Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-02-01 19:18:51    
Makampuni ya China barani Afrika na jamii za huko zatimiza kunufaishana

cri

   

Kutokana na kuendelea kwa uhusiano wa pande mbili kati ya China na Afrika na kuongezeka kwa mawasiliano yasiyo ya kiserikali siku hadi siku, wafanyabiashara wengi wa China wanapenda kuwekeza barani Afrika. Makampuni ya China yanaongeza uwekezaji barani Afrika na pia yanatoa mchango mkubwa kwa jamii za huko na kutoa mchango katika kuongeza ajira na kodi kwa serikali, pande hizo mbili zinanufaishana vizuri.

Takwimu zinaonesha kuwa, hadi kufikia mwishoni mwa mwaka 2006, uwekezaji wa China katika sekta mbalimbali za Afrika umefikia dola za kimarekani bilioni 11.7 na China imekuwa nchi inayoendelea ambayo uwekezaji wake barani Afrika ni mkubwa kabisa, na katika miaka ya hivi karibuni kati ya uwekezaji huo, kiasi cha uwekezaji kutoka makampuni binafsi kimekuwa kinaongezeka kwa haraka.

Urafiki kati ya China na Afrika ni wa jadi, waafrika wengi wanakaribisha makampuni ya China, na kutokana na bidhaa za China kuwa ni zenye sifa nzuri na bei nafuu, hivyo zinakaribishwa na watumiaji wa Afrika. Takwimu zinaonesha kuwa, mwaka 2006 mapato ya uuzaji wa kampuni ya teknolojia ya Huawei ya Shenzhen barani Afrika yalifikia dola za kimarekani bilioni 2.08, na biadhaa na huduma zake zimeingia kwenye nchi karibu na 40 za Afrika. Hali kadhalika, manufaa ya kampuni kuu ya vyombo vya umeme ya China katika soko la Afrika yamekuwa mara 5 ya soko kamili. Makampuni ya vyombo ya umeme ya nyumbani ya China kama Haixin, Haier pia yamepata mafanikio na sifa nzuri.

Sifa ya uwekezaji wa makampuni ya China barani Afrika inaonekana katika sehemu zifuatazo: kwanza, katika miaka mingi iliyopita, uhusiano wa kisiasa kati ya China na Afrika umekuwa ni mzuri na uliweka msingi thabiti kwa ushirikiano na uwekezaji wa pande hizo mbili; pili, China na nchi za Afrika zinasaidiana katika maliasili, mazao, soko na wafanyakazi, na mazingira hayo yametoa fursa nyingi za uwekezaji kwa makampuni ya China; tatu, makampuni ya China yamesaidia kujenga miradi ya serikali ya China na mashirika ya kimataifa barani Afrika, hivyo yanajua hali ya kisiasa, kiuchumi na soko la Afrika, na yana uzoefu wa uwekezaji; nne, serikali ya China inachukua hatua za kuunga mkono makampuni ya China kwenda kuwekeza barani Afrika. Katika kipindi cha mkutano wa wakuu wa baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika uliofanyika hapa Beijing mwaka 2006, serikali ya China ilitangaza hatua za kusukuma mbele ushirikiano wa kiuchumi na biashara kati ya China na Afrika na kutoa fursa mpya ya kuwekeza kwa makampuni ya China barani Afrika.

Wakati makampuni ya China yanapopata mafanikio kwa kufanya kuwekeza barani Afrika, pia yanatoa mchango kwa jamii ya huko, na kupata maslahi ya kijamii na kiuchumi. Kampuni ya Zhongxing iliingia kwenye soko la Afrika miaka 10 iliyopita, hivi sasa imeanzisha vituo zaidi 10 vya kutoa mafunzo nchini Afrika Kusini na Angola, na kila mwaka vinatoa mafunzo kwa maelfu ya mafundi na wasimamizi wa makampuni ya Afrika yanayoshirikiana na kampuni hiyo, na baadhi ya wafanyakazi hao waliofundishwa wanafanya kazi kwenye ofisi ya usimamizi wa kampuni ya Zhongxing barani Afrika.

Kampuni ya madini ya Afrika ni tawi la kampuni ya China linalochimba shaba nyekundu nchini Zambia. Kampuni hiyo inatilia maanani kuanzisha uhusiano mzuri na jamii ya huko, na katika miaka miwili iliyopita zimeanzisha harakati nyingi za kunufaisha wakazi wa huko. Mkurugenzi mmoja wa kampuni hiyo Bw. Xu Ruiyong alieleza kuwa kampuni hiyo ilipanga kutenga dola za kimarekani bilioni 7 kwa ajili ya ukarabati wa barabara moja na hospitali moja mwaka huu na kujenga vituo vinne vya mabasi kwenye miji mitatu ya kwenye vitongoji, na kutoa zana tatu za mazoezi ya kujenga mwili kwenye makazi ya watu. Kampuni hiyo pia inashiriki kwenye harakati ya kuchangisha fedha na kushiriki kwenye harakati za siku ya mazingira ya kimataifa, siku ya ugonjwa wa ukimwi na kutoa fedha za msaada.

Ukumbi wa mkutano wa kimataifa wa Sudan uliojengwa na kampuni ya miradi wa ujenzi ya Shanghai mwezi Aprili mwaka 2005, ulikabidhiwa rasmi kwa serikali ya Sudan, na mikutano mikubwa ya kimataifa imefanyika kwenye ukumbi huo. Hivi sasa, uhusiano kati ya China na Afrika unaelekea kuendelea kwenye sekta mbalimbali, kuimarika na kunufaishana na makampuni ya China kunatoa mchango mkubwa zaidi katika kusukuma mbele maendeleo ya uhusiano kati ya China na Afrika.

Habari nyingine zinasema kampuni ya ujenzi ya China inapata uaminifu kutoka kwa wananchi wa Msumbiji. Jumba la wizara ya mambo ya nje, kituo cha mkutano wa kimataifa, kituo cha duka kubwa, na ukifanya utalii mjini Maputo nchini Msumbiji, unaweza kuona majengo mazuri yaliyojengwa na kampuni ya ujenzi ya China. Siyo mjini Maputo tu, hata kwenye sehemu nyingine za Msumbiji unaweza kuona busara na moyo wa kufanya kazi kwa bidii wa wahandisi wa China, zikiwemo barabara kuu la nambari 1, na miradi mingi ya utoaji wa maji kwenye miji mingi nchini kote.

Ofisa mwandamizi wa miradi ya viwanda ya idara ya kuhimiza uwekezaji wa Msumbiji Bw. Tobo, alisema watu wa Msumbiji wanaheshimu shughuli zinazofanywa kwa ustadi na kampuni ya ujenzi ya China. Kuna makampuni mengi ya ujenzi ya China nchini Msumbiji na yanapendwa na kuaminika nchini Msumbiji kutokana na utaalamu wa kiwango cha juu na moyo wa kufanya kazi kwa bidii. Miradi ya jengo la bunge la Msumbiji, kituo cha mikutano ya kimataifa, jengo la wizara ya mambo ya nje yaliyojengwa kwa msaada wa kampuni ya Hua'an ya China ilimalizika kwa mpango uliowekwa, na yote ina sifa nzuri.

Kutokana na sifa ya miradi hiyo, kampuni ya Hua'an inaaminiwa na serikali ya Msumbiji, na ilipata miradi mingi zaidi ya ujenzi, ikiwemo mradi wa upanuzi wa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Maputo, mradi wa kukarabati ikulu ya Msumbiji na jengo la wizara ya habari ya taifa.

Makampuni ya China yalipokwenda Msumbiji, serikali ya huko ilikuwa na wasiwasi na uwezo wao. Idara ya kampuni ya ushirikiano wa kimataifa ya Henan ya China nchini Msumbiji ilipogombea kandarasi ya mradi wa kujenga daraja moja, wawakilishi wa Msumbiji hawakujua uwezo wa kampuni hiyo. Mkurugenzi wa idara hiyo Bw. Lin ming aliwaalika wawakilishi hao kutembelea China na kutembelea ujenzi wa daraja mjini Shanghai na kuondoa wasiwasi wao kuhusu utaalamu wa ujenzi wa China.

Hata katika ushindani na kampuni za nchi za Magharibi, makampuni ya ujenzi ya China pia yanafanya vizuri. Kwa mfano, barabara kuu nambari moja ya Msumbiji ilijengwa na makampuni ya nchi kadhaa za nje, ikiwemo kampuni ya ushirikiano wa kimataifa ya Henan ya China. Lakini sehemu nyingi za barabara hiyo zilizojengwa na makampuni ya nchi nyingine zilirudiwa kujengwa tena, lakini sehemu iliyojengwa na kampuni ya China ilijengwa mara moja tu na ina sifa nzuri. Waziri wa ujenzi wa Msumbiji alisifu akisema: "sehemu ya barabara hiyo iliyojengwa na kampuni ya China ni nzuri kabisa."