Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-02-27 19:49:07    
Mapishi ya uyoga mweupe na nyama ya nguruwe

cri

Mahitaji

Uyoga mweupe gramu 300, vipande vya vitunguu maji gramu 2, tangawizi gramu 2, sukari gramu 10, mchuzi wa sosi vijiko viwili, mvinyo wa kupikia vijiko viwili, chembechembe za kukoleza ladha kijiko kimoja

Njia

1. osha nyama ya nguruwe, halafu uikate iwe vipande vipande.

2. ondoa mizizi ya uyoga mweusi halafu ukate iwe vipande.

3. washa moto halafu mimina mafuta kwenye sufuria, tia vipande vya tangawizi, na vitunguu maji korogakoroga, halafu tia vipande vya nyama ya nguruwe, korogakoroga, punguza moto endelea kukoroga, vipakue.

4. washa moto tena, mimina mafuta kidogo, halafu tia sukari korogakoroga halafu tia vipande vya nyama ya nguruwe, korogakoroga, mimina mvinyo wa kupikia, mchuzi wa sosi korogakoroga, mimina maji mpaka yachemke, punguza moto endelea kuchemsha kwa dakika 40, halafu tia vipande vya uyoga mweupe endelea kuchemsha kwa dakika 10, ipakue. Mpaka hapo kitoweo hiki kiko tayari kuliwa.