Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-03-14 13:53:33    
Botswana yataka kuimarisha ushirikiano kati yake na China katika sekta za uchumi, biashara na utamaduni

cri

Balozi wa Botswana nchini China hivi karibuni alipohojiwa na mwandishi wa habari wa shirika la habari la China?Xinhua, alisema, Botswana inataka kuimarisha ushirikiano kati yake na China katika sekta za uchumi na biashara, hasa katika utengenezaji wa vitu vya vioo, vitu vya ngozi, utengenezaji wa vito na nguo. Balozi huyo alisema anawasiliana na wafanyabiashara wengi wa China, hasa wafanyabiashara kutoka mkoa wa Zhejiang. Amewataka wafanyabiashara wawekeze nchini Botswana, ili kuimarisha ushirikiano kati ya China na Botswana, na kusaidia kutatua tatizo la ajira nchini Botswana.

Ingawa Botswana ina maliasili nyingi za madini, lakini ukosefu wa fedha unazuia maendeleo ya sekta nyingi. Balozi wa Botswana nchini China alijulisha kuwa, ili kuvutia uwekezaji kutoka nchi za nje, Botswana inachukua hatua maalumu za kuhimiza uwekezaji. Kwa mfano kodi ya viwanda vya utengenezaji ni asilimia 15, ni kodi ya chini kabisa katika nchi za kusini mwa Afrika.

Tangu mwaka 1975 zilipoanzisha uhusiano wa kibalozi, China na Botswana zinadumisha uhusiano mzuri wa ushirikiano, mwaka 2005 thamani ya biashara kati ya nchi hizo iliongezeka na kufikia dola za kimarekani milioni 62.52 kutoka dola za kimarekani laki tatu hadi laki tano za mwaka 1982. China inauza nguo na bidhaa za umeme nchini Botswana, na Botswana inauza alamasi kwa China.

Balozi huyo alisema China imeipatia Botswana misaada mingi. Alijulisha kuwa kampuni ya maendeleo ya Bwawa la Magenge Matatu ya China inafanya ushirikiano na Botswana, na kujenga bwawa ili tatizo la ukosefu wa maji wakati wa ukame litatuliwe. Licha ya hayo kampuni nyingi za China zinashiriki kwenye ujenzi wa barabara, hospitali, shule, na mikahawa nchini Botswana?Bidhaa ndogo ndogo za China pia zinakaribishwa nchini Botswana, na wakazi wengi wanazipenda.

China na Botswana si kama tu zinaimarisha biashara kati yao, bali pia zinazidisha mawasiliano ya utamaduni kati yao. Botswana ikiwa ni nchi inayopokea watalii wengi barani Afrika, asilimia 38 ya ardhi nchini Botswana ni sehemu ya uhifadhi wa wanyama pori. Botswana ina mbuga tatu za wanyama. Mwaka 2007 Botswana ilishiriki kwa mara ya kwanza kwenye mkutano wa biashara ya utalii wa kimataifa wa China uliofanyika mjini Kunming, China, pia iliwaalika waandishi wa habari kwenda Botswana kutembelea na kupiga picha, ili kuwavutia watalii wengi zaidi wa China.

Kutokana na kukaribishwa kwa lugha ya Kichina kwenye nchi mbalimbali duniani siku hadi siku, vijana wa Botswana wanavutiwa na utamaduni wa China. Tarehe 23 mwezi Oktoba mwaka 2007 Chuo kikuu cha Botswana na kikundi cha uongozi wa kueneza lugha ya Kichina cha China vilisaini makubaliano kuhusu ushirikiano katika kujenga chuo cha Confucius, na kujenga daraja la mawasiliano kati vijana wa China na Botswana. Imefahamika kuwa sasa hivi wanafunzi 50 wa Botswana wanasoma nchini China.

****************************

Kampuni ya Huawei ya China na kampuni ya Telekom ya Rwanda zimesaini makubaliano yenye thamani ya dola za kimarekani milioni 35. Kutokana na makubaliano hayo, kampuni ya Huawei ya China itajenga na kuboresha miundo mbinu kadhaa ya mawasiliano ya simu kwa ajili ya kampuni ya Telekom ya Rwanda.

Baada ya kukamilishwa kwa mradi huo, mtandao wa mawasiliano ya simu wa kampuni ya Telekom ya Rwanda utawasiliana na mtandao wa simu za mkononi wa Uganda, mpaka wakati ambapo kampuni ya Telekom ya Rwanda itakapoweza kutoa huduma ya simu za mkononi nchini Uganda, wakati huo huo miundo kadhaa ya simu za nyumbani ya kampuni ya Telekom ya Rwanda pia itaboreshwa.

Habari nyingine zimesema ujumbe wa biashara wa China ulioundwa na kampuni kadhaa za China mwezi Februari ulisaini makubaliano yenye thamani ya dola za kimarekani milioni zaidi ya 200 na kampuni za Zambia. Kampuni za nchi hizo mbili pia zilifikia maoni mengi ya ushirikiano wenye thamani ya dola za kimarekani milioni 300.

Mkurugenzi wa shirikisho la biashara kati ya Zambia na China kwenye sherehe ya kusaini makubaliano aliisifu China kwa uungaji mkono na misaada yake kwa maendeleo ya uchumi barani Afrika. Alisema kusainiwa kwa makubaliano hayo ni kutimiza ahadi yake kwa China kwenye mkutano wa wakuu wa Baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika uliofanyika hapa Beijing mwaka 2006. Mkurugenzi huyo alisema, katika mchakato wa China kubadilika kuwa nchi yenye nguvu ya uchumi kutoka nchi maskini, bila shaka ina uzoefu mkubwa. Alieleza imani yake kuwa kampuni za Zambia zitapata maendeleo ya kasi kutokana na ushirikiano kati yao na kampuni za China.

********************

China na Togo mwezi Februari zilisaini makubaliano saba ya ushirikiano wa uchumi na teknolojia. Kutokana na makubaliano hayo, China itatoa misaada kwa miradi iliyokubaliwa na serikali za nchi hizo mbili, na kutokana na maombi ya Togo, China imekubali kutoa vifaa vyenye thamani ya Yuan milioni 5 kwa Togo. Licha ya hayo chini ya mfumo wa mkutano wa wakuu wa Baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika uliofanyika hapa Beijing mwaka 2006, China imekubali kuisaidia Togo kujenga kituo cha utoaji wa mafunzo ya ufundi wa kilimo, shule mbili na kituo cha kupambana na ugonjwa wa malaria.

Habari nyingine zinasema wataalamu wa kilimo wa China wanaoisadia Senegal hivi karibuni walifanya semina kuhusu ujuzi wa upandaji wa mpunga, na kutafuta njia ya kuongeza kiasi cha uzalishaji wa mpunga nchini Senegal, na kutimiza lengo la kujitosheleza kwa mpunga. Wataalamu wa China waliona kuwa kama ardhi ya sehemu ya mto Senegal itatumika kikamilifu, Senegal itaweza kujitosheleza kwa mpunga.

Wataalamu wa China waliona kuwa ili kuongeza kiasi cha uzalishaji wa mpunga, ni lazima kubadilisha njia ya upandaji wa mpunga, inapaswa kutumia kikamilifu maji ya mto Senegal, kupanda mpunga kwa mashine. Senegal ni nchi yenye mahitaji makubwa ya mpunga, kila mwaka inahitaji tani laki 9 za mpunga, kati ya hizo tani laki 6 zinaagizwa kutoka nchi za Asia, na serikali kila mwaka inatoa dola za kimarekani milioni 100 kununua mpunga kutoka nchi za nje.

Idhaa ya kiswahili 2008-03-14