Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-02-10 18:32:56    
Dada aliyeanzisha bendi ya muziki za kabila la wadong

cri

Wu Hui mwenye umri wa miaka 22, alizaliwa katika kijiji kimoja cha wilaya ya Liping, mkoani Guizhou. Alipokuwa mtoto, hali ya kiuchumi ya familia yake haikuwa nzuri, hivyo yeye alimwaachia dada yake fursa ya kwenda shule. Baada ya hapo, yeye alijiunga na kikundi cha sanaa ya nyimbo za kabila la Wadong cha Liping kutokana na sauti yake nyororo.

Mwaka 2005 Wu Hui alianzisha kikundi cha nyimbo za kabila la Wadong pamoja na wasichana wengine wanne. Wasichana hao walishiriki kwenye mashindano ya kuimba nyimbo ya Guizhou. Wu Hui na wenzake walipata nafasi ya pili katika mashindano hayo. Baada ya mashindano hayo, idara husika ya mkoa wa Guizhou iliwapeleka wasichana hao kwenye chuo cha sanaa cha chuo kikuu cha Guizhou kujifunza uimbaji bila kulipa. Wu Hui alisema,

"Fursa hii imebadilisha maisha yangu. Wakati nilipoarifiwa kuwa nimekubaliwa kusoma kwenye chuo hicho, nilifurahi sana na hata nilitokwa na machozi."

Katika chuo kikuu cha Guizhou, Wu Hui na wenzake 12 wa makabila madogomadogo kutoka sehemu mbalimbali za China wanafuatiliwa sana. Wu Hui na wasichana wengine wa kabila la Wadong waliishi katika bweni moja. Kila usiku walikuwa wanaimba bwenini.

Lugha ya Kabila la Wadong haina maandishi, hivyo desturi, utamaduni na shughuli nyingine zinapaswa kurithiwa kwa uimbaji wa nyimbo wa kabila hilo kizazi hadi kizazi. Sasa Wu Hui pamoja na wenzake walifanya kazi ya kuratibu na kurekodi nyimbo hizo. Licha ya hayo, wanaona kuwa, wanamuziki walianza kupiga muziki ya makabila madogomadogo kwa mitindo kadha wa kadha ya maonesho ya muziki, ili kuzifanya nyimbo za makabila madogomadogo zifurahishe watu wengi zaidi. Wu Hui alisema anataka kuwa na uvumbuzi katika maonesho ya nyimbo za Kabila la Wadong. Alisema,

"Ni lazima kudumisha mtindo wa jadi wa nyimbo za kabila la Wadong. Lakini watazamaji watachoka baada ya kusikiliza nyimbo chache katika maonyesho ya muziki. Tuna matumaini ya kuwa na mwalimu mmoja kutufundisha kudumisha umaalumu wa nyimbo za kabila la Wadong na pia kufanya uvumbuzi. Kwa sababu watazamaji wengi hawaelewi lugha yetu, kama nyimbo zinaimbwa kwa mtindo mpya, wanaweza kuburudishwa zaidi."

Kutokana na kuimba nyimbo za kabila la Wadong, Wu Hui aliweza kujiunga na chuo kikuu, na pia alifanya sauti yake ijulikane kote nchini na hata duniani. Yeye akiwa mmoja kwenye kikundi cha nyimbo na ngoma kufanya ziara katika sehemu nyingi za China, pia walikwenda Russia, Ukraine, Uholanzi kuonesha nyimbo za kabila la Wadong kwa watazamaji wa nchi za nje.

Mkoa wa Guizhou ulifanya matamasha mbalimbali ambapo watu wengi wenye uwezo wamejitokeza na kupata fursa ya kusoma katika chuo kikuu, vile vile unahimiza kuendeleza sanaa za makabila madogomadogo. Wu Hui alisema, sasa watu wengi zaidi wanajua nyimbo za kabila la Wadong, kwa sababu watu wengi wanapenda kwenda kutalii kwenye maskani yake. Yeye na watu wa nyumbani kwake wanahisi mabadiliko ya maisha yanayoletwa na utamaduni wa kabila lao. Alisema,

"Nchi yetu inatilia maanani zaidi kuendeleza utamaduni wa makabila madogomadogo, tuna matumaini kuwa utamaduni wa kabila letu unaweza kuenziwa na kurithiwa daima dawamu."

Idhaa ya kiswahili 2008-02-10