Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-02-13 19:56:36    
Mapishi ya vipande vya nyama ya nguruwe

cri

Mahitaji Nyama ya nguruwe gramu 200, mayai manne, M.S.G gramu 2, mvinyo wa kupikia gramu 30, wanga gramu 30, chumvi gramu 5, mafuta ya ufuta gramu 100, chumvi iliyochanganywa na pilipili kima, mafuta gramu 500.

Njia

1. Osha nyama ya nguruwe, ikate iwe vipande vyenye urefu wa sm 4 na upana wa sm 2, iweke kwenye bakuli, tia chumvi, M.S.G na mvinyo wa kupikia kisha korogakoroga.

2. Koroga mayai, tia wanga korogakoroga. Weka vipande vya nguruwe kwenye mayai yaliyokorogwa.

3. Tia mafuta kwenye sufuria ,pasha moto mpaka yawe na joto asilimia 60, tia vipande vya nguruwe kimoja baada ya kingine, vikaange mpaka viwe rangi ya hudhurungi, vipakue kwenye sahani, mimina mafuta ya ufuta, wakati utakapokula unaweza kuchovya vipande kwa chumvi iliyochanganywa kwa pilipili kima.