Mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya ulifanyika tarehe 18 mjini Brussels kujadili msimamo wa pamoja kuhusu suala la Kosovo baada ya kujitangazia uhuru. Lakini kutokana na tofauti ambazo ni vigumu kuzisawazisha, mwishowe mkutano huo ulipaswa kukubali kila nchi mwanachama ifanye uamuzi wake yenyewe kuhusu kutambua uhuru wa Kosovo. Juhudi za Umoja huo unaotetea "kusema kwa kauli moja" kwa mara nyingine tena zimezama katika hali ya shida.
Azimio lililopitishwa kwenye mkutano huo linasema, Umoja wa Ulaya siku zote unaheshimu katiba ya Umoja wa Mataifa na maazimio yote ya Baraza la Usalama yanayotetea kulinda mamlaka ya nchi na ukamilifu wa ardhi, pamoja na kuzingatia migogoro iliyotokea katika miaka ya 90 na hali ya sasa ya kuwa chini ya himaya ya kimataifa, Umoja wa Ulaya unaona kuwa suala la uhuru wa Kosovo ni "tukio lisilo la kawaida" ambalo halijaenda kinyume na katiba na maazimio hayo, kwa hiyo Umoja huo utakubali uhusiano na Kosovo unaoamuliwa na kila mwananchi kwa mujibu wa mazoea yake na kanuni zake za kimataifa.
Baada ya azimio hilo kupitishwa, waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa Bw. Bernard Kouchner alitangulia kutangaza kuwa Ufaransa inatambua uhuru wa Kosovo na kusema, "hakuna njia nyingine zaidi ya uhuru katika utatuzi wa suala la Kosovo", na "uhuru wa Kosovo ni mwisho wa vurugu za Balkan". Waliofuata kuutambua uhuru wa Kosovo ni mawaziri wa mambo ya nje wa Uingereza, Ujerumani na Italia. Waziri mambo ya nje wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier alisema, baada ya jumuyia ya kimataifa kushindwa kusuluhisha mwaka uliopita, tukio la uhuru wa Kosovo haliwezi kuepukika. Pamoja na hayo nchi za Ubelgiji, Uswisi, Czech, Denmark, Finland, Poland na Ireland pia zimeonesha kuwa zitatambua uhuru wa Kosovo kwa njia ya kidiplomasia.
Lakini nchi za Hispania, Slovakia, Cyprus, Ugiriki, Romania na Bulgaria ambazo zina migogoro ya kujitawala kikabila zinapinga kuutambua uhuru wa Kosovo, kati ya nchi hizo hasa ni Hispania ambayo inasumbuliwa zaidi na tatizo la kutaka kujitawala kwa kabila la Basque. Waziri wa mambo ya nje wa Hispania Bw. Miguel Angel Moratinos, tarehe 18 kwenye mkutano huo alisisitiza kuwa serikali ya Hispania kamwe haitatambua uhuru wa Kosovo kwa sababu kitendo hicho hakilingani na sheria za kimataifa.
Misimamo tofauti ya nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya kuhusu uhuru wa Kosovo inatokana na hali ilivyo ya kila nchi mwanachama. Mwezi Juni mwaka 1999 Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilipitisha azimio likisisitiza Shirikisho la Yugoslavia lina mamlaka ya utawala kwa sehemu ya Kosovo na kutuma kundi la Umoja wa Mataifa kusimamia sehemu hiyo. Lakini kabila la Albania ambalo linachukua 90% ya watu wa Kosovo linataka kujitawala. Mwezi Machi mwaka uliopita, ushauri uliotolewa na mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Kosovo kujipatia uhuru chini ya usimamizi wa kimataifa haukupitishwa katika mkutano wa Baraza la Usalama kutokana na kupingwa na Russia. Kisha Umoja wa Mataifa uliidhinisha Umoja wa Ulaya, Marekani na Russia zisimamie kwa pamoja mazungumzo kati ya Serbia na Kosovo, lakini kutokana na tofauti kubwa ya misimamo kati ya pande mbili, mazungumzo yalivunjika mwezi Novemba mwaka jana. Tokea hapo Marekani ikaanza kuchochea Kosovo kujipatia uhuru na nchi muhimu kati ya nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya, Uingereza, Ufaransa na Ujerumani zinasogeza misimamo yao karibu na Marekani.
Nchi zinazopinga uhuru wa Kosovo zinafahamu fika hatari ya "pipa la baruti" hilo la Ulaya. Tarehe 18 rais wa Romania alivitaka vyama vyote vya kisiasa nchini humo viwe na uvumilivu na visitoe maneno makali kuhusu Kosovo kujitangazia uhuru kwa upande mmoja, ili kukwepa kuzusha matatizo ya kikabila nchini humo.
Cha kutia maanani ni kuwa bila kujali kupingwa na Serbia na Russia, tarehe 16 Umoja wa Ulaya uliamua kutuma kundi lake kwenda Kosovo kwa lengo la kuchukua nafasi ya kundi la Umoja wa Mataifa kusaidia kurejesha utulivu. Kwa hiyo ni wazi kwamba Umoja wa Ulaya ushaitambuua Kosovo kuwa ni nchi yenye mamlaka na kuanza kutimiza kuigeuza Kosovo kwa mpango wake.
|