yake ya kukipinga Chama cha upinzani cha Demokrasia. Imefahamika kwamba Bw. Yasuo Fukuda alishika madaraka wakati ambapo chama tawala kilikuwa kimepoteza karibu nusu ya viti bungeni na waziri mkuu Bw Shinzo Abe alipaswa kujiuzulu ghafla. Tokea mwezi Septemba mwaka jana alipoanza kushika madaraka ya waziri mkuu, siku zote amekuwa anasisitiza kuwa sera zake za utawala ni kwa ajili ya kuleta utulivu wa jamii na kuwatuliza wananchi kimaisha.

Lakini mwanzoni kutokana na kushika madaraka katika hali ya dharura, hakutoa sera halisi za kutimiza nia hiyo, na ilimpasa akabiliane na matatizo mengi yaliyoachwa na mawaziri wakuu wa zamani, yakiwemo matatizo ya kupotea kwa kumbukumbu za fedha za malipo ya uzeeni na watu karibu elfu moja waliopata ugonjwa wa maini kutokana kutumia dawa fulani na kuzifanya hatua mpya za mapambano dhidi ya ugaidi zipitishwe katika bunge. Bahati nzuri ni kuwa, miezi mitatu baadaye matatizo hayo yote yalitatuliwa, na hatua mpya za mapambano dhidi ya ugaidi ingawa zilikumbwa na pingamizi, lakini mwishowe zilipitishwa bungeni, kumbukumbu kuhusu fedha za malipo ya uzeeni zimeratibiwa, na sheria ya kuwasaidia wagonjwa wa maini kutokana na kutumia dawa fulani pia ilipitishwa bungeni, yote hayo yaliwafanya watu wa Japan wamwamini zaidi. Zaidi ya hayo, ziara yake aliyoifanya nchini China mwishoni mwa mwaka jana ilimpatia sifa, uhusiano kati ya China na Japan umekuwa mzuri ikilinganishwa na wa zamani, na uchumi wa Japani unaweza kufufuka kwa kusaidiwa na China. Utafiti wa maoni ya raia uliofanywa hivi karibuni umeonesha kuwa kiasi cha watu wanaomwunga mkono Bw Yasuo Fukuda hivi karibuni ghafla kimeacha kupungua.

Wachambuzi wanaona kuwa sera za Bw Yasuo Fukuda zinazotilia mkazo "mazingira safi" zinatokana na mtazamo wake wa mbali. Hivi sasa chama tawala kinakumbwa na shida kubwa kila kinapopiga hatua za utekelezaji, wakati Chama cha upinzani cha Demokrasia kinapodhibiti baraza la juu. Lakini hivi sasa theluthi mbili ya viti vya baraza la chini bado vinadhibitiwa na chama tawala. Kutokana na hali hiyo Bw. Yasuo Fukuda hakubali kuvunja baraza la chini na kufanya uchaguzi mkuu kabla ya wakati, kwa sababu wakati anapokuwa anaungwa mkono na watu wachache kwenye baraza la mawaziri itakuwa ni hatari kwa madaraka kunyakuliwa na Chama cha Demokrasia, na Japan ni nchi mwenyeji wa mkutano wa viongozi wa nchi nane kubwa utakaofanyika mwezi Julai mwaka huu, akiwa mwenyeji wa mkutano huo Bw. Yasuo Fukuda angeweza kujipatia sifa katika shughuli zake za diplomasia. Na sifa za shughuli za kidiplomasia zinasaidia kugeuza hali duni ya chama tawala, kwa hiyo itakuwa ni manufaa kwa Bw. Yasuo Fukuda kama uchaguzi mkuu ukifanyika baada ya mwezi Julai.

Lakini atawezaje kujipatia sifa kwenye mkutano wa viongozi wakuu wa nchi kubwa nane? Bw. Yasuo Fukuda anaona kuwa "mazingira safi" ni suala muhimu na linafuatiliwa duniani, shughuli zinazohusiana na suala hilo zinaweza kumwongezea sifa. Kwa upande mwingine, kuhusu utawala wa ndani, Bw. Yasuo Fukuda anaweza kutumia suala hilo kufuta pendekezo lililotolewa na Chama cha Demokrasia la "Kodi ya Muda ya Petroli". Kwa ujumla sera ya kulinda "mazingira safi" inaweza kumnufaisha Bw. Yasuo Fukuda katika mambo ya ndani na ya nje.