Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-02-28 19:24:24    
Bw. Liu Guijin azungumzia ziara yake nchini Sudan

cri

Mjumbe maalum wa serikali ya China anayeshughulikia Suala la Darfur Bw. Liu Guijin, tarehe 27 huko Khartoum aliitisha mkutano na waandishi wa habari, akijibu maswali ya waandishi wa habari kuhusu ziara yake nchini Sudan. Bw. Liu Guijin alifanya ziara ya siku nne nchini Sudan kuanzia tarehe 24 hadi 27. Wakati wa ziara yake alikuwa na mazungumzo na viongozi wa Sudan na maofisa wahusika, pia alitembelea Nyala, mji mkuu wa mkoa wa Darfur kusini nchini Sudan. Alipozungumzia mafanikio ya ziara yake hiyo, Bw. Liu Guijin alisema:

"Nafurahia matokeo ya jumla ya ziara yangu. Sio kama serikali ya Sudan haitaki kutatua masuala, na ufuatiliaji wake kuhusu baadhi ya masuala una sababu zake, lakini ni lazima tutambue kwamba bado kuna migongano kati ya serikali ya Sudan na nje, na watu wa nje bado hawaelewi mambo mengi. Lakini serikali ya Sudan inapenda kuimarisha mawasiliano na mazungumzo na jumuiya ya Kimataifa, kwani maofisa wengi waandamizi wa Sudan wameniambia kuwa, kama utatuzi wa Suala la Darfur utakwama kwa muda mrefu, wananchi wa Sudan watakumbwa na balaa zaidi, na maendeleo ya nchi ya Sudan yataathiriwa vibaya zaidi".

Alipojibu Swali la mwandishi wa habari wa Misri kuhusu kuifanya Michezo ya Olimpiki ya Beijing ya mwaka 2008 kuwa Suala la kisiasa, Bw. Liu Guijin alisema:

"Michezo ya Olimpiki ya Beijing ya mwaka 2008 siyo Michezo ya Olimpiki ya China tu, ni Michezo ya awamu mpya ambayo China ikiwa ni mwenyeji wa michezo hiyo, itashirikisha nchi mbalimbali na wananchi wao. Kuhusisha masuala yanayotokea nchini Sudan ambayo iko mbali sana na China na Michezo ya Olimpiki ya Beijing, ni jambo ambalo ni vigumu kuwaelewesha watu. Nimedhihirisha mara kwa mara kuwa, moyo wa kimsingi wa Michezo ya Olimpiki ni michezo yake isiyo ya kisiasa, kuifanya Michezo ya Olimpiki iwe ya kisiasa, kutaleta madhara makubwa sana kwa siku za mbele, kwani kufanya hivyo ni kama kuwatia moyo baadhi ya watu au nguvu fulani maalum ya kisiasa kuhusisha wanavyopenda Michezo ya Olimpiki na mambo mengine yasiyohusiana hata kidogo na michezo hiyo".

Bw. Liu Guijin alisema, uhusiano kati ya China na Sudan ni uhusiano wa kawaida sana kati ya nchi na nchi, ambao hauna tofauti na ule kati ya China na nchi nyingine za Afrika. Bw. Liu alisema:

"Tunapinga kithabiti kufanya uhusiano kati ya China na Sudan uwe wa kisiasa, vyombo fulani vya habari na baadhi ya jumuiya zisizo za kiserikali zinalaani zaidi ushirikiano kati ya China na Sudan kwenye sekta ya mafuta, ushirikiano huo hauna kitu cha kushangaza, kwani nchi za magharibi zimefanya jambo hilo kwa zaidi ya miaka mia moja, China haipaswi kulaumiwa. Juzi nilitembelea kiwanda cha kusafisha mafuta cha Khartoum, nilishangaa sana, kiwanda hiki kimefanya kazi kwa miaka 10 , na kuiwezesha nchi ya Sudan iliyoagiza mafuta ya petroli kutoka nje kuwa nchi inayoshughulika na uchimbaji na uyeyushaji wa mafuta, na yenye kiwanda cha mafuta kilichozatitiwa kwa seti nzima ya teknolojia na vifaa, na kusukuma mbele maendeleo ya uchumi wa nchi hiyo, mfano kama huo sio mingi duniani. Hivyo nasema, ushirikiano kati ya China na Sudan hasa ushirikiano kati yao kwenye sekta ya mafuta ya petroli ni wa kunufaishana na uwazi, ambao haukatazi kushirikisha nchi nyingine, ndiyo maana haupaswi kulaumiwa hata kidogo".

Bw. Liu Guijin alisisitiza kuwa, China inapodumisha uhusiano wa kirafiki na ushirikiano kati ya Sudan, pia imeshiriki kwa juhudi kubwa katika utatuzi wa Suala la Sudan. Alisema:

China ikiwa moja kati ya wajumbe watano wa kudumu wa Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa, imeshiriki kwa juhudi kubwa katika utatuzi wa Suala la Sudan, China ikiwa ni mhusika anayehimiza juhudi za pande mbalimbali, juhudi zake zinatambuliwa na jumuiya ya Kimataifa pamoja na nchi kadhaa za magharibi. Na msimamo wa China kuhusu Suala la Sudan unaungwa mkono na kueleweka kwa nchi nyingi za Afrika na nchi nyingi zinazoendelea. Na malengo ya China na baadhi ya nchi kubwa za magharibi ni ya pamoja, lakini hatua halisi ni tofauti kidogo. Hivyo China inadumisha majadiliano na Baraza la usalama nchi nyingine za wajumbe wa kudumu wa Baraza hilo. Hii imeonesha kuwa China inajitahidi kutafuta njia ya mawasiliano, mashauriano na ushirikiano, badala ya mapambano na jumuiya ya Kimataifa pamoja na nchi kubwa za magharibi kuhusu Suala la Sudan".