Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-02-18 15:23:21    
Kosovo yajitangazia uhuru kwa upande mmoja

cri

Bunge la Kosovo tarehe 17 lilifanya mkutano maalumu na kupitisha taarifa ya kujitangazia uhuru, kwa upande mmoja imejitangazia uhuru na kujitenga na Serbia. Taarifa inasema, Kosovo itatekeleza mpango wa mjumbe maalumu wa zamani wa Umoja wa Mataifa Bw. Marti Ahtisari kuhusu "uhuru wa Kosovo chini ya usimamizi wa kimataifa", na kukubali Umoja wa Ulaya kutuma kundi maalum kuingia Kosovo na kutaka jeshi la kulinda amani la Umoja wa Mataifa liendelee kuwepo ndani ya Kosovo. Taarifa pia inasema Kosovo iliyo huru itajishughulisha amani na utulivu wa kanda yake, na kuhakikisha kuwa inakuwa na uhusiano mzuri na nchi jirani.

Baada ya taarifa hiyo kutangazwa, katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Ban Ki-moon katika siku hiyo mara alitoa taarifa baada ya mkutano wa faragha, akizitaka pande zote ziheshimu ahadi bila kuchukua hatua yoyote inazohatarisha amani na utulivu wa kikanda. Taarifa imesisitiza kuwa kabla ya kupata agizo la Umoja wa Mataifa, kundi maalumu la Umoja wa Mataifa litaendelea kutekeleza azimio No. 1244 la Umoja wa Mataifa.

Rais wa Serbia Boris Tadic alisema, Serbia kamwe haitatambua uhuru wa Kosovo, na Serbia itabatili hatua hiyo ya Kosovo kwa njia zote za amani, kidemokrasia na za haki. Naibu wa kwanza wa katibu Rais wa Russia Bw. Dmitry Peskov alisema, hatua ya Kosovo kujitangazia uhuru ni haramu, Russia inapinga kabisa uhuru wa Kosovo. Taarifa ya wizara ya mambo ya nje ya Russia inataka Umoja wa Mataifa ufanye mkutano maalumu kujadili hali ya Kosovo. Waziri wa mambo ya nje wa Romania alisisitiza kuwa Romania inapinga hatua ya Kosovo kujitangazia uhuru kwa upande mmoja.

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Liu Jianchao tarehe 18 alisema, utatuzi wa suala la Kosovo unahusiana na amani na utulivu wa sehemu ya Balkan, kanuni za uhusiano wa kimataifa na heshima ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. China siku zote inaona kuwa njia nzuri ya kutatua suala la Kosovo ni kufanya mazungumzo na kufikia mpango unaokubaliwa na pande mbili za Serbia na Kosovo.

Uhuru wa Kosovo unaungwa mkono na Marekani na nchi nyingine za Magharibi. Baada ya Kosovo kujitangazia uhuru, baraza la serikali la Marekani lilitangaza kuzitaka pande zote mbili zijizuie na kukwepa kutokea vitendo vyovyote vya uchokozi. Rais wa Marekani Bw. George W. Bush alisema, Marekani itaendelea kushirikiana na nchi washirika wake ili kuhakikisha vitendo vya mabavu visitokee. Mjumbe wa Umoja wa Ulaya anayeshughulikia sera za kidiplomasia na mambo ya uslama Bw. Solana Madariaga alizitaka pande zote mbili zitulie.

Wachambuzi wanaona kuwa kujitangazia uhuru kwa upande mmoja kwa Kosovo, kutakumbana na matatizo mengi yanayohusu kutambuliwa kimataifa na kutatua masuala mengi ya kijamii na ya kiuchumi.

Kutokana na hali ilivyo hivi sasa, nchi nyingi hazijatoa taarifa yoyote ya kutambua uhuru wa Kosovo isipokuwa tu nchi chache za Magharibi, na nchi nyingi za Ulaya zina wasiwasi kuwa uhuru wa Kosovo utasababisha hali mbaya katika sehemu ya Ulaya.

Hivi sasa miundo mbinu yote iliyopo sasa ilijengwa na Yugoslavia ya zamani, vita karibu miaka kumi vimeharibu miundo hiyo, na maji na umeme unatoka kwa Serbia. Zaidi ya hayo suala la kijamii pia ni kubwa kwa Kosovo, hivi sasa Kosovo ni kama kituo kikubwa cha kuhamisha bidha za magendo duniani, uchumi wake unategemea misaada ya kimataifa tu. Karibu nusu ya wakazi hawana kazi, na 80% ya vijana wanashindwa kupata ajira, na kati yao wengi wanafanya biashara za magendo, dawa za kulevya na kuibia watu. Kutokana na hali hiyo Kosovo inakabiliwa na matatizo mengi ya kiuchumi.

Idhaa ya kiswahili 2008-02-18