Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-01-30 19:33:28    
Mapishi ya choroko ndefu tamu na kamba-mwakaje

cri

Mahitaji

Choroko ndefu tamu gramu 200, kamba-mwakaje gramu 50, pilipili hoho gramu 5, vitunguu maji na vitunguu saumu kila kimoja gramu 5, chumvi gramu 2, chembechembe za kukoleza ladha gramu 2, sosi ya mchuzi gramu 2, maji ya wanga gramu 5

Njia

1. osha choroko ndefu tamu na kamba-mwakaje, halafu washa moto weka vyote kwenye maji joto, halafu pakua. Kata pilipili hoho iwe vipande.

2. washa moto, mimina mafuta kwenye sufuria, tia vipande vya vitunguu maji na vitunguu saumu, korogakoroga halafu tia kamba-mwakaje korogakoroga, tia vipande vya pilipili hoho, korogakoroga, halafu tia choroko ndefu tamu korogakoroga, tia chumvi, chembechembe za kukoleza ladha na mchuzi wa sosi korogakoroga mimina maji ya wanga korogakoroga, ipakue. Mpaka hapo kitoweo hiki kiko tayari kuliwa.