Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-03-04 16:38:33    
Wafanyakazi wa Darfur kwenye Shamba la Khartoum

cri

Kwenye kitongoji cha Khartoum, mji mkuu wa Sudan, kuna shamba moja linaloendeshwa na Wachina, wafanyakazi wa shamba hilo wote wanatoka kutoka sehemu ya Darfur. Kwa kufanya kazi huko wanaweza kukidhi mahitaji ya familia zao na huku wanatoa mchango kuendeleza shamba hilo.

Shamba hilo ni kama kijiji kimoja nchini China, mbwa wanabweka na kuku wanalia, miti ni mingi na mboga ziko kila mahali. Anayeendesha shamba hilo ananitwa Fan Chuanzhao, ni Mchina anayetoka kutoka mkoa wa Shandong, China, anaonekana mwenye umri wa miaka zaidi ya 40 hivi. Alisema, alianzisha shamba hilo mwaka 2005.

"Shamba hilo lina eneo la hekta kumi hivi, tunalima mboga za aina nyingi za Kichina."

Mboga za shamba hilo zinalimwa kwa ajili ya makampuni ya China na masoko huko Khartoum. Kwenye mji wa Khartoum kuna mashamba mengi kama hilo, tofauti na mashamba mengine ni kwamba shamba hilo linawaajiri tu watu wanaotoka Darfur.

Mliyosikia ni sauti ya mtaalamu wa kilimo akimfundisha mfanyakazi mmoja wa Darfur namna ya kufunga mdodoki kwenye vijiti kwa kamba.

Mtaalamu huyo wa China anayeongea Kiarabu anaitwa Zhang Zhenjiang, pengine utastaajabu kwamba anawezaje kuongea Kiarabu hali amekuwa huko kwa nusu mwaka tu. Bw. Zhang Zhejiang alisema alilazimika kujifunza lugha ya Kiarabu kutokana na mazingira. Alisema,

"Nimelazimika kujifunza Kiarabu, ama sivyo nisingeweza kuwasiliana nao, ninapoongea Kichina hawaelewi, walipoongea Kiarabu mimi pia sikuelewa, kazi haikuweza kufanyika."

Ndani ya shamba hilo kuna wafanyakazi wa Darfur zaidi ya 20. Lakini kwa nini shamba hilo linawaajiri watu wa Darfur tu, mwendeshaji wa shamba hilo Bw. Fan alisema, kwa sababu hawakusoma sana, ni vigumu kwao kuajiriwa katika sehemu nyingine. Alisema,

"Wao ni watu waaminifu, hali yao ya maisha ni mbaya, kazi yao haihitaji sana elimu, ni vigumu kwao kupata kazi mahali pengine."

Mfanyakazi mwenye umri wa miaka 40 hivi Bw. Abudulla anatoka Darfur Magharibi, amekuwa mfanyakazi mzoefu. Alisema,

"Kazi yangu ni kufunga mdodoki kwenye vijiti ili utambae vizuri."

Kutokana na kufundishwa na wataalamu wa China, wafanyakazi hao wa Darfur wamedhibiti haraka ufundi wa kilimo cha mboga. Kutokana na muda mrefu wa kukaa pamoja na Wachina wameweza kuongea kidogo Kichina na kuweza kutaja baadhi ya majina ya mboga za Kichina.

"Buocai, Jiucai, Youcai, Donggua."

Bw. Fan alieleza kuwa, wafanyakazi hao wanafanya kazi kwa muda wa saa saba na nusu kila siku, kila mwezi wanapata dola za Marekani kiasi cha 170, wanatumia fedha hizo kutunza familia zao. Lakini watu hao wana maoni gani kuhusu bosi wao? Bw. Abudulla alisema,

"Ni mtu mzuri, anatujali sana."

Na bosi huyo anasemaje kuhusu wafanyakazi wake? Bw. Fan alisema,

"Wanafanya kazi kwa juhudi nyingi. Wanafanya vizuri kama wanavyoambiwa, hakuna haja ya kuwasimamia."

Kuhusu mipango wao wa baadaye, mfanyakazi mwenye umri wa miaka 25 Bw. Hasin alisema kwa sasa hana mpango wa kurudi nyumbani.

"Nataka kujifunza mengi zadi hapa ili nipange maisha baadaye."

Bw. Abudulla alisema ni matumaini yake kuwa ataweza kurudi nyumbani baada ya muda mfupi. Alisema,

"Ingawa hivi sasa hakuna usalama kwenye sehemu ya Darfur, lakini naona baadaye hali itakuwa salama."

Na Bw. Fan pia ana mpango wake, alisema baada ya Darfur kuwa salama ataanzisha shamba jingine huko. Alisema,

"Sote tunatamani kuwe na amani, matumani yangu ni kuanzisha shamba huko na kuwahudumia wakazi wa Darfur."