Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-02-05 20:11:53    
Meneja mkuu wa kampuni inayoshirikiana na China kutengeneza ndege zinazofanya safari kwenye matawi ya njia

cri

Ukikutana na Bw. Roberto Rossi de Souza kwa mara ya kwanza, huenda utafikiri yeye ni profesa mwangwana na mpole anayefundisha fasihi kwenye chuo kikuu badala ya meneja mkuu wa kampuni ya Embraer. Alisema katika muda mrefu uliopita alikuwa na matumaini kuwa atatembelea China, ambayo ni nchi kubwa yenye historia ndefu na watu wengi. Alitimiza matumaini hayo alipokuwa na umri wa miaka zaidi ya 60. Hivi sasa Bw. Souza ameishi nchini China kwa miaka miwili.

Kabla ya miaka mitatu iliyopita, shirika la ndege la Brazil na kampuni ya kutengeneza ndege ya Harbin ya China ziliunda kampuni ya ndege ya Embraer ya Harbin. Hii ni mara ya kwanza kwa China na Brazil kushirikiana kwenye utengenezaji wa ndege zinazofanya safari kwenye matawi ya njia. Mhandisi Roberto Rossi de Souza alishika cheo cha meneja mkuu wa kampuni hiyo kwa furaha. Kabla ya miaka kadhaa iliyopita, Shirika la ndege la Brazil lilifanya utafiti kuhusu soko la safari za ndege kwenye matawi ya njia, Bw. Souza alipata habari nyingi kuhusu mahitaji ya ndege hizo nchini China yanayoongezeka siku hadi siku. Alipozungumzia soko hilo lenye uwezo mkubwa wa kupata maendeleo, alisema,

"Tulilinganisha soko la safari za ndege kwenye matawi ya njia nchini China na masoko ya nchi nyingine, kwa mfano, ndege hizo zinachukua asilimia 40 ya soko la usafiri wa ndege nchini Marekani, lakini zinachukua asilimia 7 nchini China, hivyo soko la China lina uwezo mkubwa wa kupata maendeleo. Tunaona kuwa shughuli za usafiri wa ndege zitaendelea kuongezeka haraka kwa miaka 10 hadi miaka 20 ijayo nchini China, yaani mwelekeo huo utaendelea hadi mwaka 2020, hayo ni maoni ya pamoja ya mashirika ya ndege ya Brazil na kampuni ya utengenezaji wa ndege ya Harbin."

Bw. Souza anaona kuwa teknolojia za kisasa za kiwanda cha kutengeneza ndege cha Harbin ni sababu muhimu ya kujenga kiwanda hicho mjini humo, alisema,

"Kampuni zote mbili zina uwezo mkubwa kwenye utengenezaji wa ndege. Kampuni ya utengenezaji wa ndege ya Harbin iko mjini humo, tunaweza kutumia baadhi ya mashine za kampuni hiyo, ambazo zimerahisisha kazi zetu. Shughuli za utengenezaji wa ndege zimefanyika mjini Harbin kwa muda mrefu, na kampuni ya utengenezaji wa ndege ya Harbin ina wafanyakazi wengine wenye uzoefu mkubwa kuhusu utengenezaji wa ndege, hiyo inamaanisha kuwa tunaweza kupata teknolojia na maarifa hapa."

Kutokana na sababu hizo, miaka 6 iliyopita China na Brazil zilisaini mkataba, na nchi hizo mbili zilianza kushirikiana katika kutengeneza ndege zinazofanya safari kwenye matawi ya njia. Baada ya kampuni hiyo kuanzishwa, Bw. Souza anaona kuwa suala linalohitaji kutatuliwa mapema ni ushirikiano kati ya mafundi wa nchi hizi mbili. Hivyo hatua ya kwanza iliyochukuliwa na kampuni hiyo ni kuwapatia wafanyakazi mafunzo ya lugha ya Kiingereza. Alisema,

"Nafikiri suala la kwanza ni lugha, yaani kutatua suala la mawasiliano kati ya wafanyakazi wa nchi mbili. Kwenye kampuni yetu, Kiingereza ni lugha ya pili ya Wachina na Wabrazil. Hivyo tunatilia maanani kuinua uwezo wa wafanyakazi katika kuzungumza lugha ya Kiingereza. Tumeanzisha darasa la Kiingereza na kutoa mafunzo kwa wafanyakazi. Hatua hiyo imepata mafanikio, sasa naweza kuzungumza na wafanyakazi wengi kwa Kiingereza."

Baada ya kutatua suala la mawasiliano, Bw. Souza pia anafanya juhudi kubwa katika kuanzisha utamaduni wa kampuni hiyo, alisema,

"Tumegundua tofauti kati ya utamaduni wa China na Brazil, hivyo tumewaalika wataalamu wa Brazil kufanya utafiti kuhusu utamaduni wa China, na kujenga mtizamo kuhusu thamani ya mambo wa kampuni yetu, ili kujenga uhusiano mzuri kati ya Wachina na Wabrazil, na kupata maendeleo kazini. Kwa mujibu wa mtizamo huo kuhusu thamani ya mambo, tunaheshimu watu na utamaduni tofauti, tunasisitiza kutilia mkazo sifa na usalama wa matumizi ya bidhaa zetu."

Baada ya kuwa na mtizamo kuhusu thamani ya mambo na utamaduni wa kampuni hiyo, shughuli za kampuni hiyo zinapata maendeleo hatua kwa hatua, kiwango cha teknolojia cha wafanyakazi wa China pia kimeinuka haraka. Kuanzia nusu ya pili ya mwaka 2003 ambapo kampuni hiyo ilitengeneza ndege ya kwanza aina ya ERJ145, hadi mwishoni mwa mwaka 2004, ambapo kampuni hiyo imetengeneza ndege tano, mafundi wa Brazil wamepungua kuwa 6 kutoka 54. Licha ya teknolojia za kisasa za Shirika la ndege la Brazil, kampuni hiyo pia imewafundisha Wachina njia mpya ya usimamizi. Bw. Jiang Da ambaye ni naibu meneja mkuu wa kampuni ya Embraer alisema,

"Tumejifunza mengi kutoka kwa mradi huo wa ushirikiano. Kwa mfano, mradi huo unahusu usimamizi wa uchukuzi wa bidhaa duniani. Makampuni 670 yanatengeneza ndege aina ya ERJ145 duniani, na makampuni zaidi ya 200 yaliyoko Marekani, Ulaya, na Amerika ya Kusini yanatengeneza ndege moja kwa moja. Mstari wa utengenezaji ulijengwa kwa mujibu wa wazo la kampuni ya Brazil, ambao unaweza kusimamiwa mara moja wakati wa utengenezaji. Hii ni njia muhimu ya kutengeneza ndege kwa ufanisi mkubwa na gharama ndogo kwenye viwanda vingi vya nchi za nje, ambayo bado ni mpya nchini China."

Hadi hivi sasa kampuni ya Embraer imetengeneza ndege karibu 20 kwa ajili ya mashirika ya ndege ya China. Bw. Souza anaridhika na mafanikio hayo, na ana matumaini makubwa kuhusu ushirikiano kati ya China na Brazil, alisema,

"Ushirikiano huo umepata mafanikio makubwa, na kazi zote zinaendelea vizuri. Ni wazi kuwa kutokana na soko kubwa nchini China na ongezeko kubwa la soko hilo, tuna mustakabali mzuri sana. Nafiriki tumepata mwenzi mzuri wa ushirikiano."

Mwishowe, Bw. Souza alisema alikuja China kutoka Brazil ambayo iko kwenye Ikweta, lakini amezoea maisha nchini China, na anapenda mji wa Harbin ulioko kaskazini mwa China. Wachina wenye ukarimu mkubwa, ni sababu muhimu kwake yeye kuweza kufanya kazi mjini humo.