Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-02-11 18:11:30    
Utamaduni wa wanyama 12 wanaowakilishi miaka

cri

Katika kalenda ya kilimo ya China, kila mwaka unawakilishwa na mnyama mmoja, kuna jumla ya wanyama kumi na wawili wanaowakilisha miaka 12, na kila miaka 12 ni duru moja. Kuanzia tarehe 7 Februari mwaka 2008 tumeingia katika "mwaka wa panya". Makala hii inahusu wanyama hao 12 na "panya".

Tunapotaja "panya" pengine unaweza kukumbuka Mickey Mouse wa Disneyland na filamu ya katuni "Paka na panya".

"Panya" unayezungumzia ni panya anayejulikana duniani, lakini panya katika kipindi hiki ni "panya" wa China anayewakilisha mwaka. Kwa nini Wachina wanatumia panya kuwakilisha mwaka, na kuna masimulizi gani yanaymhusu "panya" huyo, hebu tueleze.

Kabla ya kueleza kuhusu "mwaka wa panya" nataka kuwaeleza kuhusu wanyama 12 wanaowakilisha miaka. Wachina wanatumia wanyama wa aina 12 kuwakilisha miaka, wanyama hao licha ya panya wengine ni ng'ombe, chui, sungura, dragoni, nyoka, farasi, mbuzi, kima na kuku.

Matumizi ya wanyama wa aina 12 kuwakilisha miaka yalianza katika enzi ya Spring na Autumn katika historia ya China, yaani karne ya 6 K.K. na ilipokuwa katika karne ya 5 na 6 matumizi hayo yalikuwa yameenea kote nchini China. Wahenga wa China licha ya kutumia wanyama wa 12 kuwakilisha miaka, pia walitumia wanyama hao kuwakilisha miezi na muda ya saa.

Wachina wanawaunganisha wanyama wawili wawili kuwa kikundi kimoja kwa kuonesha matumaini yao. Kwa mfano:

Panya na ng'ombe wako katika kundi moja. Panya anawakilisha akili, ng'ombe anawakilisha juhudi za kazi. Wahenga wa China waliona kuwa, mtu akiwa na akili tu bila juhudi za kazi atakuwa mtu asiye na akili timamu, na mtu akiwa na juhudi tu bila akili atakuwa mjinga, kwa hiyo ni lazima awe mtu mwenye sifa zote hizo mbili.

Chui na sungura wako katika kundi moja. Chui anawakilisha ujasiri na ukali, na sungura anawakilisha tahadhari. Mtu anayeounganisha sifa zote hizo mbili atakuwa mtu mwenye ujasiri na makini. Kama mtu akiwa na ujasiri bila kuwa na tahadhari, atakuwa mtu mwenye ujasiri wa kujihatarisha, na akiwa mwenye tahadhari tu atakuwa mwoga.

Farasi na mbuzi wako katika kundi moja. Farasi anawasilisha kusonga mbele bila kusimama, na mbuzi anawakilisha upole na kuwa na makini kuangalia mazingira yaliyo karibu naye. Mtu akisonga mbele tu bila kuangalia mazingira yaliyo karibu naye atajigongagonga, na mwishowe atapotea njia. Lakini akiangalia tu mazingira tu bila kusonga mbele atashindwa kufikia lengo lake. Kwa hiyo ni lazima mtu awe na sifa zote mbili hizo.

Kutokea kwa matumizi ya wanyama wa aina 12 kuwakilisha miaka kunahusika na unajimu. Katika jamii ya kale, wahenga wa China waligundua majira ya baridi na joto yanarudia rudia, na pia waligundua kwamba mwezi unapopevuka mara 12 ni mwaka mmoja, kwa hiyo wanyama wanaowakilisha miaka wamewekwa wa aina 12.