Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-01-23 11:21:16    
Kampuni za China zajenga njia kuu yenye mwendo kasi ya upashanaji habari kwa waafrika

cri

Kwenye makao makuu ya kampuni ya mawasiliano ya habari ya Zhongxing mjini Shenzhen, maofisa kadhaa waandamizi wa kampuni hiyo walimwonesha mwaandishi wetu wa habari kadi moja ya simu za mkononi mwandishi wa habari wetu, kadi hiyo ilinunuliwa mwishoni mwa karne iliyopita wakati kampuni ya Zhongxing ilipoanza shughuli zake barani Afrika.

Naibu mjumbe mkuu wa zamani wa kampuni ya Zhongxing nchini Libya Bw. Liu Kehui alisema, mwaka 1999 miundo mbinu ya mawasiliano ya habari ya nchi nyingi barani Afrika ilikuwa iko nyuma, soko la mtandao wa simu za mkononi lilikutoa chini ya ukiritimba wa wafanyabiashara wa utoaji wa zana za mawasiliano ya habari wa nchi za magharibi. Wakati huo kutoa maombi ya kukodi simu kulihitaji dola za kimarekani elfu 2 pamoja na fedha za huko elfu 2, na gharama za simu za mkononi zilikuwa za juu zaidi.

Kutokana na hali hiyo kampuni ya mawasiliano ya habari ya Zhongxing ambayo imeshika teknolojia muhimu ya simu za mkononi, iliwasili nchini Libya mwaka 1999, mwaka 2000 kampuni ya Zhongxing ilianzisha mtandao wa majaribio wa mawasiliano ya habari nchini Libya, na kuanzisha shughuli zake barani Afrika.

Nchi kadhaa barani Afrika zina ardhi kubwa lakini watu wachache, ambapo mtandao wa simu za nyumbani katika nchi hizo ulikuwa wa nyuma sana, familia nyingi hazikuwa na simu za nyumbani, na watu walikuwa wanatumia simu ghali za mkononi zinazotumia mtandao uliojengwa na nchi za magharibi. Kutokana na hali hiyo, kampuni za mawasiliano ya habari za Huawei na Zhongxing za China ziliamua kueneza matumizi ya simu za mkononi za CDMA, simu hizo zinatumika kwenye sehemu nyingi zaidi, na bei yake ni ya chini.

Sifa ya zana za mawasiliano ya habari na simu za mkononi zilizotengenezwa na China zimefikia hata kuzidi ile ya bidhaa kama hizo zilizotengenezwa na nchi za magharibi, aidha, bei ya bidhaa za China ni ya chini kuliko ile ya bidhaa za nchi za magharibi. Kwa upande wa huduma, kampuni za mawasiliano ya habari za China zinazingatia zaidi mahitaji ya watumiaji wa Afrika. Ili kujibu ombi la msaada la mteja, kampuni za mawasiliano ya habari za nchi za magharibi huenda zinahitaji mwezi mmoja, lakini kampuni ya Zhongxing inahitaji siku mbili au tatu tu.

Kwa upande mwingine kampuni za China zinawasaidia wenzi wa biashara wa Afrika kuwaandaa watu wenye ujuzi. Kila mwaka kampuni ya Zhongxing na kampuni ya Huawei zinawaandaa watu elfu kadhaa wenye ujuzi wa teknolojia na usimamizi kwa wenzi wao wa biashara barani Afrika, waafrika wengi waliopewa mafunzo wamekuwa maofisa waandamizi wa ofisi za kampuni ya Zhongxing barani Afrika.

Mwaka 2003 kampuni ya Zhongxing na wadau wa biashara wa huko zilisaini makubaliano yenye thamani ya dola za kimarekani milioni 43, hii ilionesha kuwa kampuni za mawasiliano ya habari za China zimeanza kupata maendeleo ya kasi barani Afrika. Hivi sasa kampuni za Huawei na Zhongxing zimechukua nafasi nyingi zaidi kwenye soko la CDMA barani Afrika. Kwenye soko la GSM linalochukua asilimia 70 ya soko la mawasiliano ya habari, nafasi za kampuni hizo mbili pia zinaongezeka siku hadi siku.

Hivi sasa nchini Libya, kadi ya simu za mkononi chini ya mtandao wa simu za mkononi uliojengwa na kampuni ya Zhongxing inauzwa kwa dola tatu za kimarekani, zamani kadi moja kama hiyo iliuzwa kwa dola za kimarekani elfu 4. Mtandao wa simu za mkononi uliojengwa na kampuni za China umesifiwa na wakazi wa huko kuwa ni "mtandao wa umma".

Naibu Mkuu wa zamani wa kampuni ya Zhongxing nchini Libya Bw. Liu Kehui alisema, hatasahau usiku mmoja wa mwezi Septemba mwaka 2004, ambapo kituo cha televisheni cha Libya kilitangaza kuwa mtandao wa simu za mkononi uliojengwa na kampuni ya Zhongxing utaanza kuuza kadi za simu za mkononi, wakazi wa huko walifurahi sana na kuwasha fataki ili kusherehekea habari hizo. Siku ya pili kituo cha televisheni kilitangaza moja kwa moja hali ya mauzo ya kadi za simu za mkononi, ambapo watu wengi walishindwa kununua kadi za simu za mkononi huko mji mkuu, hata walikwenda miji mingine kununua kadi hizo.

Bw. Liu Kehui alisema, teknolojia na bidhaa za mawasiliano ya habari za kampuni za China zinawanufaisha watu wa Afrika, na kubadilisha mtindo wa maisha yao, pia zimeimarisha mawasiliano kati ya Afrika na nchi nyingine. Ofisa wa kampuni ya Zhongxing Bw. Zhou Hongfeng alisema, tangu China ilipoanza kufanya mageuzi na kufungua mlango, mabadiliko makubwa yametokea nchini China, sifa nzuri ya bidhaa za China inawafanya waafrika waone uwezo wa wachina. Alisema kampuni ya Zhongxing inaweza kuungwa mkono na watu wa Afrika, kwa kuwa wananchi wa China na Afrika wanaungana mkono na kuaminiana.

Habari nyingine zinasema benki ya maendeleo ya China na serikali ya Kenya tarehe 6 zilisaini makubaliano ya mfumo kuhusu ushirikiano wa maendeleo na ukusanyaji wa mitaji. Ukiwa mradi muhimu wa kwanza kwenye makubaliano hayo, benki ya maendeleo ya China itatoa mkopo wa dola za kimarekani milioni 16.7 kwa Kenya, ili kuunga mkono ujenzi wa nyumba za familia za huko zenye mapato ya chini.

Kiongozi wa kikundi cha kazi ya Kenya cha Benki ya maendeleo ya China Bw. Zhu Qingdong alisema, benki hiyo ina uzoefu mkubwa katika ujenzi wa miundo mbinu, ujenzi wa nyumba kwa ajili ya familia zenye mapato ya chini, elimu, matibabu, na uhifadhi wa mazingira, na inapenda kufanya ushirikiano wa karibu zaidi na Kenya, ili kuhimiza maendeleo ya jamii na uchumi nchini Kenya, na kuboresha kiwango cha maisha ya wakazi wa huko.

Waziri wa fedha wa Kenya alisema, kusainiwa kwa makubaliano hayo kutaweka msingi mzuri kwa ushirikiano wa muda mrefu kati ya serikali ya Kenya na benki ya maendeleo ya China, na sekta za mawasiliano ya barabara, umeme na mawasiliano ya habari nchini Kenya zitanufaishwa kutokana na makubaliano hayo.

Balozi wa China nchini Kenya Bw. Zhang Ming alisema, kuimarisha ushirikiano kati ya China na Kenya katika sekta ya fedha ni hatua moja muhimu ya kutekeleza maamuzi yaliyotolewa kwenye mkutano wa wakuu wa Baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika uliofanyika hapa Beijing mwaka jana. Kuchukua mradi wa ujenzi wa nyumba kwa ajili ya familia zenye mapato ya chini kumeonesha kuwa benki ya maendeleo ya China inatilia maanani majukumu ya jamii. Alisema mradi huo utaboresha hali ya makazi nchini Kenya, pia utaongeza urafiki kati ya wananchi wa China na Kenya.