Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-03-14 20:07:35    
Mwelekeo wa uchaguzi wa bunge la Iran

cri

Uchaguzi wa 8 wa bunge la Iran utafanyika rasmi tarehe 14, lakini inaonekana kuwa watu hawafuatilii sana uchaguzi huo. Wachambuzi wanasema, kwa kuwa watu wengi wa kundi la mageuzi wamefutiwa haki ya kushiriki kwenye uchaguzi huo, hivyo kundi la wahafidhina bado watapata viti vingi zaidi, na kuendelea kudhibiti bunge. Bunge la Iran ni chombo cha ngazi ya juu kabisa cha utungaji wa sheria. Bunge hilo lina baraza moja tu, kuna viti 290 bungeni, na kipindi cha madaraka ya kila mbunge ni miaka minne. Ushidani kwenye uchaguzi huo utakuwa kati ya makundi matatu ya kisiasa, yaani kundi la "The United Principlist Front" na kundi la "The Inclusive Coalition" la wahafidhina na kundi la "The Reformist Alliance" la wanamageuzi. Lakini theluthi moja ya wagombea wa kundi la mageuzi walifutiwa haki ya kushiriki kwenye uchaguzi huo, hivyo wachambuzi wanaona kuwa, kundi la wanamageuzi halitashinda na kundi la wahafidhina litaendelea kudhibiti bunge.

Ingawa sheria ya uchaguzi wa bunge inaruhusu wagombea kufanya kampeni kwa njia mbalimbali zikiwemo kuitisha mikutano na waandishi wa habari, kwa kupitia vyombo vya habari vya jadi, na kwenye mtandao wa Internet, lakini kamati ya usimamizi wa katiba iliondoa sifa ya wagombea wa kundi la mageuzi kabla ya wakati, kitendo hicho bila shaka kimepunguza ushindani wa kundi la mageuzi, na kulisaidia kundi la wahafidhina kuendelea kudhibiti bunge. Watu hawana hamu kubwa ya kushiriki kwenye uchaguzi huo, hasa huko Tehran, mji mkuu wa Iran. Ingawa hakuna upinzani wa wazi, lakini hali ya kimya na uzembe wa watu inayoonekana nadra huenda kinaonesha kuwa hawajaridhika.

Baada ya rais Mahmoud Ahmadinejad kuingia madarakani mwaka 2005, kundi la mageuzi linaloongozwa na rais wa zamani Bw. Mohammad Khatami na kundi la upole linaloongozwa na mwenyekiti wa kamati ya maslahi ya nchi ya Iran Bw. Akbar Hashemi Rafsanjani hawana uwezo. Tarehe 4 mwezi Septemba mwaka jana, Bw. Rafsanjani alichaguliwa kuwa mwenyekiti wa Baraza la wataalam wa Iran, badala ya kiongozi wa kidini wa kundi la wahafidhina Bw. Ali Meshkini kufariki dunia. Jambo hilo lilichukuliwa kuwa ushindani kati ya kundi lenye msimamo wa kati na kundi la wahafidhina, na vyombo vya habari vya Iran pia viliona kuwa, kuchaguliwa kwa Bw. Rafsanjani kulichukuliwa kuwa ni "maendeleo makubwa" ya maisha ya kisiasa ya Iran.

Lakini baada ya miezi kadhaa, kundi la mageuzi halikuweza kufanya kampeni kubwa, na uwezo wake wa ushindani ulipungua. Wagombea wa kundi la mageuzi watakaoshiriki kwenye uchaguzi walikadiria kuwa, kundi la mageuzi linaweza kupata viti 50 tu kati ya viti 290.

Lakini jambo moja linastahili kufuatilia, yaani uchaguzi huo utawafanya wanachama wengi zaidi wa kundi la wanamgambo wa mapinduzi ya kiislam waingie bungeni, na idadi ya waumini wa dini bungeni itapungua. Wachambuzi wanaona kuwa, mabadiliko hayo ni "alama muhimu", kwani wanachama hao wote ni wa kundi la wahafidhina. Rais Mahmoud Ahmadinejad siku zote ana msimamo mkali katika suala la nyuklia la Iran, hivyo uungaji mkono wake unapungua siku hadi siku, na katika maskani yake Tehran, watu wanapinga sera yake ya "kutoshirikiana" na jumuiya ya kimataifa.

Lakini uchaguzi huo wa bunge mwishoni utanufaisha kundi la wahafidhina. Japo bunge halitadhibitiwa na serikali ya Mahmoud Ahamadinejad, lakini litamtii kiongozi wa ngazi ya juu Ayatollah Ali Khamenei wa kundi la wahafidhina, na katika siku za baadaye pia halitatoa changamoto kubwa kwa sera za mambo ya ndani na nje za rais Mahmoud Ahmadinejad.