Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-02-13 19:47:16    
Nyimbo za jadi za kichina zaonesha upendo wa wageni kwa China

cri

Mashindano ya fainali ya kuimba ya wanafunzi wa nchi za nje wanaosoma nchini China ya kombe la Laihua kwa mwaka 2007, yalifunguliwa rasmi huku wimbo wa mtindo wa kitibet "uwanda wa juu wa Qinghai-Tibet" ukiimbwa. Sauti ya kuvutia ya mwimbaji wake Bi. Lin Wensun ilikuwa kama kweli inaonesha picha za ardhi ya ajabu ya Tibet.

Bi. Lim Wen Suen ni mwanafunzi kutoka Malaysia anayesomea muziki wa jadi wa kichina kwenye chuo cha muziki cha China. Kutokana na athari aliyoipata kutoka kwa baba yake, Bi. Lim Wen Suen alikuwa anavutiwa na kujifunza muziki wa jadi wa China toka akiwa mtoto. Baada ya kuja China amekuwa na ufahamu kamili na wa kina zaidi kuhusu muziki wa jadi wa kichina. Bi. Lim Wen Suen alisema:

"nyimbo za jadi za kichina ni tofauti na zile za nchi za magharibi, zinafuata mbinu ya noti 5 za muziki, na njia ya kuziimba pia ni tofauti. Nyimbo za jadi za kichina kama zile zilizoimbwa na mwimbaji Song Zuying zote ni za mtindo dhahiri wa kichina, ziliimbwa kwa sauti nyembamba na zinavutia sana."

Mashindano ya kuimba ya kombe la Laihua kwa wanafunzi wa nchi za nje wanaosoma kwenye vyuo vikuu mjini Beijing, yalianza kufanyika toka mwezi Oktoba mwaka 2007, na yaliwashirikisha wanafunzi wapatao 200 kutoka nchi 35 zikiwemo Korea ya Kusini, Russia, Malaysia, Marekani na Malaysia.

   

Baada ya mashindano ya ngazi mbalimbali, hatimaye wagombea 16 waliingia kwenye fainali. Mashindano ya fainali yalifanyika hivi karibuni katika jumba la muziki la chuo kikuu cha makabila cha China. Wagombea hao waliimba nyimbo za aina mbalimbali, mbali na nyimbo za jadi, wengi wao pia walichagua nyimbo maarufu za Pop nchini China.

Mwanafunzi kutoka Korea ya Kusini anayesoma katika chuo kikuu cha ualimu cha Beijing Bw. Noh Seung Woo alishangiliwa sana alipokuwa anaimba wimbo maarufu sana nchini China "I believe". Bw. Noh Seung Woo alisema, utamaduni wa China ndio uliomvutia kuja China na kujifunza lugha ya Kichina na utamaduni wake. Ingawa alikaa nchini China kwa muda wa miezi mitatu tu, ameanza kupenda mazingira ya masomo na maisha nchini China. Kushiriki kwenye mashindano hayo kumetokana na yeye kujifunza kichina, na kuimba kunasaidia kuinua uwezo wake wa kuongea lugha ya kichina. Bw. Noh Seung Woo alisema:

"kushiriki kwenye mashindano kama hayo kunanisaidia kujifunza kichina na kufahamu utamaduni wa China. Mbali na wimbo huo, pia ninakumbuka maneno ya nyimbo nyingi nyingine za kichina."

Ofisa wa shirikisho la elimu ya juu la Beijing ambalo ni moja ya waandaaji wa mashindano hayo Bw. He Xiangmin alisema, wanafunzi wengi wa nchi za nje wanaosoma nchini China si kama tu wanasoma lugha ya kichina na masomo mengine ya sayansi, zaidi ni kuwa wanavutiwa na kuwa na hamu ya kufahamu utamaduni wa China. Wanafunzi hao ni wachangamfu vyuo kwao, wanavutiwa sana na utamaduni wa China, na nyimbo pia ni moja ya sehemu inayobeba utamaduni huo. Mashindano ya kuimba si kama tu yanaburudisha masomo na maisha ya wanafunzi hao, kuimarisha mawasiliano na maelewano kati yao, bali pia yanasaidia kuhamasisha zaidi hamu yao ya kufahamu utamaduni wa China, hata upendo mkubwa kwa China unaweza kuonekana kutoka kwenye nyimbo zilizoimbwa nao.

Mwendeshaji wa mashindano hayo Bw. Francis Tchiegue kutoka Cameroon alisema, sababu ya yeye kuja China kutoka mbali inatokana na kupenda utamaduni wa China na historia yake ndefu. Bw. Francis Tchiegue alisema:

"nadhani utamaduni wa China ni wa kina sana, tulipokuwa nje ya China tulikuwa tunaona kwamba China ni sawasawa na nchi nyingine duniani, hakuna tofauti kubwa. Lakini baada ya kuja China, nimegundua kuwa nchi hiyo ni ulimwengu mwingine mwenye utamaduni mkubwa sana. Katika muda wa miaka minne nilipokuwa nasoma hapa nchini China, nimejifunza mambo mengi hasa kuhusu mambo ya maisha. Ninapendekeza watu wa nchi za nje waje na kukaa kwa muda nchini China, nchi hii kweli ni ya ajabu sana!"

   

Mashindano hayo yalikuwa yafanyika katika hali ya furaha, kuimba kwa dhati kwa wagombea pamoja na majibu ya walimu watazamaji, viliendelea kuleta furaha zaidi kwenye mashindano hayo. Hatimaye wanafunzi wanne walipewa tuzo ya ngazi ya kwanza.

Ofisa wa shirikisho la elimu ya juu la mji wa Beijing Bw. He Xiangmin alisema, ili kuburudisha masomo na maisha ya wanafunzi zaidi ya elfu 60 kutoka nchi za nje wanaosoma mjini Beijing, shirikisho hilo litaandaa mashindano mbalimbali ya kombe la Laihua kila mwaka. Kwa mwaka huu ni mashindano ya kuimba, zamani yaliwahi kufanyika mashindano kuhusu kucheza muziki, michezo ya meza na shughuli nyingine. Mashindano hayo yataendelea katika siku za baadaye ili kuimarisha maelewano na kuhamasisha nia ya wanafunzi hao kujifunza utamaduni wa China.