Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-03-04 16:55:17    
Mtaalamu wa Indonesia anayeshiriki kwenye ujenzi wa Bandari ya Guigang

cri

Mji wa Guigang ni mji mwenye bandari mpya kwenye mto wa ndani katika mkoa unaojiendesha wa kabila la wazhuang wa Guangxi, China. Bandari ya mji huo ni bandari kubwa zaidi kwenye mto wa ndani katika sehemu ya kusini magharibi mwa China. Katika miaka ya hivi karibuni, shughuli za uchumi zinaozohusiana na bandari hiyo zimepata maendeleo ya haraka. Bw. Richard Joost Lino kutoka Indonesia ni mmoja kati ya watu wanaoshiriki kwenye ujenzi wa bandari hiyo.

Mto Xijiang unaopita kwenye mji wa Guigang ni mto muhimu wa uchukuzi katika sehemu ya kusini mwa China. Upande wa Mashariki wa mji huo kuna mikoa ya Guangdong, Hongkong na Macau ambayo iko mbele kiuchumi, na magharibi ya mji huo ni sehemu ya magharibi ya China yenye maliasili nyingi za kimaumbile. Mji huo pia ni mji muhimu unaounganisha China na nchi za Asia ya Kusini Mashariki.

Mwezi Mei mwaka 2006 serikali ya Guigang na kampuni ya P.T.AKR ya Indonesia ziliwekeza pamoja na kuanzisha kampuni ya uchukuzi wa makontena kwenye bandari ya AKR ya Guigang. Bw. Lino ni meneja mkuu wa kampuni hiyo, pia ni mjumbe wa bodi ya wakurugenzi wa kampuni hiyo, alisema,

"Nilikuja China kwa mara ya kwanza mwezi Julai mwaka 2005, baadaye nilikuja mjini Guigang na kurudi Indonesia kila mwezi, ili kuchunguza uwezekano wa kuwekeza kwenye ujenzi wa bandari ya Guigang"

Bw. Lino ni mtaalamu wa ujenzi wa bandari kutoka Indonesia. Kila mwaka anaishi mjini Guigang kwa muda mrefu, alisema,

"Ninaishi hapa kwa muda mrefu, kila mwaka ninarudi Indonesia kwa siku 20 hivi tu, kwa sababu kazi za hapa ni nyingi."

Kutokana na kuwa hali ya hewa ya mkoa wa Guangxi inafanana na ya Indonesia, tena mawasiliano kati ya sehemu hizo mbili ni mengi tangu zamani, hivyo Bw. Lino amezoea kuishi mjini Guigang, alisema,

"Siwezi kuzungumza Kichina, lakini sioni mpweke hapa, watu wa hapa ni mwenye moyo wa urafiki, ni rahisi kuishi hapa, na ninapenda maisha ya hapa."

Bw. Lino ameishi na kufanya kazi mjini Guigang kwa karibu miaka mitatu. Anafuatilia kwa karibu maendeleo ya uchumi wa China, na amestaajabishwa na maendeleo ya kasi ya uchumi wa China, alisema,

"Naona kuwa China imepata maendeleo makubwa sana. Katika miaka 15 hadi miaka 20 iliyopita, hakuna nchi yoyote iliyoweza kuwa na athari kwa uchumi wa dunia kama China. Kwa mfano, nikiwa ni mtaalamu wa bandari, niliwasiliana na bandari za Guangzhou na Shanghai mwishoni mwa miaka ya 80 karne iliyopita. Wakati huo bandari ya Jakarta ya Indonesia ilikuwa ni ya kisasa zaidi kuliko bandari hizo mbili, lakini hivi sasa bandari hizo zimefikia kiwango cha juu duniani, ambazo ni za kisasa zaidi kuliko bandari ya Jakarta. Tunaweza kujua maendeleo makubwa ya uchumi wa China kutoka kwa bandari za China. China itakuwa sehemu muhimu ya uchumi wa dunia."

Bw. Lino anayafurahia maendeleo ya uchumi wa China, alisema maendeleo makubwa ya uchumi wa China yameihimiza kampuni ya P.T.AKR iharakishe uwekezaji mjini Guigang, alisema,

"Kampuni ya P.T.AKR imefanya shughuli nchini China kwa miaka 10, pia ina shughuli zake mjini Liuzhou. Kampuni yetu ilitambua kuwa mji wa Guigang uko kwenye sehemu muhimu ya kimkakati, ambayo iko katikati ya mkoa wa Guangxi, na umeunganisha mikoa ya Yunan, Guizhou na Sichuan ambayo haipakani ya bahari, na mkoa wa Guangdong ambao unapakana na bahari. Uchukuzi wa bidhaa kwenye mto ni njia iliyo nafuu. Kutokana na umuhimu wa mji huo, kampuni yetu ilichagua kufanya shughuli zake hapa."

Mwaka 2000 China ilianza kutekeleza mkakati wa uendelezaji wa sehemu ya magharibi, kuvutia uwekezaji, teknolojia na wataalamu kutoka nje, ili kusukuma mbele maendeleo ya watu, maliasili, mazingira, uchumi na jamii yenye uwiano katika sehemu hiyo. Eneo kubwa na maliasili nyingi za kimaumbile za sehemu ya magharibi pia vinaunga mkono maendeleo ya uchumi wa sehemu ya mashariki. Ni wazi kuwa mji wa Guigang ulioko katikati ya sehemu hizo mbili ni mahali muhimu pa mawasiliano. Bw. Lino alieleza kuwa kampuni ya uchukuzi wa makontena katika bandari ya AKR ilirekebisha mpango wa ujenzi wa zamani ili kuendana na maendeleo ya haraka ya uchumi, alisema,

"Kabla kampuni yetu haijaanza kushiriki kwenye ujenzi wa bandari ya Guigang, serikali ya mji huo ilikuwa imetunga mpango na kufanya maandalizi ya ujenzi wa bandari hiyo. Kwa mujibu wa mpango wa serikali, bandari hiyo itakuwa na uwezo wa kupakia na kupakua makontena laki 1.5 na bidhaa zisizowekwa kwenye makontena tani milioni 1.8 kwa mwaka. Baada ya kampuni yetu kushiriki kwenye mradi huo, tuna matumaini kuwa uchukuzi wa bidhaa utahitaji bandari kubwa zaidi, hivyo tumetunga mpango mpya na kujenga bandari yenye uwezo wa kupakia na kupakua makontena laki 2 na bidhaa zisizowekwa kwenye makontena tani milioni 3 kwa mwaka."

Bw. Lino amefanya juhudi kubwa kwa ujenzi wa bandari ya Guigang. Moyo wake wa kuwajibika na kazi unasifiwa na wenzake wa China. Ofisa wa serikali ya Guigang Bw. Pang Zetao alisema,

"Bw. Lino ni mtu mtulivu mwenye moyo wa urafiki, na anayefanya kazi yake kwa makini. Ana moyo wa urafiki kuhusu China, hasa mji wa Guigang. Anafanya juhudi zote kushiriki kwenye ujenzi wa bandari ya Guigang. Anapofanya kazi na kuishi pamoja na wakazi wa Guigang, tunaona kuwa amezoea kabisa hali ya mji wetu."

Bw. Lino anafurahia mazingira mazuri ya uwekezaji mjini Guigang, na ushirikiano na uungaji mkono wa serikali ya huko na wafanyakazi wa China, alisema,

"Serikali ya mji huo imetoa uungaji mkono mkubwa kwa mradi wetu. Kwa bahati nzuri tulipata fursa ya kuja hapa. Tunapohitaji msaada, serikali ya hapa huchukua hatua mbalimbali ili kutusaidia. Mradi wetu umepata maendeleo makubwa. Pia nimepata uungaji mkono wa wafanyakazi wengi, hivyo ingawa kazi yangu ina changamoto nyingi, lakini inanifurahisha."

Bw. Lino alimwambia mwandishi wetu wa habari kuwa, ingawa ameishi mjini Guigang kwa zaidi ya miaka miwili, lakini bado hawezi kuzungumza kw aKichina. Ili kueleza maoni yake kuhusu kazi na maisha yake mjini Guigang, alijifunza sentensi moja ya Kichina kutoka kwa mkalimani, alisema kwa makini,

"Ninaishi mjini Guigang kwa furaha!"