Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-02-05 16:17:58    
Watu wa kabila la Wasala wanaoishi mkoani Qinghai

cri

Kwenye sehemu ya juu ya Mto Huanghe, kuna kabila dogo la Wasala linaloamini dini la Kiislamu na lenye historia ya zaidi ya miaka 800. Watu wa kabila hilo hasa wanaishi kwenye wilaya inayojiendesha ya kabila la Wasala la Xunhua mkoani Qinghai. Leo tutawaletea maelezo kuhusu watu wa kabila hilo.

Ili kutembelea wilaya ya Xunhua, mwandishi wetu wa habari aliendesha gari kutoka Xi'ning, mji mkuu wa Qinghai, na kuelekea milimani kwa upande wa kusini mashariki. Baada ya kupita genge la Lamu, mandhari nzuri ilimvutia mara moja, aliona maji ya Mto Huanghe yalikuwa yakitiririka kwa nguvu kutoka kwenye genge. Wilaya ya Xunhua iliyoko kando ya Mto Huanghe ingawa iko kwenye uwanda wa juu wa Qinghai, lakini hali ya hewa ya sehemu hiyo ni nzuri kutokana na mtiririko wa mto huo.

Tarafa ya Jiezi ya wilaya ya Xunhua ni mahali ambapo wahenga wa watu wa kabila la Wasala waliweka maskani yao mwanzoni, hivyo tarafa hiyo ina umaalumu mkubwa zaidi wa kabila la Wasala. Katikati ya barabara kuu ya tarafa hiyo, kuna sanamu moja ya ngamia mweupe iliyotengenezwa kwa mawe. Watu wa kabila la Wasala wanamchukulia ngamia mweupe kama ni ishara ya kabila hilo. Hadithi ya ngamia mweupe kubadilika kuwa jiwe inasimuliwa mara kwa mara kwenye sehemu ya Xunhua, hadithi hiyo inahusu namna ya watu wa kabila la Wasala walivyohamia kwenye sehemu hiyo kutoka Asia ya Kati.

Inasemekana kuwa zaidi ya miaka 800 iliyopita, kulikuwa na kabila moja lililoamini dini ya Kiislamu kwenye sehemu ya Asia ya Kati. Kiongozi wa kabila hilo alichukiwa sana na mfalme wake, ili kuepuka na maafa, kiongozi huyo aliamua kuwaongoza watu wa kabila hilo kuhamia upande wa mashariki, kwa lengo la kutafuta sehemu yenye amani na maisha bora, wakafunga safari wakiandamana na ngamia mmoja mweupe. Baada ya kupita milima mirefu, majangwa makubwa na matatizo mengine mengi, walifika kwenye sehemu chini ya mlima moja wenye ardhi nyekundu kando ya Mto Huanghe. Wakati huo waligundua kwamba ngamia wao aliyekuwa amebeba kitabu muhimu cha Kurani kilichoandikwa kwa mikono na maji na udongo waliochukua kutoka nyumbani kwao ametoweka, walimtafuta usiku kucha, hatimaye walimpata kando ya chemchem ya maji, ngamia huyo mweupe alikuwa amebadilika kuwa jiwe, lakini vitu ailvyokuwa amebeba havikuharibika. Watu wa kabila hilo walistaajabu sana, ambapo waliona maji na udongo waliochukua kutoka nyumbani kwao, hauna tofauti hata kidogo na ule wa sehemu hiyo. Watu hao waliamini kuwa huo ni uamuzi wa mungu, wakapiga kambi na kujenga makazi kando ya chemchem hiyo ya maji, na chemchem hiyo ikaitwa Chemchem ya maji ya Ngamia. Wao ndio wahenga wa kabila la Wasala, na sehemu iliyochaguliwa sasa ni sehemu inayoitwa Xunhua. Baada ya kuweka makazi yao, watu hao walioana na watu wa makabila mengine, hivi sasa kabila hilo limekuwa na idadi ya watu zaidi ya laki moja.

Kitabu cha Kurani kwenye hadithi hiyo kilithibitishwa na wataalumu wa historia kuwa ni kitabu cha kale zaidi cha Kurani kilichoandikwa kwa mkoni nchini China, inakadiriwa kuandikwa kati ya karne 8 hadi karne 13. Sasa kitabu hicho chenye thamani kubwa kiko wapi? Mwalimu wa shule ya tarafa ya Jiezi Bw. Huang Jiquan alimwambia mwandishi wetu wa habari kuwa, kitabu hicho kinahifadhiwa kwenye jengo lililoko karibu na Chemchem ya Ngamia, alisema,

"Hii ndiyo sehemu ambayo kitabu cha Kurani kilichoandikwa kwa mikono cha kabila la Wasala kinahifadhiwa. Hivi sasa kuna vitabu vitatu vya Kurani vilivyoandikwa kwa mkono duniani, na hiki ni kimoja kati ya vitabu hivyo."

Watu wa kabila la Wasala walijenga nyumba zao kando ya Mto Huanghe, pia walianzisha utamaduni na sanaa yenye umaalumu wao.

Wapendwa wasikilizaji, mliosikia ni muziki uliopigwa na mzee Han Zhanxiang ambaye ni msanii wa kabila la Wasala kwa kinanda cha muziki cha Kouxian. Kouxian ni kinanda kidogo cha muziki chenye historia ndefu na umaalumu wa kabila hilo, kina urefu wa sentimita karibu mbili tu na hutengenezwa kwa shaba au fedha. Kouxian inapigwa kwa ulimi, hivyo inaweza kutoa muziki wa sauti ya chini tu, lakini muziki huo unapendwa sana na watu wa kabila la Wasala hasa wanawake. Zamani mtu wa kabila hilo alipiga Kouxian peke yake wakati wa usiku mara kwa mara, ili kuondoa wasiwasi, na kueleza hisia zake moyoni.

Kuimba nyimbo za Huer ni njia nyingine muhimu kwa watu wa kabila la Wasala kueleza hisia zao. Bw. Han Zhanxiang pia ni mwimbaji hodari wa Huer, alipokuwa kijana alianza kujifunza kuimba nyimbo hizo. Alipozungumzia nyimbo za Huer, Bw. Han Zhanxiang alisema,

"Watu wa kabila la Wasala wana lugha yao, lakini hawana maandish. Hivyo historia na utamaduni wa kabila letu unadumishwa mdomo kwa mdomo. Huer ya kabila la Wasala ni tofauti na ya sehemu nyingine, ina aina nyingine kwenye sehemu ya Xunhua, na zile zinazoimbwa zaidi ni nyimbo za aina 63. Baadhi ya nyimbo za Huer zinasifu maskani yetu, na nyingine zinawasifu watu wa kabila la Wasala."

Bw. Han Zhanxiang aliposema, alikuwa na furaha sana, na aliimba wimbo wa Huer.

Wimbo huo uliimbwa hivi Spring inakuja, maskani kwa watu wa kabila la Wasala ina mandhari nzuri, mimea ya ngano inapendeza, maua yanachanua vizuri na milio ya ndege inawavutia sana watu. Wimbo huo wa Huer umetuelezea mandhari nzuri ya Xunhua, na maisha mazuri ya watu wa kabila la Wasala.

Idhaa ya kiswahili 2008-02-05