Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-03-05 15:33:14    
Mapishi ya nyama ya ng'ombe na mizizi ya mianzi

cri

Mahitaji:

Nyama ya ng'ombe gramu 200, uyoga gramu 20, figili gramu 15, mizizi ya mianzi gramu 15, pilipili hoho gramu 10, puilipili mboga gramu 10, sosi ya pilipili hoho gramu 5, vitunguu maji gram 5, vitunguu saumu gramu 5, chumvi kijiko kimoja, chembechembe za kukoleza ladha nusu ya kijiko kimoja, unga wa pilipili manga nusu ya kijiko.

Njia:

1. kata vitunguu maji, vitunguu saumu, pilipili hoho na pilipili mboga ziwe vipande. Kata mizizi ya mianzi na figili ziwe vipande, osha uyoga halafu weka kwenye maji ya moto halafu upakue. Kata nyama ya ng'ombe iwe vipande.

2. washa moto, mimina mafuta halafu tia sosi ya pilipilihoho, korogakoroga, tia vipande vya vitunguu maji, vitunguu saumu, pilipili hoho na pilipili mboga korogakoroga halafu tia vipande vya ng'ombe korogakoroga, tia vipande vya mizizi ya mianzi na figili, korogakoroga, tia chumvi, chembechembe za kukoleza ladha, unga wa pilipili manga korogakoroga, ipakue. Mpaka hapo kitoweo hiki kiko tayari kuliwa.