Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-02-19 14:44:04    
Barua 0210

cri

Msikilizaji wetu Mbarak Mohammed Abucheri wa sanduku la posta 792 Kakamega, Kenya ametuletea barua akieleza maoni yake kuhusu Mkutano wa 17 wa Chama cha Kikomunisti cha China uliofanyika mwezi Oktoba mwaka jana, akisema anawapongeza wajumbe wa Chama cha Kikomunisti cha China waliohudhuria mkutano wa 17 kujadili pamoja mambo ya nchi. Tangu kuanzishwa kwa Chama cha Kikomunisti cha China na kushika hatamu za uongozi kuitawala nchi ya China, Wachina wamechuma maua adimu katika bustani ya maisha na kupata matumaini na matarajio moja baada ya mengine. Taa ya matumaini ndiyo imewangazia na kubadilisha maisha yao machungu kuwa matamu.

Alisema katika kikao hicho, wajumbe walijadili na kuidhinisha "Taarifa ya kazi za Serikali" kukagua na kuidhinisha mpango wa kuhimiza mageuzi ya Chama cha Kikomunisti cha China, na kuweka utaratibu wa kisheria. Anakumbuka kuwa mambo muhimu yaliyozingatiwa katika mkutano huo, kwanza ni kuunganisha watu wa makabila mbalimbali ya watu wa China na ufunguaji mlango kwa watu wa nje bila kuwabagua kwa misingi ya kikabila, rangi au dini. Kwa mwaka huo, Chama cha Kikomunisti cha China pia kilitoa mchango mkubwa kuhusu muungano na mashauriano baina ya watu, nchi na mataifa mbalimbali na kujenga serikali adilifu na safi. Katika mwongozo wake Chama cha Kikomunisti kinatilia maanani utawala bora na kupambana na rushwa na kuzingatia demokrasia.

Na katika kuimarisha uwiano wa uchumi wa masoko wa kijamaa, serikali ya China chini ya Chama cha Kikomunisti ina mipango halisi katika kufanya kazi vizuri na kuendelea kufanya mageuzi ya teknolojia, kushughulikia viwanda na kuendeleza nguvu kazi za kuhudumia maisha na uzalishaji mali, kupanua njia za kuajiri wafanyakazi, kuweka utaratibu wa bima kwa watu wasio na ajira, kugeuza dhana kongwe kuhusu kazi za sulubu na kuajiriwa, na kuinua uwezo wa kukinga hatari ya kutokuwa na ajira. Mara kwa mara wachina wamekuwa wakihimizwa kutekeleza maendeleo endelevu katika mambo ya kisayansi na uhifadhi mazingira, kufuatia mfumo bora wa kisiasa na demokrasia uliowekwa na Chama cha Kikomunisti. Ni kupitia uongozi bora na mtizamo safi, taifa la China limepata maendeleo makubwa na kuwavutia mataifa ya ulimwengu. Kwa sasa China inaongoza kwa hali ya kuimarika kiuchumi na teknolojia, kibiashara, kwani bidhaa zake zina soko kubwa kote duniani. Anasema vilevile taifa la China limepata ufanisi kwa kuwa taifa lenye wataalamu wa ujenzi barabara na miundo misingi mengine kama vile hospitali, viwanja vya michezo. Ufanisi umeyafanya mataifa ya magharibi kufungua macho baada ya kuona China imekuwa na upeo wa juu kiuchumi na maendeleo ya kibiashara. Pia ni kutokana na China kuona umuhimu wa kuanzisha ushirikiano na mataifa ya bara Afrika.

Idhaa ya kiswahili 2008-02-19