Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-02-19 15:54:30    
Beijing inavyofanya juhudi za kutoa mafunzo kwa ajili ya Michezo ya Olimpiki ya Walemavu

cri
Michezo ya Olimpiki ya Walemavu ya mwaka 2008 itafunguliwa baada ya nusu mwaka mjini Beijing, China. Kila Michezo ya Olimpiki ya Walemavu ni tamasha kubwa kwa walemavu duniani, na michezo hiyo itakayofanyika nchini China itakuwa fursa nzuri kwa maendeleo ya shughuli za walemavu nchini China. Ili kuiandaa michezo hiyo kwa mafanikio, Beijing inafanya maandalizi kwa juhudi kubwa, na kuanzisha kazi ya kutoa mafunzo kwa pande zote.

Ili kufikia kiwango cha juu cha utoaji wa huduma kwa ajili ya Michezo ya Olimpiki ya Walemavu, inapaswa kushughulikia vizuri kazi ya utoaji wa mafunzo. Kikundi cha uratibu wa kazi ya kutoa mafunzo kwa ajili ya Michezo ya Olimpiki ya Beijing, hivi karibuni kilifanya mkutano kuhusu kazi ya kutoa mafunzo kwa ajili ya Michezo ya Olimpiki ya Walemavu. Mkurugenzi wa kikundi hicho Bw. Zhu Shanlu anasema, ikilinganishwa na Michezo ya Olimpiki, Michezo ya Olimpiki ya Walemavu ina umaalum wake kipekee, na hii imeweka kiwango cha juu kwa huduma za wafanyakazi kwa ajili ya michezo hiyo, ni lazima kutoa mafunzo yanayohusika, hatua hiyo itazihimiza shughuli za kutoa huduma na wananchi wawe na mwamko na uwezo wa kuwasaidia walemavu. Bw. Zhu Shanlu ameeleza kuwa, utoaji wa mafunzo kwa ajili ya Michezo ya Olimpiki ya Walemavu una umaalum ufuatao:

"Mafunzo kwa ajili ya Michezo ya Olimpiki ya Walemavu yana undani zaidi wa kitamaduni, yanashirikisha watu kufanya mazoezi halisi, yanaweka kipimo maalum, na yanahusiana na watu wa jamii nzima. Michezo ya Olimpiki ya Walemavu ni shughuli zinazowahusu walemavu, na walemavu wanatakiwa kupewa upendo na heshima."

Bw. Zhu Shanlu ameeleza kuwa, lengo la kazi ya utoaji wa mafunzo kwa ajili ya Michezo ya Olimpiki ya Walemavu ni kutoa huduma vizuri zaidi kwa ajili ya Michezo ya Olimpiki ya Walemavu, na kuimarisha sifa na uwezo wa watu wanaoshughulikia kazi ya maandalizi kwa ajili ya michezo hiyo. Hivyo inapaswa kufuata umaalum wa walemavu, na kutoa mafunzo kwa maofisa, wafanyakazi na watu wanaojitolea wa Michezo ya Olimpiki ya Walemavu.

Mwanzoni mwa mwezi Januari, Idara ya watu wanaojitolea wa Kamati ya Maandalizi ya Michezo ya Olimpiki ya Beijing iliandaa semina ya pili kwa walimu wanaotoa mafunzo kwa watu wanaojitolea kwenye Kituo cha mazoezi ya michezo kwa walemavu wa China. Wakati wa semina hiyo, kuna mafunzo mengi yaliyowashirikisha watu kufanya mazoezi yanayofanana na hali halisi wakati wa Michezo ya Olimpiki ya Walemavu, kama vile namna ya kuwasaidia wachezaji walemavu kuendesha viti vyenye magurudumu. Baada ya semina hiyo, watu wanaojiandaa kuwa walimu watakaotoa mafunzo kwa watu wanaojitolea, watapewa mtihani unaoandaliwa na Idara inayoshughulikia mambo ya watu wanaojitolea ya Kamati ya maandalizi ya Olimpiki ya Beijing, na watu watakaofaulu watakuwa walimu rasmi wa kutoa mafunzo kwa watu wanaojitolea kwenye Michezo ya Olimpiki ya Walemavu.

Watu wapatao 100 wa kujitolea wamejifunza ujuzi mbalimbali kuhusu michezo hiyo, chini ya maelezo halisi ya wataalamu 30. Kati ya mafunzo mbalimbali, uwezo wa kuwasaidia walemavu unawekewa mkazo zaidi. Kwa mfano mafunzo kuhusu kuwafundisha watu wa kujitolea kuendesha viti vyenye magurudumu yalifanyika kwa saa moja. Watu wanaojitolea wanakaribisha sana mafunzo kama hayo, na kujifunza kwa makini kutoka kwa walemavu wanaohitaji misaada. Zhang Sai ni mtu anayejitolea aliyeshiriki kwenye mafunzo hayo, alisema amepata ujuzi mbalimbali unaohusu na utoaji wa huduma kwenye Michezo ya Olimpiki ya Walemavu akisema:

"Naona kuwa nimejifunza mambo mengi kuhusu Michezo ya Olimpiki ya Walemavu, na kupata ufahamu mpya kuhusu michezo hiyo, hususan namna ya kutoa huduma maalum kwa walemavu. Naona kuwa mafunzo hayo yanatupa fursa nzuri ya kushiriki kwenye mazoezi halisi, hatua ambayo inanihimiza nipate maendeleo ya kasi."

Bw. Zhu Shanlu ameeleza kuwa, mazoezi kama hayo ni njia nzuri ya kutoa mafunzo kwa ajili ya Michezo ya Olimpiki ya Walemavu, na wataongeza nguvu katika kazi ya kuwasaidia walemavu kwenye shughuli mbalimbali mjini Beijing. Alisema:

"Tunawahimiza watu wa jamii nzima ya Beijing washiriki na kuhimiza utoaji wa mafunzo kwa ajili ya Michezo ya Olimpiki ya Walemavu. Mafunzo hayo yameanzishwa kati ya watu wanaofanya kazi ya kutoa huduma kwenye viwanja vya ndege, mawasiliano, usalama wa umma, afya, mikahawa na vivutio vya utalii, na yanahusu mambo yanayowasaidia walemavu, na yanafanyika kwa njia ya ana kwa ana, kujifunza mwenyewe na kwa kupitia mtandao wa Internet."

Kwa maoni ya Bw. Zhu Shanlu kiwango cha utoaji wa mafunzo kinategemea uwezo wa walimu. Kikundi cha uratibu wa kazi ya utoaji wa mafunzo kwa ajili ya Michezo ya Olimpiki ya Beijing kitafuata mahitaji ya utoaji wa mafunzo, kuhimiza ujenzi wa uwezo wa walimu, Bw. Zhu Shanlu alisema:

"Tunawahimiza wataalamu wanaoshughulikia kazi ya walemavu na michezo ya walemavu wawe walimu wanaotoa mafunzo yanayohusika, na walimu watakaoshughulikia utoaji wa mafunzo kuhusu maandalizi ya Michezo ya Olimpiki ya Walemavu wanapaswa kufikia kiwango cha juu zaidi. Licha ya kuwachagua walimu wenye uzoefu mkubwa, kikundi cha uratibu cha kazi ya utoaji wa mafunzo kwa ajili ya Michezo ya Olimpiki ya Beijing pia kimetunga mwongozo unaohusika, kama vile vitabu vya ujuzi kuhusu Michezo ya Olimpiki ya Walemavu, aidha kikundi hicho kitaweka malengo mbalimbali ya mafunzo, ili kuhakikisha mafanikio ya utoaji wa mafunzo hayo.

Idhaa ya kiswahili 2008-02-19