Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-02-28 16:06:34    
Umoja wa Mataifa waanzisha harakati za miaka 7 za kutokomeza vitendo vya kimabavu dhidi ya wanawake

cri

Umoja wa Mataifa tarehe 25 kwenye makao makuu yake mjini New York ulianzisha harakati za kupambana na vitendo vya kimabavu dhidi ya wanawake duniani. Harakati hizo zitadumu kwa miaka saba, ambapo idara husika na mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa, zitashiriki kwenye harakati hizo, na itakuwa harakati kubwa zaidi katika historia ya Umoja wa Mataifakwa ajili ya kulinda haki na maslahi halali ya wanawake.

Kwenye sherehe ya kuanzisha harakati hizo, katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Ban Ki-Moon na mke wake Bibi Yoo Soon-taek, waliongoza wajumbe waliohudhuria sherehe hiyo kupuliza vipenge vyao vya mikononi, na kuonesha kuanzishwa kwa harakati za kupambana na vitendo vya kimabavu dhidi ya wanawake.

Bw. Ban Ki-Moon kwenye hotuba yake alisisitiza kuwa, vitendo vya kimabavu dhidi ya wanawake havikubaliki, havisameheki na havivumiliki. Alisema, wanaume wanapawa kubeba wajibu wa kuzuia vitendo vya kimabavu dhidi ya wanawake.

Aliwataka wanaume wote duniani watoe taarifa wazi kwa kutumia fursa hii, kulaini vitendo vya kimabavu dhidi ya wanawake. Pia alisema wanaume wanapaswa kuchukua utoaji wa taarifa kama hiyo kuwa ni fahari kwao.

Katika maendeleo ya utamaduni wa binadamu, wanawake wameathiriwa vibaya na vitendo vya kimabavu kwa muda mrefu, na vingi ni kutoka kwa wanaume. Wakati huo huo, vitendo hivyo vya kimabavu siyo tu vinatoka kwenye familia zao, bali pia vinahusiana na sababu nyingi za utamaduni na jamii. ?

Ripoti moja ya Benki ya Dunia inaonesha kuwa, mmoja kati ya kila wanawake watatu alipigwa na mume wake au rafiki yake mwanaume, kulazimishwa kufanya ngono na kunyanyashwa kwa namna nyingine; na mmoja kati ya kila wanawake watano alikumbwa na ajali ya kubakwa au vitendo vya kujaribu kumbaka. Hatari za ubakaji na vitendo vya kimabavu za familia zilizowakabili wanawake wenye umri kati ya miaka 15 hadi miaka 44 duniani, ni kubwa kuliko hatari ya kutokana na vita, magonjwa na ajali. Katika migogoro iliyotokea kwenye sehemu mbalimbali duniani, wanawake mara kwa mara wanachukuliwa kama silaha za kulipiza kisasi na kuwadhalilisha. Katika mauaji ya Rwanda yaliyotokea mwaka 1994, wanawake wapatao zaidi ya laki kadhaa walibakwa. Wakati huo huo, kutokana na kuwepo kwa desturi mbaya katika sehemu kadhaa, wanawake wengi duniani walikumbwa na ukeketaji, na wanawake wengi waliuawa na jamaa zao kutokana na kufanya ngono kabla ya ndoa au kuwa na uhusiano nje ya ndoa.

Aidha, wanawake waliuawa katika uuzaji wa watu, mashambulizi ya jinsia, au kutokana na kukosa mahari ya kutosha, pamoja na kutoa mimba kutokana na udhalilishaji wa kijinsia, vyote hivyo ni vitendo halisi vya mabavu dhidi ya wanawake ambavyo vinatokea kila mara. Hata katika nchi zilizoendelea katika mambo ya utamaduni na uchumi, vitendo visivyo vya haki dhidi ya wanawake bado ni vingi. Takwimu zinaonesha kuwa, karibu nusu ya wanawake wa nchi za Umoja wa Ulaya, walikumbwa na mashambulizi ya kijinsia kazini.

Lengo la harakati hizo za Umoja wa Mataifa ni kuitangazia dunia nzima kuwa, jamii ya binadamu katika zana zenye ustaarabu kamwe haivumili vitendo hivyo. Mkurugenzi mtendaji wa mfuko wa idadi ya watu wa Umoja wa Mataifa Bw. Thoraya Obaid alisema, katika miaka mingi iliyopita jamii ya binadamu imekalia kimya vitendo hivyo vya kimabavu, leo tunaanzisha harakati hizo kuvunja ukimya, na kuzifanya sauti za wanawake zisikike katika dunia nzima.

Naibu katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia mambo ya uchumi na jamii Bw. Sha Zukang pia alisema, kama alivyosema Bw. Ban Ki-Moon, vitendo vya kimabavu dhidi ya wanawake ni kikwazo kikubwa katika kutimiza ajenda ya maendeleo ya Umoja wa Mataifa ikiwemo lengo la Milenia. Pia alisema, idara husika inayoongozwa naye itafanya juhudi kadiri iwezavyo ili kuunga mkono harakati hizo. Alisema kuanzia leo, harakati hizo zitafanywa pamoja na utimizaji wa lengo la Milenia, na ana matumaini kuwa hadi kufikia mwaka 2015 maendeleo ya jamii na uchumi na kazi ya kulinda haki na maslahi halali za wanawake vitapata mafanikio makubwa kote duniani.

Idhaa ya kiswahili 2008-02-28