Mkutano wa wakuu wa nchi za Umoja wa Ulaya wa majira ya spring, ambao utafanyika kwa siku mbili, umepangwa kuanza usiku wa tarehe 13 kwenye makao makuu ya Umoja wa Ulaya huko mjini Brussels. Mkutano huo utafuatilia zaidi mambo ya uchumi yakiwemo masuala mawili ya mpango wa utekelezaji wa "mkakati wa Lisbon" katika miaka mitatu ijayo, pamoja na hatua za kukabiliana na mgogoro kwenye soko la fedha.
Mkutano wa wakuu wa nchi za Umoja wa Ulaya wa majira ya Spring ya mwaka huu unakabiliwa na hali mbaya ya uchumi. Kwa upande mmoja, kutokana na kuathiriwa na kupanda kwa bei ya mafuta na thamani ya Euro, uchumi kwenye eneo linalotumia Euro, ambao ulidumisha ongezeko kwa miaka miwili mfululizo, ulianza kupungua kwa kasi katika robo ya nne ya mwaka jana, na kiasi cha kuongezeka kwa uchumi kwa mwaka huu, pia kinaelekea kupungua na kuwa 1.8% ikilinganishwa na kile cha 2.2% kilichotarajiwa. Kwa upande mwingine, mgogoro wa mikopo ya ngazi ya pili wa nchini Marekani, ambao umesababisha msukosuko wa masoko ya fedha, umezuia vibaya uwekezaji na ununuzi wa bidhaa katika nchi za Umoja wa Ulaya, hali hiyo imekwamisha ongezeko la uchumi wa Umoja wa Ulaya. Kutokana na hayo jukumu moja la haraka la mkutano huo wa Umoja wa Ulaya ni kutafuta njia nzuri ya kutatua matatizo ya uchumi yaliyoko hivi sasa barani Ulaya.
"Mkakati wa Lisbon" kuhusu mstakabali wa uchumi wa Umoja wa Ulaya ni ajenda ya kwanza kujadiliwa kwenye mkutano huo wa wakuu wa nchi. Mpango wa "mkakati wa Lisbon", ambao ulitungwa mwaka 2000, una lengo la kuufanya Umoja wa Ulaya uwe na nguvu kubwa zaidi ya ushindani katika dunia kuliko Marekani kabla ya mwaka 2010. Kutokana na kushindwa kuutekeleza vizuri mpango huo, Umoja wa Ulaya ulifanya marekebisho kuhusu mpango huo katika mwaka 2005, na kuweka kuhimiza ongezeko la uchumi na kutoa nafasi nyingi zaidi za ajira kuwa lengo jipya la maendeleo ya uchumi kabla ya mwaka 2010. "Mkakati wa Lisbon" uliozinduliwa upya ulihimiza kwa nguvu maendeleo ya uchumi wa Umoja wa Ulaya katika kipindi cha kwanza cha utekelezaji cha miaka mitatu, mwaka jana ongezeko la uchumi wa Umoja wa Ulaya lililizidi lile la Marekani kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2001, ambapo kiasi cha ukosefu wa ajira kilipungua kwa mfululizo. Katika wakati huu, ongezeko la uchumi wa Marekani linapungua, Euro inakabiliwa na shinikizo la kupanda thamani, katika tarehe 26 mwezi uliopita kiasi cha ubadilishaji wa dola za kimarekani kwa Euro kilifikia 1 kwa 1.5, na thamani ya Euro iliongezeka kwa mfululizo, hali ambayo inaathiri sana usafirishaji bidhaa wa Umoja wa Ulaya kwa nchi za nje. Isitoshe kupanda kwa bei ya mafuta ya petroli kunaongeza kupungua kwa uchumi wa Umoja wa Ulaya, na utekelezaji wa "mkakati wa Lisbon" katika kipindi kijacho cha miaka mitatu unakabiliwa na changamoto kubwa. Kutokana na matatizo yanayotokea hivi sasa katika maendeleo ya uchumi, kamati ya Umoja wa Ulaya imetunga mpango wa utekelezaji wa "mkakati wa Lisbon" kati ya mwaka 2008 na mwaka 2010 katika mwezi Desemba mwaka uliopita, inaushuri Umoja wa Ulaya uhimize nchi wanachama wake kuimarisha mageuzi ya uchumi katika miaka mitatu ijayo kuhusu maeneo manne ya elimu na uvumbuzi, uboreshaji wa mazingira ya biashara, mageuzi ya soko la nguvu-kazi, na nishati na mabadiliko ya hali ya hewa, tena ilitoa hatua halisi kadhaa. Mkutano huo wa wakuu wa nchi utajadili na kupitisha mpango huo wa utekelezaji na kuongeza nguvu ya maendeleo ya uchumi wa Umoja wa Ulaya katika siku za baadaye.
Mgogoro wa masoko ya fedha ya duniani, ambao umeathiri maendeleo ya uchumi wa Umoja wa Ulaya, ni suala lingine linalofuatiliwa na mkutano huo. Hivi karibuni benki kuu 5 za nchi za magharibi zikiwemo kamati ya akiba ya shirikisho la Marekani na benki kuu ya Ulaya zilishirikiana kwa mara ya pili kuingiza fedha nyingi kwenye mzunguko wa fedha ili kuhamasisha mzunguko wa fedha kwenye masoko na kulikabiliana na tatizo la kupungua kwa utoaji mikopo. Viongozi wa Umoja wa Ulaya walisema mara nyingi kuwa hali ya jumla ya uchumi wa Umoja wa Ulaya ni nzuri, hivyo umoja huo hautaifuata Marekani kuchukua hatua za kuhimiza ongezeko la uchumi ikiwemo ya kupunguza faida ya fedha zilizowekwa benkini, na utatilia mkazo kuboresha masoko ya fedha.
|