Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-02-22 17:36:16    
Makampuni ya China yashiriki kwenye ujenzi wa uchumi wa Nigeria

cri

Katika miaka ya hivi karibuni, makampuni ya China iliyamekuwa yanashiriki kwenye ujenzi wa uchumi wa Nigeria, miradi ya ujenzi iliyojengwa na makampuni ya China inaendelea vizuri na kutoa mchango mkubwa kwa maendeleo ya uchumi na jamii ya Nigeria.

Mwezi Mei mwaka jana, satellite nambari moja ya mawasiliano ya habari ya Nigeria iliyotengenezwa na China ilikurushwa kwa mafanikio, kabla ya hapo kampuni ya miradi ya ujenzi ya China nchini Nigeria iliruhusiwa kujenga kituo cha udhibiti wa satellite ya mawasiliano ya habari ardhini huko Abuja na ilimaliza ujenzi wa mradi huo mwezi Aprili mwaka jana. Kituo hicho kilitoa uhakikisho wa kiufundi kwa urukaji wa satellite hiyo baada ya kurushwa.

Kampuni hiyo pia iliruhusiwa kujenga mradi wa subway ya Abuja, yenye urefu wa subway hiyo ni kilomita 60.7 ambayo ni subway ya kwanza nchini Niegira, na muda wa mradi huo ni miaka mine. Usanifu na ujenzi wa mradi huo utafanywa na kampuni hiyo na kigezo cha tekenolojia kitakachotumiwa ni kigezo taifa cha China.

Mjini Lagos, kampuni ya ujenzi wa China nchini Nigeria inafanya mradi wa ukarabati wa daraja la Lagos. Naibu meneja mkuu wa kampuni hiyo Bw. Shi Hongbing alieleza kuwa, mradi huo utabadilisha njia mbili za barabara ya magari kuwa njia nne, daraja hilo lina urefu wa mita 600 na barabara yake ina urefu wa kilomita 18, mradi huo unatarajia kukamilika mwezi Mei mwaka 2008 ambao utasaidia ujenzi wa kituo kipya cha sayansi na tekenolojia cha Lagos.

Aidha kampuni ya CGCOC nchini Nigeria hivi sasa inashughulikia ujenzi wa miradi ya uwanja wa ndege, kingo za mito na barabara. Meneja wa kampuni hiyo Bw. Li Xuhui alipozungumzia juhudi zinazofanywa na makampuni ya China kushiriki kwenye ujenzi wa miundo mbinu wa Nigeria, alisema " Tufanya ujenzi wa miundo mbinu nchini Nigeria tumeleta manufaa kwa wananchi wa huko na kupata uaminifu wao pia tumepata ufanisi na kusifiwa vizuri na upande wa Nigeria."

Nigeria ina upungufu wa umeme lakini ina maliasili mengi ya gesi, mafuta na maji, makampuni ya China yanashiriki kwneye ujenzi wa mradi wa kituo cha kuzalisha umeme kwa nishati ya maji, na kutoa uhakikisho wa nishati kwa maendeleo ya uchumi ya Nigeria. Kwa mfano wa kituo cha kuzalisha umeme kwa gesi cha Omotoso kilichojengwa na kampuni ya uagizaji na uuzaji wa mashine ya China, ujenzi wa kituo hicho ulianza mwezi Machi mwaka 2005, vikundi vinane vya mashine tayari vimefanyiwa majaribio, na mashine hizo zimeanza kuzalisha umeme. Aidha kampuni ya Ge Zhouba ya China na kampuni ya CGCOC nchini Nigeria, zimepata ruhusa kujenga mradi wa kuzalisha umeme kwa maji wa Mombala nchini Nigeria uliowekewa dola za kimarekani bilioni 1.46, mradi huo ni mkubwa kabisa unaojengwa na kampuni ya China barani Afrika na umesifiwa kuwa mradi huo ni kama mradi wa magenge matatu ya China nchini Nigeria.

Kampuni za China zinajitahidi kushiriki kwenye miradi mingi ya ujenzi wa kiuchumi wa Nigeria, kutokana na kupanuka kwa ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na Nigeria. Kutokana na juhudi za pamoja za pande hizo mbili, ushirikiano kati ya nchi hizo mbili utaendelea kupanuka.

Habari nyingine zinasema, waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Yang Jiechi mwanzoni mwa mwaka huu alikwenda Bujumbura, mji mkuu wa Burundi kushiriki sherehe ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa shule ya urafiki kati ya Burundi na China. Makamu wa rais wa Burundi Bw. Sahinguvu, waziri wa mambo ya nje wa Burundi Bi. Antoinette Batumubwira na naibu waziri wa elimu ya msingi na elimu ya sekondari Bw. Ernest Mberamiheto na balozi wa China nchini Burundi Bw. Zeng Xianqi walihudhuria sherehe hiyo.

Shule hiyo ni moja ya shule tatu zitakazojengwa kwa msaada wa China kwa Burundi, kutokana na ahadi zilizotolewa na China katika mkutano wa wakuu wa baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika uliofanyika hapa Beijing. Kila shule itakuwa na eneo la meta za mraba 5,500 na madarasa 6, na kila darasa linaweza kuwa na wanafunzi 50.

Shule nyingine mbili zitajengwa mkoani Karuki, katikati mwa Burundi, hivi sasa kazi ya kuchagua sehemu za kujenga shule hizo imekamilika, na ujenzi unatarajiwa kuanza mwezi Machi mwaka huu na utafanywa na kampuni ya ujenzi ya Hainan ya China.

Naibu waziri wa elimu ya msingi na elimu ya sekondari Bw. Mberamiheto alisema, China ilitoa misaada ya pande zote kwa Burundi hasa katika mambo ya elimu na afya.

Burundi iliwahi kukumbwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kwa miaka 12. Mwaka 2005, Burundi ilifanya uchaguzi mkuu na kuanzisha serikali mpya, serikali ya Burundi na kundi la upinzazni zilisaini makubaliano ya kusimamisha vita kwa pande zote hivyo hali ya Burundi ilitulia. Lakini baada ya vita, wakimbizi wengi walirudi nyumbani makwao, kulikuwa na tatizo kubwa kwa watoto kwenda shule. Shule nyingi za Burundi ziliharibiwa katika vita na kulikuwa na upungufu wa waalimu. Burundi inahitaji kukarabati, serikali ya Burundi inafahamu umuhimu wa elimu katika maendeleo ya nchi hiyo. Baada ya kuapishwa kuwa rais wa Burundi, Rais Pierre Nkurunziza mwezi Agosti mwaka 2005 alitangaza serikali kuanza kutekeleza utaratibu wa elimu ya lazima ya miaka 6 katika shule nchini Burundi.

China inaelewa hisia za kutarajia kukarabati nchi walizo nazo wananchi wa Burundi, hivyo ilitoa misaada mingi kwa Burundi katika mambo ya elimu. Majengo mapya ya chuo kikuu cha ualimu cha Burundi yalijengwa huko Bujumbura kwa msaada wa China. Mradi huo ulianza mwezi Julai mwaka 2005 na umepangwa kumalizika kabla ya mwezi Juni mwaka huu. Rais Nkurunziza alipotembelea mradi huo alisifu sana usanifu na sifa ya ujenzi wa mradi huo.

Urafiki kati ya China na Burundi ni wa jadi, uhusiano kati ya nchi hizo mbili uliendelezwa vizuri, na mkutano wa wakuu wa Baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika umetia nguvu mpya ya uhai kwa ushirikiano kati ya nchi hizo mbili.

Idhaa ya kiswahili 2008-02-22