Waziri wa mambo ya nje wa Russia Bw. Sergey Lavrov tarehe 23 mwezi Januari huko Moscow kwenye mkutano na waandishi wa habari aliwaeleza mafanikio iliyoyapata Russia katika shughuli za kidiplomasia mwaka 2007, na sera ya kidiplomasia ya nchi hiyo.
Mkutano huo na waandishi wa habari ulifanyika adhuhuri ya siku hiyo kwenye ukumbi wa mkutano wa kituo cha habari cha wizara ya mambo ya nje ya Russia. Waandishi wa habari wa vyombo vya habari vya nchi hiyo pamoja na wa vyombo vya nchi za nje walioko mjini Moscow walihudhuria. Mwaka 2007, kwenye masuala ya nyukilia ya Iran, hadhi ya Kosovo, upangaji wa mfumo wa kuzuia makombora kwenye Ulaya ya mashariki na ya mashariki ya kati, Russia ilipinga sera za kidiplomasia za kujichukulia uamuzi, kufuata sera za kidiplomasia zenye ncha nyingi na kuonesha hali ya kujiamini katika shughuli za kidiplomasia. Bw. Lavrov alisema,
"Russia imeimarisha utaratibu wa taifa chini ya uongozi wa rais Vladimir Putin katika miaka karibu minane iliyopita, uchumi wake unaelekea kuwa wa kisasa, kutatua masuala mengi ya jamii, na imeleta uhakikisho kwa ajili ya usalama wa nchi kutokana na kushiriki kwa mapana kwenye ushirikiano wa kimataifa. Kwa mara ya kwanza, Russia kuwa na uwezo, dhamira na nguvu ya kiuchumi ya kutatua masuala mengi. Likiwemo suala jipya la kubeba majukumu mengi zaidi katika shughuli za kimataifa."
Alipozungumzia suala la nyukilia la Iran Bw. Lavrov alisema, masuala matatu kati ya masuala saba yaliyotolewa na shirika la nishati ya atomiki duniani kwa Iran yametatuliwa, na masuala mengine yaliyosalia, yatatatuliwa katika wiki 3 au 4 zijazo. Mswada wa azimio jipya kuhusu suala la nyukilia la Iran ni matokeo ya mazungumzo yaliyofanywa na mawaziri wa mambo ya nje wa nchi 6 katika mji wa Berlin. Mswada wa azimio jipya unazingatia maendeleo ya kazi kati ya shirika la kimataifa la nishati ya atomiki na Iran, haukuagiza kuweka vikwazo vikali dhidi ya Iran, isipokuwa unaimarisha hadhi ya shirika la nishati ya atomiki duniani katika mazungumzo na Iran.
Kuhusu suala la jumuiya ya NATO kujipanua kuelekea mashariki, Bw. Lavrov alisema hayo ni matokeo ya vita baridi, ambayo hayasaidii utatuzi wa suala lolote halisi la usalama. Russia inaamini kuwa hakuna haja muhimu ya upande wa usalama kwa NATO kujipanua kuelekea mashariki, haiwezi kuimarisha usalama wa sehemu yote ya Ulaya, ni kinyume chake kuwa "itazalisha mipaka mipya yenye viwango tofauti vya usalama". Bw. Lavrov alisema, Russia haina wasiwasi kuhusu NATO kujipanua kwenda mashariki, lakini inafuatilia kwa makini mchakato huo.
Bw. Lavrov alisema mujibu na msingi wa kutunga sera za kidiplomasia za Russia ni kuweko ncha nyingi humu duniani, inaona hii inalingana na maslahi ya kimsingi ya Russia na maendeleo ya dunia ya leo. Alisema Russia inapenda kufanya ushirikiano na nchi zote zinazotarajia kufanya ushirikiano nayo juu ya msingi wa usawa na kunufaishana. Russia inataka kutatua masuala nyeti ya kimataifa kwa njia ya majadiliano ya pamoja. Bw. Lavrov alisema,
"Tunaona mwelekeo wa kimsingi wa maendeleo ya dunia ya leo ni kuelekea hali ya kuweko kwa ncha nyingi, ambayo inafanya kazi muhimu kila siku ipitayo katika utatuzi wa masuala ya kimataifa. Tunaona kutatua suala la utulivu wa mkakati wa kimataifa siyo mambo kati ya Russia na Marekani tu, sasa imetokea nafasi ya kuweka kanuni za utulivu wa mkakati wa kimataifa inayoshirikisha nchi zote, hususan nchi za Ulaya ili kuhakikisha usalama wa pamoja. Kwa hiyo, Russia inapendekeza kushirikisha nchi nyingi zaidi wakati wa kujadili masuala kama ya mkataba kuhusu silaha za kawaida za Ulaya, mfumo wa kupambana na makombora na makombora ya masafa ya kati na mafupi."
Alipozungumzia kazi za kidiplomasia za Russia katika mwaka 2008, Bw. Lavrov alisema,
"Kazi muhimu ya kwanza ni kurekebisha vizuri kanuni za usalama wa Ulaya. Na kujenga mfumo wa usalama wa pamoja wa Ulaya."
Bw. Lavrov alisisitiza kuwa Russia haitajitia katika mapambano kwenye suala lolote lile.
|