Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-03-05 18:51:36    
China yashiriki kwenye maonesho ya teknolojia ya mawasiliano ya habari duniani

cri

Maonesho makubwa ya sayansi na teknolojia ya duniani, ambayo ni maonesho ya teknolojia ya upashanaji habari ya Hannnover ya Ujerumani (CeBIT), yalifunguliwa tarehe 4 mwezi Machi, maonesho hayo yenye eneo la mita za mraba laki 2.4, yalishirikisha kampuni na viwanda 584 kutoka nchi na sehemu 77 za duniani. Ofisa mmoja husika wa China alisema, bidhaa nyingi zaidi zinazooneshwa na China kwenye maonesho hayo ni za elektroniki, hususan zile za kuongoza safari za magari na za video na audio zinazowekwa kwenye magari zinafuatiliwa na watu wengi. Kampuni na viwanda vya China vinapata faida kubwa kila mwaka kwenye maonesho hayo, na vimepanua maonesho yao kutokana na kuongezeka kwa shughuli zao za biashara. Kwa mfano, kampuni mbili maarufu za China, "Hua Qi" na "Huawei" zimepanua maeneo yao kwenye maonesho hadi kufikia mita za mraba zaidi ya 200. Msimamizi mkuu wa teknolojia wa kampuni ya teknolojia ya tarakimu ya Hu Qi,, Bw. Cheng Gang alisema,

"Kushiriki kwetu kwenye maonesho hayo mwaka huu ni hatua moja muhimu ya kwenda kwenye masoko ya dunia kwa bidhaa zetu zenye nembo ya Patrioc. Tulianza kushiriki kwenye maonesho hayo tangu miaka michache iliyopita, tofauti yetu kati ya mwaka huu na ya zamani ni kuwa safari hii tumeweka malengo kadhaa muhimu. La kwanza ni kufanya matangazo kuhusu kamera zetu za kamera zenye teknolojia ya kitarakimu, kamera zetu za aina hiyo zimepata maendeleo makubwa nchini China katika miaka ya karibuni, hivi sasa tunataka kuzipeleka kwenye masoko ya dunia, kushiriki kwetu kwenye maonesho safari hiyo ni hatua muhimu ya kwanza."

Vitendo vya kampuni na viwanda vya China kwenye maonesho ya CeBIT katika miaka ya karibuni, vinasifiwa na watu hata na washindani wake. Kiongozi wa kampuni moja ya kompyuta ya Ujerumani Bw. Ralf Bachmann alipohojiwa na mwandishi wetu wa habari alisema, alifuatilia sana maendeleo ya maonesho ya China ya mwaka huu, anaamini kuwa sekta ya teknolojia ya mawasiliano ya habari ya China itapata maendeleo ya kushangaza. Alisema,

"Kutokana na maendeleo makubwa ya sekta ya mawasiliano ya habari ya China katika miaka ya hivi karibuni, mwaka 2008 China inaweza kudumisha maendeleo yake mazuri, ni dhahiri kuwa ninachosema siyo kuhusu kompyuta peke yake, China imepata maendeleo makubwa katika maeneo mbalimbali. Hii inaonesha kuwa sekta ya teknolojia ya mawasiliano ya habari ya China itakuwa na mstakabali mzuri katika siku za baadaye."

Habari alizopata mwandishi wetu wa habari kwenye maonesho hayo zinasema, kuna sababu tatu ya kuongezeka kwa kampuni na viwanda vinavyoshiriki kwenye maonesho ya Hanover. Kwanza, vinaweza kupata oda kwenye maonesho, hususan kwa kampuni na viwanda vidogo na vya wastani; Pili, vinaweza kufanya watu wengi zaidi kuvifahamu, na kuonesha uwezo wao kwa wenzi wa ushirikiano wa siku za baadaye wa Ulaya; Tatu, vinaweza kufahamu hali mpya ya maendeleo ya sekta ya teknolojia ya mawasiliano ya habari. Kuhusu hayo, meneja wa uhusiano na nje wa kampuni moja ya vyombo vya umeme ya mji wa Shenzhen, Bw. Xiong Jiang alisema,

"Katika mwaka uliopita, kampuni yetu ilishiriki kwa mara ya kwanza kwenye maonesho hayo na iliagiza eneo la mita za mraba 100, tulifurahi kuona watu wengi walifahamu bidhaa zetu. Kwa hiyo mwaka huu tumepanua zaidi eneo la maonesho yetu, tunatarajia kupata wakala wengi zaidi wa mauzo ya bidhaa zetu na kupata wenzi wa ushirikiano."

Kwa kampuni na viwanda vingi vya China, lengo lao kubwa kabisa ni kuweza kuingia kwa haraka kwenye masoko ya dunia. Kwenye maonesho hayo, kampuni maarufu ya kompyuta ya Huashuo kutoka sehemu ya Taiwan, China ilionesha kompyuta za lap top, ambayo baadhi ya vitu vyake vilitengenezwa na mali-ghafi ya mianzi. Kompyuta hiyo inayounganisha teknolojia ya kisasa na utamaduni wa jadi wa China licha ya kuendana na kauli-mbiu ya maonesho ya mwaka huu ya "teknolojia ya mawasiliano ya habari isiyo na uchafuzi wa mazingira", ina umaalumu wa utamaduni wa jadi ya China.