|
Wizara ya mambo ya nje ya Iraq tarehe 11 ilitangaza kuwa wajumbe wa nchi hiyo na Marekani wameanza kufanya mazungumzo kuhusu uhusiano wa kudumu kati ya nchi hizo mbili. Kwenye mazungumzo tatizo sugu ni suala la jeshi la Marekani nchini Iraq. Wachambuzi wanaona kuwa mazungumzo hayo yanafanyika wakati unapokaribia mwaka wa tano tokea vita vya Iraq vizuke, yanafuatiliwa sana.
Ukweli ni kwamba mazungumzo kati ya pande mbili yameanza mapema tokea mwezi Agosti mwaka jana. Mazungumzo ya hivi sasa ni makubwa kati ya mazungumzo mengi yaliyopita. Tarehe 26 Novemba mwaka jana Rais George Bush wa Marekani na waziri mkuu wa Iraq walisaini waraka wa Nuri al-Maliki ambao uliamua kufanya mazungumzo kuhusu masuala ya siasa, uchumi na usalama kati ya nchi hizo mbili. Kwa mpango mazungumzo hayo yatamalizika mwezi Julai mwaka huu na kutoa taarifa rasmi mwezi Agosti.
Tarehe 20 Machi mwaka 2003 bila ya idhini ya Umoja wa Mataifa nchi za Marekani na Uingereza zilianzisha vita vya Iraq kwa nia ya kuupindua utawala wa Saddam Hussein. Mwezi Oktoba mwaka huo Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilipitisha azimio No. 1511 likiidhinisha kuunda jeshi la muungano lililoongozwa na Marekani na kuingia nchini Iraq ili kulinda usalama wa Iraq, na hii inamaanisha kuhalalisha jeshi la Marekani kuwepo nchini Iraq. Tokea hapo Baraza la Usalama lilipitisha azimio No. 1790 likiamua kurefusha muda wa jeshi hilo la muungano nchini Iraq mpaka mwisho wa mwaka huu. Kutokana na muda huo kukaribia kumalizika, Marekani imekuwa ikijitahidi kutia saini na Iraq ili kuliwezesha jeshi la Marekani kuendelea kubaki nchini humo. Kwa hiyo Marekani inatumai kuzungumza zaidi kuhusu suala la kuendelea kubaki kwa jeshi la Marekani, na huku ikiweka kanuni mfululizo kuhusu uhusiano kati ya nchi hizo mbili.
Marekani inatumai kudumisha muda wa kuwepo kwa jeshi la Marekani nchini Iraq, ili kuhakikisha manufaa yake ya kisiasa na ya kijeshi katika kanda ya Mashariki ya Kati. Rais George Bush aliwahi kusema kwamba Marekani haitaondoa jeshi lake kabla ya watu wa Iraq kuwa na uwezo wa kujilinda. Lakini baadhi ya vyombo vya habari vinaona kuwa kwenye mazungumzo hayo pengine Marekani itarekebisha idadi ya askari wa jeshi hilo. Kabla ya hapo serikali ya Iraq iliwahi kuishauri Marekani kuwa mambo ya usalama nchini Iraq yashughulikiwe na jeshi la Iraq peke yake, na jeshi la Marekani likae nje ya miji nchini humo, na wakati huo jeshi la Marekani lipunguze askari hadi kufkia elfu 50 kutoka laki 1.6 la sasa, na Marekani haina pingamisi kuhusu ushauri huo. Waziri wa ulinzi wa Marekani Bw. Robert Gates mwezi uliopita kwenye bunge alisema, kwenye makubaliano kati ya Marekani na Iraq serikali ya Rais George Bush haitawajibika kuilinda Iraq. Na Bw. George Bush mwenyewe pia alisema, ingawa Marekani haitaki kujenga kituo cha kudumu cha kijeshi nchini Iraq, lakini kuhakikisha kuwepo kwa jeshi la Marekani kunalingana na manufaa ya pande mbili. Wachambuzi wanaona kuwa kama ushauri huo wa Iraq ukitimizwa, Marekani itapata manufaa ya aina tatu, yaani jeshi la Marekani litaondoka nchini Iraq kwa sehemu; pili jeshi la Marekani litapata ruhusa ya kubaki nchini Iraq kwa muda mrefu, sawa na kupata kituo cha kijeshi cha kudumu nchini humo; na tatu ni kupata manufaa mengi katika ukarabati wa nchi ya Iraq.
Lakini, ndani ya serikali ya Iraq kuna maoni tofauti kuhusu kubakiza jeshi la Marekani kwa muda mrefu. Baadhi ya maofisa wanaona kuwa Iraq inapaswa kujenga uhusiano wa kimkakati na Marekani na kupata "uhakikisho wa usalama" kama jeshi la Marekani likiendelea kukaa nchini humo. Lakini maofisa wengi zaidi wanaona kuwa ni lazima jeshi la Marekani liondoke nchini Iraq.
Mazungumzo ya suala la kubaki kwa jeshi la Marekani nchini Iraq yatakuwa magumu na pengine yatakuwa ya muda mrefu na ya "vuta nikuvute". Vyombo vya habari vinaona kuwa mazungumzo yanayofanyika sasa ni muhimu kwa pande mbili na pia kwa mustakabali ya kanda ya Mashariki ya Kati.
|