Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-03-12 19:34:20    
Mapishi ya nyama ya bata

cri

Mahitaji

Nusu ya bata mmoja, vitunguu maji gramu 5, tangawizi gramu 5,mvinyo wa kupikia vijiko viwili, mchuzi wa sosi vijiko viwili, chumvi kijiko kimoja, sukari kijiko kimoja, pilipili hoho gramu 2

Njia

1. osha nyama ya bata halafu weka kwenye sufuria yenye maji, chemsha kwa dakika 5 ipakue na uikaushe.

2. mimina mafuta madogo kwenye sufuria, weak nyama ya bata kwenye sufuria, ikaange mpaka iwe rangi ya hudhurungi, mimina mvinyo wa kupikia na mchuzi wa sosi, ipakue.

3. chemsha maji kwenye sufuria, weka bata kwenye sufuria tia vipande vya vitunguu maji, tangawizi, pilipili hoho, chumvi na sukari, chembechembe za kukoleza ladha. Baada ya kuchemka punguza moto baada ya dakika 50 ipakue. Mpaka hapo kitoweo hiki kiko tayari kuliwa.