Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-01-31 16:30:59    
Shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa kupunguza kiasi cha vifo vya watoto wenye umri chini ya miaka mitano

cri

Shirika la kuwahudumia watoto la Umoja wa Mataifa tarehe 22 lilitoa ripoti ya hali ya watoto duniani ya mwaka 2008. Shirika hilo limesema, kujenga na kuimarisha mpango wa utunzaji wa afya kwenye maeneo ya mitaa ni hatua muhimu ya kupunguza idadi ya vifo vya watoto hasa watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano, na pia ni hatua muhimu ya kutimiza lengo la milenia la Umoja wa Mataifa kuhusu kupunguza kwa theluthi mbili ya vifo vya watoto wenye umri chini ya miaka mitano hadi kufikia mwaka 2015.

Shirika hilo limetoa ripoti likisema, katika miaka ya hivi karibuni nchi mbalimbali duniani zimeunda mfumo wa matunzo ya afya kwenye maeneo ya mitaa, na kupata maendeleo makubwa katika kutoa humuda za kimsingi za afya na chanjo ya kinga, kuhamasisha kina mama kunyonyesha watoto, na kutetea kutumia chumvi yenye madini ya joto, na kupunguza idadi ya vifo vya watoto wenye umri chini ya miaka mitano. Katika mwaka 2006 idadi ya watoto wenye umri chini ya miaka mitano waliokufa ilifikia milioni 9.7 duniani, ambayo ni idadi ndogo kabisa katika historia.

Ripoti zinasema, kutokana na juhudi zilizofanywa na pande mbalimbali, ugonjwa wa ndui umetokomezwa duniani, na ugonjwa wa surua na polio pia unadhibitiwa kwa ufanisi. Idadi ya watoto wenye utapiamlo katika nchi mbalimbali inapungua, na kuboreshwa kwa hali ya maji, mazingira ya afya na afya ya watu pia kumesaidia kupunguza magonjwa ya malaria.

Ripoti hiyo pia inasema, hivi sasa kila siku watoto elfu 26 duniani wanakufa. Wengi kati yao ni kutokana na magonjwa ambayo yanaweza kuzuilika. Watoto wote hao wanaishi katika nchi zinazoendelea, na idadi ya watoto wenye umri chini ya miaka mitano wanaokufa katika sehemu ya kusini mwa Sahara, ni nusu ya idadi hiyo ya duniani.

Shirika la kuwahudumia watoto la Umoja wa Mataifa limeeleza kuwa, sehemu ya kusini mwa Sahara, hasa sehemu ya magharibi na katikati ya Afrika itapewa kipaumbele katika kazi zake za baadaye. Aidha, shirika hilo litatilia maanani zaidi kwa sehemu ya Asia ya Kusini ambayo ina vifo vyingi vya watoto na nchi zenye upungufu wa matunzo ya afya ya kimsingi.

Ripoti hiyo pia inasema, katika miaka ya hivi karibuni serikali ya China imepata maendeleo makubwa katika kupunguza idadi ya vifo vya watoto.

Kuanzia mwaka 1990, idadi ya vifo vya watoto wenye umri chini ya miaka mitano nchini China imepungua kwa asilimia 50, na kasi ya kupungua kiasi hicho ni mara moja kuliko wastani wa kiasi cha duniani.

Mwaka 2006 idadi ya vifo vya watoto wenye umri chini ya miaka mitano ilikuwa ni asilimia 2.1, ni chini kabisa kuliko idadi ya wastani ya nchi zinazoendelea ya asilimia 7.9.

Mjumbe wa shirika la afya duniani WHO nchini China Bw. Han Zhuosheng alisema, kupunguzwa kwa idadi ya vifo vya watoto nchini China kutokana na uwekezaji mkubwa wa serikali ya China kwenye shughuli za afya ya umma na utungaji wa hatua za uhakikishaji wa matibabu na mpango wa kifedha wa afya. Habari zinasema kuanzia mwaka 1987 idadi ya vifaa vya afya vya China inaongezeka kwa asilimia 82, na idadi ya wafanyakazi wa idara za afya inaongezeka kwa asilimia 88.

Idadi ya vifo vya watoto ni alama ya maendeleo ya nchi, na ni uhakikisho wa ufanisi wa maendeleo ya nchi. Umoja wa Mataifa unathibitisha kupunguza kiwango hicho kuwa moja kati ya mambo manane ya lengo la Milenia.

Ripoti hiyo pia inasema, nchini China vifo vingi vya watoto ambavyo vinaweza kuepukika vinatokea katika sehemu za mbali na za mipakani zenye matatizo ya kiuchumi ambazo zina upungufu wa huduma za matunzo ya afya kwa akina mama na watoto, hivyo idadi ya vifo vya watoto katika sehemu hizo ni kubwa kuliko idadi ya mijini.

Mkuu wa ofisa wa kituo cha matunzo ya afya kwa akina mama na watoto cha nchini China Bw. Shi Qi alisema, kadiri mageuzi ya mfumo wa matibabu wa China yanavyofanyika kwa kina ndivyo mfumo wa matibabu kwenye mashina za vijiji unavyokamilika siku hadi siku, na idadi ya vifo vya watoto wachanga katika sehemu za mbali na za mipakani zenye matatizo ya kiuchumi pia itapungua zaidi.

Lakini ripoti hiyo pia inasema kasi ya kupunguza idadi ya vifo vya watoto wa nchini China sasa inapungua.

Idhaa ya kiswahili 2008-01-31