Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-02-26 17:17:51    
Kushindwa kwawasaidia wachezaji wa kuteleza barafu wa China kupata maendeleo mapya

cri
Michezo ya 11 ya majira ya baridi ya China ilimalizika hivi karibuni katika miji ya Qiqiha'er na Harbin nchini China. Kwenye mashindano ya kuteleza kwenye barafu kwa mitindo mbalimbali, mabingwa wa mchezo wa kuteleza kwenye barafu kwa wachezaji wawili wawili duniani Pang Qing na Tong Jian walipata medali ya dhahabu na fedha katika michezo ya Short Program na kuteleza kwenye barafu kisanii. Mafanikio hayo yana umuhimu mkubwa kwa wachezaji hao wawili, kwani yalipatikana kutokana na juhudi kubwa.

Kwenye Mashindano ya ubingwa ya kuteleza kwenye barafu kwa mitindo mbalimbali duniani ya mwaka 2006, Pang Qing na Tong Jian waliwashinda wachezaji wenzao wawili Zhang Dan na Zhang Hao ambao walipata medali ya fedha kwenye Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya mwaka 2006, na kupata medali yao ya kwanza ya dhahabu, pia wamekuwa mabingwa wengine wa mchezo huo baada ya kupata ubingwa kwa wachezaji hodari wa China Shen Xue na Zhao Hongbo. Kwa maoni ya watu wengine, ni jambo la kawaida kwa mabingwa wa Mashindano ya ubingwa duniani kupata medali ya dhahabu kwenye Michezo ya Majira ya Baridi ya China. Lakini kwa wachezaji Pang Qing na Tong Jian, mafanikio hayo yalipatikana kutokana na juhudi kubwa.

Baada ya kupata ubingwa kwenye mashindano ya ubingwa duniani, mungu haukuendelea kuwabariki Pang Qing na Tong Jian, na matukio ya dharura yalikwamisha maendeleo ya wachezaji hao wawili, na kuwafanya wawe kwenye chini ya kiwango chao cha uchezaji. Mwezi Septemba mwaka 2006, Pang Qing alitibiwa uvimbe kwenye figo, na mwishoni mwa mwaka 2006, Pang Qing na Tong Jian walikumbwa na ajali ya gari mjini Beijing, na Tong Jian alishonwa nyuzi kumi kadhaa kichwani kutokana na ajali hiyo na bado kovu refu limebaki kwenye paji la uso wake. Matukio hayo ya dharura yalileta athari kubwa kwa mipango ya mazoezi na mashindano ya wachezaji hao wawili. Kwenye Michezo ya majira ya baridi ya wanafunzi duniani na Michezo ya majira ya baridi ya Asia, Pang Qing na Tong Jian hawakupata mafanikio makubwa, na walifanya makosa kwenye mashindano ya kituo cha Changchun nchini China kwenye Michezo ya kuteleza kwenye barafu kwa mitindo mbalimbali yaliyofanyika mwishoni mwa mwaka 2007, kushindwa kwenye michezo hiyo kulimfanya Pang Qing asikitike na kutokwa machozi baada ya michezo hiyo kumalizika.

Lakini kwenye Michezo ya majira ya baridi ya China iliyofanyika mwaka huu, wachezaji hao wawili walionesha sura yao mpya. Kwenye mchezo wa Short Program kwenye mashindano ya kuteleza kwenye barafu kwa wachezaji wawili wawili, Pang Qing na Tong Jian walimaliza vitendo vyote kwa ustadi mkubwa, na kupata medali ya dhahabu kwenye mchezo huo bila ya mashaka yoyote. Mafanikio hayo yana umuhimu mkubwa kwa wachezaji hao wawili waliofanya juhudi kubwa. Tong Jian alisema:

"Nafurahi kuwa tumeshinda matatizo na kurudi kwenye hali nzuri."

Baada ya kukumbwa na matukio mbalimbali ya dharura, Pang Qing na Tong Jian wanakabiliwa na matatizo mbalimbali yaliyowakumba kwa moyo wa kawaida. Wakizungumzia siku zile zilizowasikitisha watu, Pang Qing na Tong Jian hawakulalamika hata kidogo. Kwa maoni ya wachezaji hao wawili, wanashukuru uzoefu huo uliowahimiza kupata maendeleo mapya bila ya kusita.

"Naona kuwa huu kama ni ukuaji wetu wa mara nyingine, kwani tunaweza kupata maendeleo mapya baada ya kushinda matatizo mbalimbali, hali ambayo imetusaidia sana."

Watu wanaokuwa na mafanikio makubwa kwenye mambo fulani duniani, huwa na sifa ya pekee na hukumbwa na vikwazo vingi. Baada ya kustaafu kwa Shen Xue na Zhao Hongbo ambao ni wachezaji hodari wa China wa mchezo wa kuteleza kwenye barafu kwa mitindo mbalimbali, Pang Qing na Tong Jian wamepewa jukumu kubwa, wanapaswa kufanya juhudi kwa pamoja na wachezaji wenzao wawili Zhang Dan na Zhang Hao, wala si kuweka lengo la kugombea medali za dhahabu tu, bali ni kuupatia mchezo huo nchini China mafanikio makubwa, na kuwasaidia na kuwahimiza wachezaji chipukizi wapate maendeleo kwa haraka. Tong Jian alisema:

"Kutokana na umri na uzoefu wetu, tunapaswa kubeba jukumu kubwa. Tuna matumaini kuwa wachezaji vijana watapata maendeleo kwa haraka, na kutuhimiza tupate mafanikio makubwa zaidi na kuweka lengo la juu zaidi kwao, ili kuzihimiza timu za michezo mbalimbali ya kuteleza kwenye barafu nchini China zifikie kiwango cha juu duniani."

Pang Qing na Tong Jian waliopata ubingwa wa dunia, bado hawakupata medali kwenye Michezo ya Olimpiki. Hadi sasa miaka miwili imebaki kabla ya kufunguliwa kwa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya mwaka 2010, wachezaji hao wawili wameanza kufanya maandalizi kwa ajili ya michezo hiyo. Wakizungumzia kuhusu lengo la michezo hiyo, Pang Qing na Tong Jian ana imani kubwa. Pang Qing alisema:

"Lengo kwangu ni kupata medali ya dhahabu!"

Ingawa Pang Qing na Tong Jian walikumbwa na matukio ya dharura na matatizo mbalimbali, lakini hawakuacha imani yao ya kupata mafanikio. Wachezaji hao wawili wametoa ahadi yao kwa kutumia mafanikio yao yaliyopatikana kwenye Michezo ya Majira ya Baridi ya China, na wataendelea kupiga hatua kuelekea kunyakua medali za dhahabu kwenye Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi.

Idhaa ya kiswahili 2008-02-26