Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-02-20 16:23:59    
Mapishi ya vipande vya vitu vitatu

cri

Mahitaji:

Nyama iliyosagwa gramu 100, mboga gramu 50, pilipili hoho moja, pilipili mboga moja, mafuta ya ufuta vijiko viwili, mvinyo wa kupikia kijiko kimoja, mchuzi wa sosi kijiko kimoja, chembechembe za kukoleza ladha kijiko kimoja, chumvi kijiko kimoja

Njia:

1. kata mboga iwe vipande, kata pilipili hoho na pilipili mboga ziwe vipande.

2. washa moto, mimina mafuta kwenye sufuria halafu tia nyama iliyosagwa, korogakoroga mpaka ikauke, tia mvinyo wa kupikia na mchuzi wa sosi korogakoroga, tia vipande vya mboga, vipande vya pilipili mboga na pilipili hoho korogakoroga, tia chembechembe za kukoleza ladha, chumvi na mafuta ya ufuta korogakoroga. Ipakue mpaka hapo kitoweo hiki kiko tayari kuliwa.