Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-02-13 19:55:57    
Mapishi ya kupika kamba

cri

Mahitaji: Kamba gramu 500, mvinyo wa kupikia gramu 25, siki gramu 10, chumvi gramu 5, sukari gramu 30, mafuta ya ufute gramu 25, mafuta gramu 100, vitunguu saumu, vitunguu maji na tangawizi kila gramu 10.

Njia:

1. osha kamba, na kupasua mgongo wake na kuondoa mstari wa mchanga kwenye mgongo.

2. tia mafuta ndani ya sufuria pasha moto mpaka yawe nyuzi ya asilimia 50, tia kamba kwenye sufuria na kuikaanga mpaka iwe rangi ya hudhurungi, tia vipande vya vitunguu maji, vitunguu saumu na tangawizi, mvinyo wa kupikia, chumvi, sukari na siki na mimina maji kidogo, chemsha kwa dakika 5, mimina mafuta ya ufute, uichukue kamba kwenye sahani, endelea kuchemsha mabaki ndani ya sufuria na yaweke kwenye kamba.