Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-01-28 19:21:57    
Kutembelea tarafa ya kale ya Rongxiang

cri

Kwenye eneo la delta ya mto Changjiang ya nchini China, mji wa Wuxi unaweza kuhesabiwa kuwa mji wa kale wenye historia ndefu. Hivi sasa ujenzi wa miji umepamba moto kote nchini China, lakini mji wa Wuxi umehifadhi baadhi ya tarafa za kale zenye sura ya asili, kati ya tarafa hizo kuna tarafa ya Rongxiang yenye historia ya miaka karibu 600.

 

Tarafa ya Rongxiang iko kwenye wilaya ya Binhu, iliyoko kwenye kiunga cha magharibi cha mji wa Wuxi, tarafa hiyo ni mahali walipozaliwa wanaviwanda na wafanyabiashara wengi wa China wa vizazi vya miaka ya karibuni. Mwanzoni kabisa, eneo hilo lilikuwa na vijiji vitabu vya Shangrong, Zhongrong na Xiarong. Mkurugenzi wa taasisi ya utafiti ya ukoo wa Rong ya chuo kikuu cha Jiangnan, profesa Chen Wenyuan alisema,

"Ukoo wa Rong ulihamia Jinling, mjini Nanjing kutoka mkoa wa Hubei, halafu ulihamia kwenye mji wa Wuxi katika mwaka wa kwanza wa enzi ya Ming katika karne ya 15. Rong Qing alipohamia huko alikuwa na umri wa miaka zaidi ya 80, alihamia huko pamoja na watoto wake watatu, mahali walipoishi watoto hao watatu, pakawa vijiji vitatu vya Shangrong, Zhongrong na Xiarong. Katika kipindi cha kati cha karne ya 19, eneo la Rongxiang lilikuwa na maendeleo sana, na tarafa ya Rongxiang ilianzishwa rasmi katika miaka ya mwanzoni mwa karne ya 20."

 

Hadi hivi sasa, sehemu ya Rongxiang bado imehifadhi vizuri mtaa wa zamani wenye urefu wa kiasi cha mita 380 na sura ya miaka ya karibuni, pamoja na majengo 157 ya miaka ya karibuni yenye umaalumu wa huko wa vipindi vya historia. Ingawa majengo hayo yana mitindo mbalimbali, lakini karibu yote ni ya ukoo wa Rong. Wataalamu wanasema, hali ya watu wa ukoo mmoja kukaa pamoja na kuendelea kwa pamoja, ni nadra kuonekana kwenye sehemu ya kusini ya mto Changjiang.

Watu wakiingia kwenye mtaa wa zamani wa Rongxiang kutoka kwenye barabara ya Liangxi, na kuangalia kutoka mbali, wanaweza kuona vichochoro vya zamani vimezungukwa na nyumba za wakazi. Lakini mara tu mtu akiingia kwenye mtaa huo wa zamani, ataona kama amerudi katika karne iliyopita. Ataona sura ya kizamani: barabara nyembamba, lango kubwa lenye rangi iliyopauka, na kuta za nyumba za mbao. Katika miaka mia moja iliyopita, majengo yaliyoko kwenye mtaa wa zamani hayakuwa na mabadiliko makubwa, nyumba zilizoko kwenye kando mbili za barabara bado ni za zamani, isipokuwa ustawi wa miaka ya zamani hauonekani tena. Mwalimu mstaafu aliyezaliwa kwenye mtaa wa Rongxiang, Bw. Rong Yaoxiang alisema, mtaa wa Rongxiang ulikuwa na maduka karibu mia moja wakati wenye ustawi, na ulikuwa ni kitovu cha shughuli za biashara kwenye eneo lile la kilomita za mraba kumi kadhaa.Alisema:  

"Karibu kila nyumba ilikuwa na duka, kwa mfano, duka la kinyozi, ingawa mtaa wa Rongxiang siyo mrefu, lakini kulikuwa na maduka 3 au 4 hivi. Zamani hapa palikuwa ni mkahawa wa kifungua kinywa, kule kulikuwa na mkahawa wa chai. Hapa palikuwa ni duka la vifaa vya ujenzi, upande huu kulikuwa ni duka la dawa, ili mradi kila nyumba ya familia moja ilikuwa na duka."

 

Kuna mitindo ya aina tatu ya majengo ya zamani kwenye mtaa wa Rongxiang. Aina ya kwanza ni majengo yaliyojengwa kwa kufuata jadi ya kichina kwa kutumia matofali na mbao, nyumba za aina hiyo zilijengwa kwa ufundi mkubwa; aina ya pili ni nyumba zilizojengwa kwa uunganishaji wa mtindo wa kichina na wa kimagharibi, ambazo kuta za nje ni zenye mtindo wa nchi za magharibi, lakini ndani yake ni zenye milango ya matofali yaliyochongwa nakshi za kisanii; na aina ya tatu ni za mtindo wa kimagharibi kabisa, ambazo zilijengwa kwa zege. Majengo ya aina hizo tatu, yote yanaonekana na mitindo iliyopendwa na wafanyabiashara wa China katika karne ya 19.

Baada ya kutoka mtaa wa zamani wa Rongxiang na kugeukia upande wa magharibi, na kupita kwenye kichochoro chembamba, ni mtaa wa Rongxiangxibang, zamani sehemu hiyo ilikuwa ni magati ya kusafiri kwa wakazi wa Rongxiang waliotaka kuingia mjini au kwenda sehemu ya nje. Mkurugenzi wa zamani wa taasisi ya utafiti ya ukoo wa Rong ya chuo kikuu cha Jiangnan, Bw. Chen Wenyuan alisema, zamani ndugu wawili wa ukoo wa Rong waliokuwa wanaviwanda, walisafiri kwa mashua kutoka hapa kwenda kujifunza ufundi mjini Shanghai.

"Ndugu wawili wa ukoo wa Rong, Rong Zongjing na Rong Desheng waliondoka hapa kwa mashua kwenda Shanghai kujifunza ufundi, walisafiri kwa siku mbili kutwa kucha."

Kwenye shule ya msingi ya Rongxiang iliyoko kwenye mtaa wa Rongxiangxibang kuna jumba la michezo lenye eneo la mita za mraba 400 lililojengwa mwaka 1915. Jengo hilo lenye ghorofa moja lilijengwa kwa zege, sehemu ya chini ni ukumbi wa mikutano, ambayo pia inaweza kutumika kwa michezo, na sehemu ya juu ni kiwanja cha michezo, wanafunzi wanaweza kucheza michezo hata katika siku zenye mvua. Namna yake ni kama jengo moja lisilo na kuta. Mzee Bw. Rong Yaoxiang alisema, jengo hilo la michezo ni la mtindo wa kijapan, mchoro wa usanifu wa jengo hilo ulitolewa na mtaalamu maarufu wa ujenzi wa miradi ya maji, ambaye pia ni mwanataaluma Bw. Hu Yuren, jengo hilo ni jumba pekee la michezo lililojengwa katika miaka ya zamani, na bado linatumika hadi sasa, alisema,

 

"Jengo hilo ni lenye mtindo wa kijapan, Bw. Hu Yuren aliwahi kusoma nchini Japan, hivyo alirudi na mchoro huo wa usanifu. Yaliwahi kujengwa majumba mawili ya michezo kwenye shule, moja katikati ni la chuo kikuu cha ualimu, lakini limebomolewa, jengo letu hilo bado ni zima, na linaendelea kutumika, hili ni jumba pekee la michezo la shuleni lililojengwa katika miaka ya zamani."

Katika tarafa ya Rongxiang, kuna sehemu moja nyingine, ambayo watalii wanapenda kwenda kuangalia, sehemu hii ilijengwa maktaba ya Dagong iliyojengwa na mwanakiwanda mzalendo Bw. Rong Desheng. Maktaba ya Dagong ilianza kujengwa mwaka 1915, ujenzi wake ulikamilika na kuanza kutumika mwaka 1916. Maktaba hiyo ni jengo lenye umbo la mchemraba, ni lenye ghorofa moja na lina mitindo ya kichina na kimagharibi. Rangi ya kuta ya hivi sasa ni nyeupe, na nguzo zake ni za rangi ya kijivu. Takwimu zinasema, Bw. Rong Desheng na kaka yake mkubwa walitumia fedha nyingi kujenga maktaba hiyo na katika shughuli za elimu. Fedha walizotumia katika kujenga shule ya umma na maktaba ya Dagong tu ni dola za fedha (Silver Dollar) milioni moja. Hivyo, maktaba ya Dagong ilikuwa maktaba binafsi iliyochukua nafasi ya kwanza kwa ukubwa, yenye athari na ukamilifu wa usimamizi kwenye sehemu ya Wuxi.